Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Hilo linafahamika tangu Malawi inapata uhuru mwaka 1964. Kwa taarifa yako mwaka 1967, Kamuzu Banda aliwahi kulianzisha na Nyerere akamtuliza.
Wewe ulishaona wapo, kumtuliza mtu, ikawa ni mkataba wa mpaka? Sawa, Nyerere alimtuliza, then what? Hiyo ndo ilitatua mgogoro wa mpaka? Kutulizana is nothing; mkataba na makubaliono ndo kila kitu.
 
Hapo umefungua page ya Malawi, ukienda page ya Tanzania pia utakuta info za ziwa hilo zik8nasibishwa na Rasilimali zilizopo Tanzania hivyo kuwa mpole. Ziwa tunalo na tunatamba nalo.
Hata mimi sitaki Tanzania iporwe ziwa Nyasa. Ila kutaka kwangu, hakuna maana yoyote, endapo hatuna makubaliono na Malawi kutatua mgogoro wa huu mpaka. Una acknowlwdge kwamba kuna dispute ya mpaka; kwahiyo hiyo dispute Tanzania haiwezi kuitumia kama karata ya kujihakikishia umiliki wa hilo ziwa. Kuna siku hiyo dispute itaisha, na inaweza kuwa ni kwa advantage kwa wamalawi, ikiwa Tanzania haitachukua jukumu la kufanya mkataba na makubaliono.

Tatizo ninaloliona, ni Tanzania kujihesabia haki pasipo na makubaliano na mkataba. Hilo ndo ombwe linalotugharimu, kama wewe unavyoamini kwamba ziwa ni lako, lakini nikikuuliza kwa mkataba upi, huwezi kuniambia.
 
Kwa ramani ambazo Malawi wanazitumia ziwa Nyasa linaonekana hivyo na wao wanaliita Lake Malawi. Lakini kwa ramani za mitaala ya Tanzania ziwa Nyasa limegawanyika kwa dotted lines (-----). Ukiona dotted lines kwenye ramani maana yake hiyo border iko kwenye dispute.

Hata Malawi kipindi cha Muluzi kurudi nyuma walikuwa wanaweka dotted lines, lakini alipokuja yule Rais Mwanamama wa kwanza wa Malawi, Joyce Banda akaja na ajenda ya kuwa ziwa ni la Malawi pekee kwa mujibu wa Heligoland Treaty ya 1870.

Uzembe wa Mwingereza kuweka mipaka hauwezi kuihalalishia Malawi kuwa ziwa lote ni lake.

Hebu fikiria bandari ya Mbambabay iliyojengwa na Wajerumani mwaka 1981 itakuwa ilijengwa ili itumie maji gani?

Common sense inakataa na ndiyo maana hata Kamuzu Banda Rais wa kwanza wa Malawi aliufyata. Bakili Muluzi wala hakuwahi kuliongelea
Kwani mtaala wa Tanzania ni international document? Kwamba, kama mtaala wa Tanzania unatambua umiliki wa ziwa nyasa, basi na dunia nzima inatambua hivo?

Na pia, uzembe wa mwingereza haumpi Tanzania haki ya kupitisha mpaka katikati ya ziwa.

Achana na common sense kwenye hili suala; hili suala ni la mikataba na makubaliano. Issue ya mjerumani kujenga bandari bamba bay, haina maana yoyote ku justify ownership. May be walijenga kwa makubaliono fulani. Itabidi tuwafuate tuwaulize ilikuwaje wakajenga hiyo bandari pale. Ni mwanzo mzuri, tukianza kuwadodosa wajerumani, watakuwa ni hizi nyaraka.
 
