Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Sema kwa nguvu kabisa. Wakati Msumbiji walikuwa busy kurasimisha mpaka, sisi Tanzania tulikuwa tumeilalia akili na kuwakoromea Malawi kwa nguvu zetu kubwa za kijeshi, tukasahau kwamba, mambo ya mipaka ni ya kimikataba na sio mabavu.

Halafu, Tanzania imekuwa ikiivimbia sana Malawi; refer ile issue ya Bashe kutaka kuwawekea vikwazo vya biashara. Kwahiyo Malawi anaiangalia Tanzania kama aggressive neighbour.
Uzuri mie nitokea ukanda huu, hili ziwa ni la Malawi, sio TZ, at least ukikaa maletho pale upande wa msumbiji, ziwa unaliona hili hapa, sio upande wa Nyasa, ni janja janja ya TZ, Ziwa ni la Malawi na msumbiji.
 
Uzalendo umepotea sana, yaani nkipitia posts za watu kwenye uzi huu nashangaa kweli ni watz? Yaani mtu unawezaje sema Mlima Kilimanjaro uko Kenya? Ziwa Victoria liko Uganda? At the same time uwe mtz? I refuse to accept this ... these are mutual exclusive events... guys guys guys... tujitathmini
Mimi binafsi sio
Mtanzania ni Mtanganyika....Halafu nitasimama na Malawi kudai Ziwa lao
 
Uzuri mie nitokea ukanda huu, hili ziwa ni la Malawi, sio TZ, at least ukikaa maletho pale upande wa msumbiji, ziwa unaliona hili hapa, sio upande wa Nyasa, ni janja janja ya TZ, Ziwa ni la Malawi na msumbiji.
Mchawi ni Heligoland Treaty. Tanzania tunasimama na Law of the Sea ambayo ni ya mabeberu. Labda itatulinda.
 
Ziwa liko hapo kyela-matema hadi Songea,njombe,Kwenda hadi mpaka wa msumbiji hawawezi kuhamisha waseme letu-lao haijambo si wote tupo humohumo.hawazuii chochote wakijaribu tu watakiona.
Kwanza kipindi cha Mkapa-Bakili muluzi tuliwasaidia bandari ya Mtwara hawa watumie kilaini tu.
Sasa bandari na ziwa kipi bora
 
Upo sahihi. Najiuliza pia: why now? Inawezekana kuna jambo ambalo ni work in progress, na labda ndo linataka kuanza rasmi.

Halafu hao hao mabeberu ndo waligawa hii mipaka, na hao hao ndo waliweka hizi sheria za mipaka sijui ni lazima upite kati kati ya ziwa bla bla. Na hizo mahakama za mipaka ni zao.

Nadhani labda mabeberu wanataka kuwaudhi Tanzania. What if hilo suala likienda mahakama za mipaka ambazo zipo chini ya mabeberu, na waka rule kwamba, ziwa lililopo upande wa Tanzania nalo ni la Malawi?

Itakuwa unfair ndio, ila wao si ndo wenye mahakama na hizo sheria ni zao. Wanaweza tu kutumia hizo sheria na historia ili kutuadhibu na kutuudhi, kutokana na dharau za CCM dhidi yao.
Hiyo kesi ikienda Mahakamani kinachoangalia mipaka ya mwisho ya kikoloni ilikuwaje? Ziwa likiitwa Lake Malawi sio? Malawi ilitawaliwa na Uingereza sio? Germany akawa Tanganyika ila wakati uo Ziwa lilikuwa upande wa Malawi ijapokuwa Watanganyika wala hawakupata shida kulitumia.
So kimsingi Mjeruman na Uingereza walikubaliana ilo Ziwe liwe upande Malawi lote, watanganyika mtaruhusiwa kulitumia sababu ya maji ila ikitokea kuna rasimali amini nakuambia Malawi atakuwa na haki zote.
 
Ziwa liko hapo kyela-matema hadi Songea,njombe,Kwenda hadi mpaka wa msumbiji hawawezi kuhamisha waseme letu-lao haijambo si wote tupo humohumo.hawazuii chochote wakijaribu tu watakiona.
Kwanza kipindi cha Mkapa-Bakili muluzi tuliwasaidia bandari ya Mtwara hawa watumie kilaini tu.
Sasa bandari na ziwa kipi bora
Msaada wa wao kutumia bandari ya Mtwara ni tendo la hisani, lakini sio mkataba wa mpaka. Kama huna makubaliano basi huna chako.

Hilo ziwa kati yao na Msumbiji, mpaka unapita katikati ya ziwa kwasababu Malawi na Msumbiji walifanya mkataba wa ku share rasilimali za ziwani kwa nchi zote, na uhusiano wao wa kidiplomasia ni mzuri. Sisi hatujawahi kuwa na mkataba wa aina hiyo na Malawi, halafu uhusiano wetu wa kidiplomasia bado ni wa mashaka (zingatia tifu la Bashe na wamalawi)
 
Wakati wenye mamlaka wakiwa busy kuponya majeraha ya MO29, kwa kuyakanusha na kupindua taarifa za ukweli; wenye dunia yao huko duniani, hawachoki kuitafiti dunia na ku shape geopolitics kulingana na taarifa sahihi za kiuchunguzi.

