Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Siwashauri' ila kama wanayo nia kweli hao waMalawi juu ya ziwa hilo; wakati wao ni sasa kulidaikwa nguvu.

Wakifanya hivyo, watakuwa wanatusaidia nasi kushughulika na hawa waovu akina Samia na Genge lake kabla hatujawawageukia wao kuwaonyesha mpaka sahihi ulipo.
Hiyo issue ilishaisha na wamenyoosha mikono kwa diplomasia shupavu ya Chifu Hangaya
 
Hivi unafahamu Hiyo JWTZ imegawanyika...??? wananchi hawapo wanachuki kuu na Serikali na Jeshi. ?? ni wakati sahihi kwa Malawi kuchukua Ziwa Lao Mapema...I support them
Hili ndo tatizo kuu, hakuna jambo baya kama kukosa support ya wananchi wako. Ikitokea vita, raia watakuwa wanampa adui coordinates tu, unashangaa ni kwanini adui yupo on target.

Ni kama vita ya Ukraine na Russia, Ukraine wanateseka sana kutokana na waukraine wenye asili ya Russia kutoa coordinates kwa jeshi la Russia.
 
Wakati wenye mamlaka wakiwa busy kuponya majeraha ya MO29, kwa kuyakanusha na kupindua taarifa za ukweli; wenye dunia yao huko duniani, hawachoki kuitafiti dunia na ku shape geopolitics kulingana na taarifa sahihi za kiuchunguzi.

Jana niliingia Instagram, kwenye post ya CIA, nikakuta wameweka taarifa nzuri nzuri kuhusu Ziwa Malawi (sisi tunalijua kama ziwa Nyasa), ikiwemo hii kwamba: ni ziwa lenye fish species nyingi kuliko ziwa lolote lile duniani, na ni ziwa la nne kubwa duniani lenye fresh water.

Binafsi hiyo ya fresh water nilikuwa naijua, ila hii ya kwamba Ziwa Nyasa lina species nyingi kuliko ziwa lingine lolote duniani, sikuwahi kuijua.

Kwa sababu kwa wenzetu CIA pia ina muunganiko wa kikazi na Makampuni ya kimarekani; nimejiuliza itakuwaje pindi makampuni ya kimarekani yatakapoanza uwekezaji wao pale Ziwa Malawi. Je, hii hatua haita chechemua mgogoro mpya wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi?

Kilichonishangaza zaidi ni kwamba: kwenye post hiyo ya CIA, hawakugusia kabisa kwamba Ziwa Malawi lipo pia nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa. Na waligongelea msumari kwa kusema, "Malawi's Lake Malawi." Je, haiwezi kuwa ni turufu kwa Malawi, kwamba mataifa makubwa yanajua tayari kwamba Ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pia ni mali ya Malawi? Na kwa sababu tayari Tanzania kupitia CCM imewabagaza wazungu; je, Tanzania itaweza kujihesabia haki ya umiliki wa ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pindi mgogoro ukirudi upya, kama dalili zinavyoonesha?

View attachment 3518251

Wenu,
MC
Ukiangalia Google maps ziwe lote lipo Malawi hakuna hata kipande chetu chochote wakati Msumbiji wao ni 50/50 na Malawi. Nomeshangaa sana. Ndio maana rais wao Joyce Banda alizua TAHARUKI wakati ule wa JK Mgogoro haujatatuliwa hadi sasa
 
Hiyo issue ilishaisha na wamenyoosha mikono kwa diplomasia shupavu ya Chifu Hangaya
Sijapata kumsikia "mdiplomasia shupavu" anayelazimisha kutawala watu wasiomtaka na kuwaua baadhi yao

haya mambo ya kujilaza akili kwa maksudi kabisa baadhi yenu inawafanya muonekane kama machizi kwelikweli. wakidai HAKI ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Sasa wewe hapa unazungumzia "diplomasia" ipi; hata kwenye swala hilo la ziwa; au ndiyo yale yale mradi tu uonekane umechangia kwa kusifu ili upate mlo wako wa leo!
 
Ukiangalia Google maps ziwe lote lipo Malawi hakuna hata kipande chetu chochote wakati Msumbiji wao ni 50/50 na Malawi. Nomeshangaa sana. Ndio maana rais wao Joyce Banda alizua TAHARUKI wakati ule wa JK Mgogoro haujatatuliwa hadi sasa
Wao na Msumbuji waliyamaliza kwa mikataba, sisi tuliyamaliza kwa kuamini mpaka upo kati kati ya ziwa bila kuwa na mkataba. Kwa ufupi ni kama tuli assume hakuna shida na wamalawi wametumia vizuri ilo ombwe tulilolitengeneza kwa kuamini Tanzania ina nguvu kuliko Malawi. Sasa wao inaonekana nguvu zao waliwekeza kupalilia narrative kiakili bila nguvu za kijeshi.
 
