Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Kumbe tungeanza huu utaratibu wa kuchimba mabwawa kwa ajili ya miradi ya wakulima na kwa ajili ya mifugo tangu enzi za uhuru leo hii tungekuwa tunaongelea bwawa au lambo moja kwa kila kijiji.......na tungetumia tozo na mkopo wa kovid kuongeza bwawa moja moja kwenye kila kijiji, inabidi prof. Assad achukue fomu aisee siyo kwa madini haya.....
 
Wakulima wanachukiliwa kama ni Watanzania wa daraja la mwisho. Nobody cares about them zaidi ya kuwaimbia mapambio ya kisiasa tu.
Watanzania tuna shida mahali, kwa nchi za dunia ya kwanza wakulima na wafugaji ndio matajiri ila huku kwetu ndio low incomer na watu wa hovyo.

Nimekuja gundua mifumo yetu ni mibovu mno.
 
Ila kuna mradi ulitengenezwa chini ya ufadhili wa wajapan kapunga rice project
Naona tulipoachiwa tukauaaa

Ova
Tangu lini mwafrika akawa na akili ya kujiongoza mwenyewe, hawa viumbe ni special species ambao wana element ya kutawaliwa na kuongozwa.

Mfano mwingine ni vile viwanda tulivyoachiwa na wakoloni vyote vimekufa, viongozi waliingia tamaa wakaviuza kwa wahuni, wahuni wakang’oa mashine na kuvitelekeza.
 
Hizi sasa ndizo kazi za hao wakurugenzi, sijui wakuu wa wilaya nk. Ila kiuhalisia hawafanyi na wamekaa kisanii zaidi. Unakuta eti mkuu wa wilaya ya Temeke anaongoza sijui jogging, au anakodi wenye ma-blog wampigie debe kwenye mitandao, usanii kwa kwenda mbele.
Hahaha
 
Nchi hii takribani asilimia 70 ya watu wake wanafanya kazi kwenye kilimo na wanaishi vijijini lakini huoni jitihada za kueleweka za watawala kwenye hiyo sekta. Utapunguzaje umaskini, umachinga uliokithiri na bodaboda kama huwekezi serious kwenye Kilimo!

Suala la Rais na mawaziri kuzunguka mikoani linashabikiwa na raia wengi tu na wanaona huo ndio uchapakazi.Kuna watu hawataki kabisa kusikia kazi za Rais na mawaziri ni za ofisini zaidi na sio kuzunguka vijijini au mitaani, hawaelewi kwa nini kuna watendaji wa kata, Halmashauri, DED , mkuu wa wilaya na mkoa au majukumu yao ni yapi ndio maana unaweza kukuta waziri anakagua tiketi za mabasi stendi au anatatua mgogoro wa shamba kijijini! Huwezi kuendesha nchi ya watu milioni 60 kwa namna hii na ikasonga mbele.
Bodaboda tunawajitaji lakini sasa imekuwa fujo
 
Wanatumia media bias kuongeza point za kisiasa, mfumo wetu wakisiasa haukopoa of course. Haya maigizo yalikuwa mengi sana kipindi flani media hasa clouds walipiga mpunga wa maana sio mchezo
Walipiga sana ili kumtangaza vizuri Mzee Baba.

Hata wasafi walichuma.
 
Bodaboda tunawajitaji lakini sasa imekuwa fujo
Bodaboda tunawahitaji kwa sababu sekta ya usafiri wa umma bado iko vibaya sana ila ukweli ni kwamba bodaboda hazipaswi kusafirisha abiria bali zinapaswa kuwa za matumizi binafsi kwa sababu ni hatari sana hata kama dereva amefuzu na yuko makini.

Barabara za lami vijijini/mitaani ni chache sana na hiyo inasababisha uchache au kutokuwepo kabisa usafiri wa gari za abiria kwa uhakika maeneo mengi ya nje ya mji au nauli kubwa kwa abiria na mizigo.
 
Inawezekana sehemu kubwa ya nchi yetu watu wake wana uwezo mdogo sana kiakili na kufikiri kwa logic.
Kama akili unamaanisha kutafuta vichocheo vya uchimi wa kijamii na kutengeneza nchi ya kizallendo.