Jana niliingia Instagram, kwenye post ya CIA, nikakuta wameweka taarifa nzuri nzuri kuhusu Ziwa Malawi (sisi tunalijua kama ziwa Nyasa), ikiwemo hii kwamba: ni ziwa lenye fish species nyingi kuliko ziwa lolote lile duniani, na ni ziwa la nne kubwa duniani lenye fresh water.

Binafsi hiyo ya fresh water nilikuwa naijua, ila hii ya kwamba Ziwa Nyasa lina species nyingi kuliko ziwa lingine lolote duniani, sikuwahi kuijua.

Kwa sababu kwa wenzetu CIA pia ina muunganiko wa kikazi na Makampuni ya kimarekani; nimejiuliza itakuwaje pindi makampuni ya kimarekani yatakapoanza uwekezaji wao pale Ziwa Malawi. Je, hii hatua haita chechemua mgogoro mpya wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi?

Kilichonishangaza zaidi ni kwamba: kwenye post hiyo ya CIA, hawakugusia kabisa kwamba Ziwa Malawi lipo pia nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa. Na waligongelea msumari kwa kusema, "Malawi's Lake Malawi." Je, haiwezi kuwa ni turufu kwa Malawi, kwamba mataifa makubwa yanajua tayari kwamba Ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pia ni mali ya Malawi? Na kwa sababu tayari Tanzania kupitia CCM imewabagaza wazungu; je, Tanzania itaweza kujihesabia haki ya umiliki wa ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pindi mgogoro ukirudi upya, kama dalili zinavyoonesha?

View attachment 3518251

Wenu,
MC
Imeisha hiyo. Na sasa ndipo naanza kuelewa kuwa zile chokochoko za Malawi kuhusu ziwa hilo zilikuwa na nguvu ya hawa wahuni.
 
Hiyo kesi ikienda Mahakamani kinachoangalia mipaka ya mwisho ya kikoloni ilikuwaje? Ziwa likiitwa Lake Malawi sio? Malawi ilitawaliwa na Uingereza sio? Germany akawa Tanganyika ila wakati uo Ziwa lilikuwa upande wa Malawi ijapokuwa Watanganyika wala hawakupata shida kulitumia.
So kimsingi Mjeruman na Uingereza walikubaliana ilo Ziwe liwe upande Malawi lote, watanganyika mtaruhusiwa kulitumia sababu ya maji ila ikitokea kuna rasimali amini nakuambia Malawi atakuwa na haki zote.
Naona tunaanza kuelewena. Kumbe ingetakiwa tangu mapema, Tanzania afanya mkataba na Malawi kuhusu haki ya ku share rasilimali zozote zitazopatikana - approach kama ya Msumbiji na Malawi. Ila kwakuwa viongozi hawakuona huo umuhimu wa kukubaliana, hilo ombwe limekuwa kete nzuri kwa Malawi
 
Imeisha hiyo. Na sasa ndipo naanza kuelewa kuwa zile chokochoko za Malawi kuhusu ziwa hilo zilikuwa na nguvu ya hawa wahuni.
Tena Malawi wana uhusiano mzuri sana na Waingereza. Itakuwa mwingireza akishirikiana na mmarekani ndo wanazisukuma hizi kete kupitia mlango wa nyuma.
 
Uzuri mie nitokea ukanda huu, hili ziwa ni la Malawi, sio TZ, at least ukikaa maletho pale upande wa msumbiji, ziwa unaliona hili hapa, sio upande wa Nyasa, ni janja janja ya TZ, Ziwa ni la Malawi na msumbiji.
😹😹😹 Kenya nao waanze kudai mlima wao wachaga hautuhusu kabisaaa!!
 
Uzalendo umepotea sana, yaani nkipitia posts za watu kwenye uzi huu nashangaa kweli ni watz? Yaani mtu unawezaje sema Mlima Kilimanjaro uko Kenya? Ziwa Victoria liko Uganda? At the same time uwe mtz? I refuse to accept this ... these are mutual exclusive events... guys guys guys... tujitathmini
Uzalendo upi unazungumzia?
Wa wananchi kuuliwa katika nchi yao na vyombo vya usalama tunavyovilipa kwa kodi zetu?
 
Watafute kazi zipo nyingi, wana ardhi nzuri walime ndizi na matunda kwa wingi walete dar 😹😹
Tip za wazungu zinatia ukilema. Maana ni hela rahisi rahisi. Utashangaa sana wazee ndo bado wapo kwenye kilimo.
 
Tip za wazungu zinatia ukilema. Maana ni hela rahisi rahisi. Utashangaa sana wazee ndo bado wapo kwenye kilimo.
Muhimu Kenya wachukue mlima wao, hao wachaga watajiju. Wizi sio mzuri.
Wakileta vurugu kung’ang’ania mlima wa watu polisi watawashughulikia kama vibaka wa MO29 waliandamana wakaiba..!!

Jeshi letu la polisi halipendi wezi 😥
 
Back
Top Bottom