Wakati wenye mamlaka wakiwa busy kuponya majeraha ya MO29, kwa kuyakanusha na kupindua taarifa za ukweli; wenye dunia yao huko duniani, hawachoki kuitafiti dunia na ku shape geopolitics kulingana na taarifa sahihi za kiuchunguzi.
Jana niliingia Instagram, kwenye post ya CIA, nikakuta wameweka taarifa nzuri nzuri kuhusu Ziwa Malawi (sisi tunalijua kama ziwa Nyasa), ikiwemo hii kwamba: ni ziwa lenye fish species nyingi kuliko ziwa lolote lile duniani, na ni ziwa la nne kubwa duniani lenye fresh water.
Binafsi hiyo ya fresh water nilikuwa naijua, ila hii ya kwamba Ziwa Nyasa lina species nyingi kuliko ziwa lingine lolote duniani, sikuwahi kuijua.
Kwa sababu kwa wenzetu CIA pia ina muunganiko wa kikazi na Makampuni ya kimarekani; nimejiuliza itakuwaje pindi makampuni ya kimarekani yatakapoanza uwekezaji wao pale Ziwa Malawi. Je, hii hatua haita chechemua mgogoro mpya wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi?
Kilichonishangaza zaidi ni kwamba: kwenye post hiyo ya CIA, hawakugusia kabisa kwamba Ziwa Malawi lipo pia nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa. Na waligongelea msumari kwa kusema, "Malawi's Lake Malawi." Je, haiwezi kuwa ni turufu kwa Malawi, kwamba mataifa makubwa yanajua tayari kwamba Ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pia ni mali ya Malawi? Na kwa sababu tayari Tanzania kupitia CCM imewabagaza wazungu; je, Tanzania itaweza kujihesabia haki ya umiliki wa ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pindi mgogoro ukirudi upya, kama dalili zinavyoonesha?
View attachment 3518251
Wenu,
MC