Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Hili suala la mawaziri kuzunguka mikoani mfano stendi za mabasi kukakugua tiketi lidhibitiwe kupunguza matumizi ya serikali hasa kipindi hichi ambapo kuna mjadala mkali kati ya kukopa zaidi au kuongeza tozo.
Hahaaa!!mfano waziri wa maji kila siku yuko ziarani tu, kupiga mikwara kwa miaka zaidi ya sita sasa, lakini matatizo ni yale yale tu, kila anaporudi tena eneo lile anakutana na tatizo lile lile tena!!!
 
Yote haya ni sababu ya CCM,na wanaendelea kulinyonya Taifa kama kupe, maendeleo ya kweli tutayasikia kwa majirani tu,sisi tutabaki kuimbiwa wimbo wa "CCM ni Ile ile oooh ni Ile ile"
 
Wakulima wanachukiliwa kama ni Watanzania wa daraja la mwisho. Nobody cares about them zaidi ya kuwaimbia mapambio ya kisiasa tu.
Wakulima wako kama kuku wakienyeji wanajihangaikia kutwa hawana uhakika na shughuli yao, hawana hakika na bei. Wakipata hasara ni yao tu.
Kama tunataka kuisadia nchi yetu ni lazima tumsaidie mkulima ili akitumia kumi apate walau ishirini na sio mbili au pengine sifuri.
 
Nilikodi heka 5, nikanunua mbili..jumla zilikuwa saba...yaani mvua hakuna...uzuri mbegu nilikuwa sijanunua, haya mambo yakutegemea mvua sio kabisa
Mkuu mimi nimekuwa nikilima kwa timing. Msimu uliopita nililima msimu huu nikaacha badala yake nikanunua. mwakani nitalima. nadhani unanielewa
 
Profesa namkubali.
Hapa nilikuwa najiuliza kwanini nisijenge bwawa langu au kisima kikubwa chini ya milima huku kwetu. Navuna maji ya mvua kwa miezi 3 hadi 4. Nasafirisha maji kwa mabomba ya mipira hadi shambani.

Tanzania kuna mengi hatuja fanya.
Soma habari ya hawa wazungu hapa....been doing hicho unachofikiri for decades...got bwawa with capacity ya over 30m litres...

 
Prof Assad angefaa kuwa waziri wa kilmo, bas tu kwa kuwa alikuwa CAG hawezi kuteuliwa
 
Inawezekana sehemu kubwa ya nchi yetu watu wake wana uwezo mdogo sana kiakili na kufikiri kwa logic.
Ni kweli imagine mtu kama Ndugai anahoji mikopo kwamba hajui imefanya nini wakti yeye ni spika amekuwa anapitisha mipango ya serikali kila bajeti.

Huu ni ukichaa,alikuwa na fursa ya kuzuia wakati wa bungee.
 
Inawezekana sehemu kubwa ya nchi yetu watu wake wana uwezo mdogo sana kiakili na kufikiri kwa logic.
Bora hata tungekuwa na huo uwezo mdg wa kufikiria kwa logic, huo uwezo kdg hatuna na hatuji kuwa nao kamwe

Jamii ya kitanzania ni ya kipuuzi mno nahisi kuliko jamii zote duniani.
 
Hahaaa!!mfano waziri wa maji kila siku yuko ziarani tu, kupiga mikwara kwa miaka zaidi ya sita sasa, lakini matatizo ni yale yale tu, kila anaporudi tena eneo lile anakutana na tatizo lile lile tena!!!
Kuna watu wanamsifia ni mmojawapo wa mawaziri wanaopiga kazi sana!! Aliyetuloga inawezekana kafa, tumebaki kama wanasesere tu.
 
Back
Top Bottom