Mi ninekuelewa
 
Huyu jamaa yupo vizuri sana. Serikali imfanye walau awe mshauri wao
 
Karne ya 21 eti bado kuna watu wanabeba ndoo na kwenda kuchota maji na kumwagilia wakati sehemu kama Jordan walianza irrigation system miaka 8000 iliyopita na Egyptian walianza 3100 BC

Huyo alieambiwa alikuwa anazunguka kutafuta posho tu ni kweli kabisa

Wote wanajua duniani kuna canals na wa Misri walichimba kwa ajili ya umwagiliaji na kupitisha bidhaa zao pia

Ila sisi miaka yote hii tumejifunza kutesa na kula rushwa na kuiba tu

Acha tuwe tunasoma au kutembelea nchi zilizojiendeleza na kuona sisi tukiishi kama wanyama wa Serengeti tu ili mradi tuzaliane tu
 
Pia Karne ya 21 bado watu wanalima kwa majembe ya mkono, ngombe na punda!
 
Umejiaminisha kabisa msomi kama huyu hakuwa analijua hili ila alisoma mada yako JF? Hivi unajua huyu anajishughulisha na kilimo na haya anayozungumzia ni mambo anayo-experience kwenye site? Pia jua hili la kilimo cha umwagiliaji limeshasemwa siku nyingi sana ila ni wanasiasa tu ndiyo hawajui? Tafadhali usijipe credit za uongo.
Siyo kila msomi anaweza kuyafanyia kazi mawazo yake wengi mpaka wapate nguvu kutoka upande mwingine.

Tuna mambo mengi yapo humu ambayo hao hao jamaa zako wanayatwaa hapa JF na kwenda kuyafanyia kazi huko unapopajua.
 
View attachment 2065734

Prof.Assad ametoa maoni yake kuhusu mfumo wa siasa wa nchi yetu. Siasa yetu inatufanya tusiwe na malengo yanayopimika. Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.

Anasema watu wanazunguka kutaka ku score point za kisiasa tu.

Amegusia kuhusu kilimo. Anasikitika sana kuona kilimo kinaimbwa wakati hakuna mabwawa ya kutosha. Anashangaa serikali imeacha maji yaende baharini/ziwani kama vile bahari ndio ina shida na maji kuliko sisi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Pro Assad, huyu ndio maana halisi ya msomi, sio wale wakuokotwa majalalani
 
Huwa inauumiza sana,kuona namna tunavyo ongozwa na watu wasio na Vision,hawana ubunifu wala sera.
Wanawaza per diems pekee..wananchi wanaogelea kwenye UMASKINI wa kutupwa..
 
Huwa inauumiza sana,kuona namna tunavyo ongozwa na watu wasio na Vision,hawana ubunifu wala sera.
Wanawaza per diems pekee..wananchi wanaogelea kwenye UMASKINI wa kutupwa..
Hawa wanaotuongoza wanatoka katikati yetu pia, hawatoki sayari ya Mars au Jupita, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wanaakisi sehemu kubwa ya watu wa nchi hii.
 
Pia Karne ya 21 bado watu wanalima kwa majembe ya mkono, ngombe na punda!

Ni jambo la kusikitisha sana
Katika binadamu ambao hawawezi kutumia akili ni baadhi ya waafrika na sisi tukiwemo

Fikiria unasikia eti kuna watu wameliwa na Mamba wakikatisha mto tena ukiuona sio mpana hivyo
Miti imejaa nguvu kazi ipo kamba zipo
Ila kutengeneza kivuko hawajui kabisa

Ila kwa uvivu ni rekodi ya dunia
 
Tangu lini mwafrika akawa na akili ya kujiongoza mwenyewe, hawa viumbe ni special species ambao wana element ya kutawaliwa na kuongozwa.

Mfano mwingine ni vile viwanda tulivyoachiwa na wakoloni vyote vimekufa, viongozi waliingia tamaa wakaviuza kwa wahuni, wahuni wakang’oa mashine na kuvitelekeza.
Comment hii ina ukweli mtupu na ni ya kibabe

Ova
 
Ni jambo la kusikitisha sana
Katika binadamu ambao hawawezi kutumia akili ni baadhi ya waafrika na sisi tukiwemo

Fikiria unasikia eti kuna watu wameliwa na Mamba wakikatisha mto tena ukiuona sio mpana hivyo
Miti imejaa nguvu kazi ipo kamba zipo
Ila kutengeneza kivuko hawajui kabisa

Ila kwa uvivu ni rekodi ya dunia
Bongo kipaumbele,platform kubwa sahv wanapewa wasanii wakata mauno

Ova
 
Back
Top Bottom