Sijapata kumsikia "mdiplomasia shupavu" anayelazimisha kutawala watu wasiomtaka na kuwaua baadhi yao

haya mambo ya kujilaza akili kwa maksudi kabisa baadhi yenu inawafanya muonekane kama machizi kwelikweli. wakidai HAKI ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Sasa wewe hapa unazungumzia "diplomasia" ipi; hata kwenye swala hilo la ziwa; au ndiyo yale yale mradi tu uonekane umechangia kwa kusifu ili upate mlo wako wa leo!
Ni sarcasm nadhani, msome tena
 
Mkuu hujui kuwa Marekani ilirithi mikataba yote ya uingereza mara baada ya kushika kiti cha superpower? We subiri katika ilo Ziwa igundulike kuna mafuta au Gas alafu utajua mwenye umiliki wa ilo ziwa ni nani! Au hujiulizi kwanini mgogoro wa eneo hilo haujafika katika Mahakama za kimataifa za usulihishi?
 
Cha msingi elewa kuwa huo mgogoro umeisha kwa Malawi kunyoosha mikono na aliyeumaliza ni huyohuyo usiyompenda.
 
Mkuu hujui kuwa Marekani ilirithi mikataba yote ya uingereza mara baada ya kushika kiti cha superpower? We subiri katika ilo Ziwa igundulike kuna mafuta au Gas alafu utajua mwenye umiliki wa ilo ziwa ni nani! Au hujiulizi kwanini mgogoro wa eneo hilo haujafika katika Mahakama za kimataifa za usulihishi?
Upo sahihi. Najiuliza pia: why now? Inawezekana kuna jambo ambalo ni work in progress, na labda ndo linataka kuanza rasmi.

Halafu hao hao mabeberu ndo waligawa hii mipaka, na hao hao ndo waliweka hizi sheria za mipaka sijui ni lazima upite kati kati ya ziwa bla bla. Na hizo mahakama za mipaka ni zao.

Nadhani labda mabeberu wanataka kuwaudhi Tanzania. What if hilo suala likienda mahakama za mipaka ambazo zipo chini ya mabeberu, na waka rule kwamba, ziwa lililopo upande wa Tanzania nalo ni la Malawi?

Itakuwa unfair ndio, ila wao si ndo wenye mahakama na hizo sheria ni zao. Wanaweza tu kutumia hizo sheria na historia ili kutuadhibu na kutuudhi, kutokana na dharau za CCM dhidi yao.
 
Uzalendo umepotea sana, yaani nkipitia posts za watu kwenye uzi huu nashangaa kweli ni watz? Yaani mtu unawezaje sema Mlima Kilimanjaro uko Kenya? Ziwa Victoria liko Uganda? At the same time uwe mtz? I refuse to accept this ... these are mutual exclusive events... guys guys guys... tujitathmini
 
Ukiangalia Google maps ziwe lote lipo Malawi hakuna hata kipande chetu chochote wakati Msumbiji wao ni 50/50 na Malawi. Nomeshangaa sana. Ndio maana rais wao Joyce Banda alizua TAHARUKI wakati ule wa JK Mgogoro haujatatuliwa hadi sasa
Hii umeiweka wazi kabisaa, hilo Ziwa ni lipo kati ya Malawi na msumbiji, Tz haihusiki kabisaa, waache janja janja. Lol
 
Kichaa pekee ndiyo ataruhusu nchi yake ipoteza sehemu ya ardhi yake!! Tupo tayari kupigana na malawi saa yoyote kulinda sehemu ya nchi yetu.
 
Hii umeiweka wazi kabisaa, hilo Ziwa ni lipo kati ya Malawi na msumbiji, Tz haihusiki kabisaa, waache janja janja. Lol
Sema kwa nguvu kabisa. Wakati Msumbiji walikuwa busy kurasimisha mpaka, sisi Tanzania tulikuwa tumeilalia akili na kuwakoromea Malawi kwa nguvu zetu kubwa za kijeshi, tukasahau kwamba, mambo ya mipaka ni ya kimikataba na sio mabavu.

Halafu, Tanzania imekuwa ikiivimbia sana Malawi; refer ile issue ya Bashe kutaka kuwawekea vikwazo vya biashara. Kwahiyo Malawi anaiangalia Tanzania kama aggressive neighbour.
 
Back
Top Bottom