Kwani mlivyoambiwa tuna vita ya kiuchumi na mabeberu hamjaelewa

Kuwa Tanzania inawindwa Kila Kona au unadhani kwamba hao CIA hawajui walifanyalo hi ni mipango mikakati ya kuishambulia Tanzania kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia na wanajua kuwa hapo katika ziwa Nyasa Kuna mgogolo na lazima wao watakuwa upande wa Malawi

Ila watafeli alafu wenyewe watashangaa hi ndio Tanzania
Hata mimi naamini kuna agenda kutoka kwa nchi za magharibi. Ila, hiyo agenda haiwezi kufeli kwa imani, kama unavyotaka kutuaminisha.
 
Hata mimi sitaki Tanzania iporwe ziwa Nyasa. Ila kutaka kwangu, hakuna maana yoyote, endapo hatuna makubaliono na Malawi kutatua mgogoro wa huu mpaka. Una acknowlwdge kwamba kuna dispute ya mpaka; kwahiyo hiyo dispute Tanzania haiwezi kuitumia kama karata ya kujihakikishia umiliki wa hilo ziwa. Kuna siku hiyo dispute itaisha, na inaweza kuwa ni kwa advantage kwa wamalawi, ikiwa Tanzania haitachukua jukumu la kufanya mkataba na makubaliono.

Tatizo ninaloliona, ni Tanzania kujihesabia haki pasipo na makubaliano na mkataba. Hilo ndo ombwe linalotugharimu, kama wewe unavyoamini kwamba ziwa ni lako, lakini nikikuuliza kwa mkataba upi, huwezi kuniambia.
Makubaliano yashafikiwa na hiyo dispute imeshaisha bwashee, ziwa ni mali ya wote.
 
Wakati wenye mamlaka wakiwa busy kuponya majeraha ya MO29, kwa kuyakanusha na kupindua taarifa za ukweli; wenye dunia yao huko duniani, hawachoki kuitafiti dunia na ku shape geopolitics kulingana na taarifa sahihi za kiuchunguzi.

Jana niliingia Instagram, kwenye post ya CIA, nikakuta wameweka taarifa nzuri nzuri kuhusu Ziwa Malawi (sisi tunalijua kama ziwa Nyasa), ikiwemo hii kwamba: ni ziwa lenye fish species nyingi kuliko ziwa lolote lile duniani, na ni ziwa la nne kubwa duniani lenye fresh water.

Binafsi hiyo ya fresh water nilikuwa naijua, ila hii ya kwamba Ziwa Nyasa lina species nyingi kuliko ziwa lingine lolote duniani, sikuwahi kuijua.

Kwa sababu kwa wenzetu CIA pia ina muunganiko wa kikazi na Makampuni ya kimarekani; nimejiuliza itakuwaje pindi makampuni ya kimarekani yatakapoanza uwekezaji wao pale Ziwa Malawi. Je, hii hatua haita chechemua mgogoro mpya wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi?

Kilichonishangaza zaidi ni kwamba: kwenye post hiyo ya CIA, hawakugusia kabisa kwamba Ziwa Malawi lipo pia nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa. Na waligongelea msumari kwa kusema, "Malawi's Lake Malawi." Je, haiwezi kuwa ni turufu kwa Malawi, kwamba mataifa makubwa yanajua tayari kwamba Ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pia ni mali ya Malawi? Na kwa sababu tayari Tanzania kupitia CCM imewabagaza wazungu; je, Tanzania itaweza kujihesabia haki ya umiliki wa ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pindi mgogoro ukirudi upya, kama dalili zinavyoonesha?

View attachment 3518251

Wenu,
MC
waje tuone, ziwa lina mafuta na gas ma madini kadhaa. Tukiona vipi tutawakabidhi Urusi wachimbe mafuta kule ziwani kama tulivyowapa kuchimba Uranium. Urusi itatupatia mitambo ya S500 tujilinde na wahuni. Unadhani tuliwapa urusi kuchimba uranium kwa bahati mbaya tu?
 
Kwani mtaala wa Tanzania ni international document? Kwamba, kama mtaala wa Tanzania unatambua umiliki wa ziwa nyasa, basi na dunia nzima inatambua hivo?

