Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Profesa namkubali.
Hapa nilikuwa najiuliza kwanini nisijenge bwawa langu au kisima kikubwa chini ya milima huku kwetu. Navuna maji ya mvua kwa miezi 3 hadi 4. Nasafirisha maji kwa mabomba ya mipira hadi shambani.

Tanzania kuna mengi hatuja fanya.
Watu wa Misri, Libya, Tunisia, Morocco wakija tanzania wakaona tuna uhaba wa maji au umeme watashangaa sana tuna akili gani.
 
Kumbe anasoma mada zetu humu jukwaani!.

Hili wazo nililitoa wkt fulani hasa kipindi kile cha uhaba wa maji, leo amegusa pale pale.
Umejiaminisha kabisa msomi kama huyu hakuwa analijua hili ila alisoma mada yako JF? Hivi unajua huyu anajishughulisha na kilimo na haya anayozungumzia ni mambo anayo-experience kwenye site? Pia jua hili la kilimo cha umwagiliaji limeshasemwa siku nyingi sana ila ni wanasiasa tu ndiyo hawajui? Tafadhali usijipe credit za uongo.
 
Hata yule Mkuu wa Mkoa huwa anazunguka kusikiliza 'matatizo' ya Wanainchi kana kwamba hawayajui.

Hakika ni kutafuta tu score za kisiasa na posho, na akifanya hivyo lazima waalike Media.
Wanatumia media bias kuongeza point za kisiasa, mfumo wetu wakisiasa haukopoa of course. Haya maigizo yalikuwa mengi sana kipindi flani media hasa clouds walipiga mpunga wa maana sio mchezo
 
Huyu kwangu ndio professor sasa sio yule macho kodo!
IMG_1964.jpg
 
Kwanini mkuu
Nchi hii takribani asilimia 70 ya watu wake wanafanya kazi kwenye kilimo na wanaishi vijijini lakini huoni jitihada za kueleweka za watawala kwenye hiyo sekta. Utapunguzaje umaskini, umachinga uliokithiri na bodaboda kama huwekezi serious kwenye Kilimo!

Suala la Rais na mawaziri kuzunguka mikoani linashabikiwa na raia wengi tu na wanaona huo ndio uchapakazi.Kuna watu hawataki kabisa kusikia kazi za Rais na mawaziri ni za ofisini zaidi na sio kuzunguka vijijini au mitaani, hawaelewi kwa nini kuna watendaji wa kata, Halmashauri, DED , mkuu wa wilaya na mkoa au majukumu yao ni yapi ndio maana unaweza kukuta waziri anakagua tiketi za mabasi stendi au anatatua mgogoro wa shamba kijijini! Huwezi kuendesha nchi ya watu milioni 60 kwa namna hii na ikasonga mbele.
 
Hii ni kweli mkuu hivi hivi kulikuwa na tija gani Makamba kupanda helikopta halafu amerudi kimya kimya licha ya mbwembwe zote..Pana harufu ya kuumiza Kodi zetu....kwa kiwango kikubwa...
Ni vituko vitupu, ni vigumu kupigia hatua kubwa za maendeleo kwa mtindo huu.
 
Back
Top Bottom