Na pia, uzembe wa mwingereza haumpi Tanzania haki ya kupitisha mpaka katikati ya ziwa.

Achana na common sense kwenye hili suala; hili suala ni la mikataba na makubaliano. Issue ya mjerumani kujenga bandari bamba bay, haina maana yoyote ku justify ownership. May be walijenga kwa makubaliono fulani. Itabidi tuwafuate tuwaulize ilikuwaje wakajenga hiyo bandari pale. Ni mwanzo mzuri, tukianza kuwadodosa wajerumani, watakuwa ni hizi nyaraka.
Mimi nakupa fact wewe unasema maybe? Sijui umri wakoa lakini huko juu kuna mahali nimeongelea suala la International rparian rights.
Kwa Ziwa Nyasa, riparian law:
✔ Inatambua ziwa kama rasilimali ya pamoja
✔ Inazuia umiliki wa upande mmoja
✔ Inalazimisha mashauriano kabla ya miradi mikubwa
❌ Lakini haitoi mpaka wa mwisho kisheria bila makubaliano au hukumu
 
Ngoja vita itokee ya kugombania Hilo ziwa Ccm waone Raia watakavyokuwa upande wa Malawi, majeshi yetu yatapigwa asubuhi mapema kabisa.
Naunga mkono hoja. Jtwz tuliwaheshimu na kuwaamini ila kwa tulichokiona kumammae heri tusapoti hata kagame tuwe watumwa wote na wao wakiwemo ili wajutie maisha yao yote
 
Iwe ziwa Nyasa au Lake Malawi ni sawa tu kwa sababu Nyasa ndio Malawi hiyohiyo.

Ila ziwa lenyewe kiukweli ni la Malawi hakuna haja ya Tanzania kung'ang'ania kwani kuwa kwake ziwa Malawi hakuzui maji kufika kwenye ufukwe wa Tanganyika.
 
Needless to say, Tanzania is no longer a force to reckon with militarily and with the way the events are happening and as the botched October 29 ignominious elections continue to divide opinions, is how the people's sense of patriotism continues to diminish as the days go by.

If the war erupts today, the enemy will definitely use the existing people's disillusionment with this government to massively subdue the heavily politicized Tanzanian military.
 
Mimi nakupa fact wewe unasema maybe? Sijui umri wakoa lakini huko juu kuna mahali nimeongelea suala la International rparian rights.
Kwa Ziwa Nyasa, riparian law:
✔ Inatambua ziwa kama rasilimali ya pamoja
✔ Inazuia umiliki wa upande mmoja
✔ Inalazimisha mashauriano kabla ya miradi mikubwa
❌ Lakini haitoi mpaka wa mwisho kisheria bila makubaliano au hukumu
Anyway, nimeongea mengi ila naona umeamua kuangalia neno, "maybe;" mengine ukayaacha!

Hayo mambo ya riparian law sijui law of the sea, yanafahamika.

Na ni vizuri ume-conclude mwenyewe kwamba: hiyo riparian law au sijui law of the sea, hai apply by default; means mpaka hii case iende mahakamani na hukumu itoke.

Sasa basi kwakuwa hatuna ushahidi kwamba hii kesi ilishaenda mahakama za mipaka na kutolewa hukumu; je, ni kwamba umekubali kwamba mpaka sasa ziwa ni la Malawi, kwa kuangalia Heligoland Treaty?
 
Malawi wanatumia principle ya uti possidetis juris (Mikataba ya mipaka ya kikoloni inalindwa) ambayo ime base kwenye Heligoland Treaty ya 1890.

Tanzania ina base kwenye principle ya median line (mipaka ya maziwa).

Ubatili wa Mkataba wa 1890 ni kama ifuatavvo:-
-Tanzania haikuwa nchi huru mwaka 1890.
-Mkataba haukutaja rasilimali chini ya ziwa (oil, gas, nk).
-Hauzingatii kanuni za kisasa za haki ya matumizi ya maji (riparian rights)
 
Back
Top Bottom