Prof. Janabi unataka uwapangie watu ratiba za kula?

Prof. Janabi unataka uwapangie watu ratiba za kula?

Hivi ndivyo vichekesho ambavyo vinapatikana Bongo.

Prof. wa kwenye media, professor Janabi siku moja nilimsikia anasema kuwa kama unavaa nguo yenye kiuno size 37 wewe ni mgonjwa. Inamaana huyu Prof. hajui kuwa kuna watu naturally wana maumbo makubwa?

Kama mwili wako una umbo dogo ukinenepa na kuvaa suruali size 32 yawezekana uko over weight. Kuna mtu mwingine akivaa suruali size 34 kulingana na mwili wake hapo tunasema anaumwa na amekonda.
Huyu Janabi hata BMI ya form 2 ina maana kaisahau?

Zaidi ya yote ni kwamba kila mtu aishi apendavyo. Hata gymnast na athletes wengi wanakufa chini ya miaka 55, hivyo maisha hayana kanuni.
Hata yeye mwenyewe na kula kwake mara 2, asifikirie ataishi milele! Muda wake na yeye ukifika, atakufa tu kama watu wengine.

Asisahau vifo havisababishwi na magonjwa tu. Anaweza akafa kwa ajali, anaweza akavamiwa na Wazee wa kazi kama ilivyotokea kwa Dr. Sengondo Mvungi na Lucky Dube; na kutangulia mbele za haki.
 
Weka picha za izo makitu
1708586967816.jpg
 
Prof uchwara sawa na Mwenzakw Kabudi tu. Sasa prof hana tofauti na Lokole huyo. Jana anasema tusile vitu vitamu. Eti hata kula chungwa au ndizi ni hatari kwa afya. Jamaa anatengeneza tension bila sababu yoyote na anatafuta trending kama Mwijaku sasa.
He is too nosy. Afunge bakuli lake sasa.
 
Matunda ni bora kuliko juisi; na sababu ni kwamba matunda yana nyuzi-nyuzi na huwezi ukala mengi yakakuzidi kwa sababu utashiba na kuacha.

Juisi haina nyuzinyuzi na unaweza ukanywa nyingi ukazidisha kiwango, na pia huongezwa sukari ambayo siyo nzuri
•Sio wote wanaotengeneza juice wanachuja, hivyo fibre iko pale pale.
•Sio wot wanaongeza sukari kwenye juice, yaani embe, nanasi na parachichi unaongeza sukari ya nini.

Prof kuna vitu anatakiwa aeleze umma vizuri, akiongea kwa mikato anapotosha jamii.
 
Wabongo wengi wanaridhika na miujiza feki kama kikombe cha babu.Profesa Janabi ametoa ushauri ukitaka ufuate hutaki acha.Wengi kinachowakera ni ukweli kwenye huo ushauri.Wapo in denial.
Wengi wamekuwa addicted na hali za maisha wanayoishi ushauri tu umekuwa nongwa.
Ni kama mraibu wa dawa za kulevya ni ngumu kushaurika.
 
Wewe mshukuru Mungu wako huna tatizo za kiafya, shida mnajifanya much know wabongo, ushakutana na mtu renal failure, ushakutana na mtu ana liver failure, ushakutana na mtu ana high cholesterol, kama hujawahi kuumwa na nyota we tulia zako tu.
Huijui dialysis, huijui renal transplant wala liver, mshukuru sana Mungu.

Hii dunia kuna watu wanapigania uhai wao kwa pombe za bei cheeee Ila matibabu ndugu wanachangishana.

Kama wewe hutaki kumsikiliza tulia ndugu yule in Dr Mbobezi ukitaka prove nenda pale Muhimbili kaombe data kama wanaruhusiwa kutoa uone jinsi Sedentary life na ulaji mbovu unavyoondoa watu duniani na kuwaacha maskini.
 
Hivi Janabi ni cardiologist ama Nutritionist?

Maana anavyoongelea chakula ni kama vile yeye ni specialized Nutritionist.

Ama ukiwa daktari unaweza kuzungumzia jambo lolote la chakula?
Nafikiri kada za afya nyingi wanasoma mambo ya Nutrition hata shule za sekondari pia kuna topics za Nutrition

Kwahio wahudumu wa afya wengi wana ujuzi na mambo ya Lishe ila anaesupervise ni Nutritionist ila wanajua wote
 
Matunda ni bora kuliko juisi; na sababu ni kwamba matunda yana nyuzi-nyuzi na huwezi ukala mengi yakakuzidi kwa sababu utashiba na kuacha.

Juisi haina nyuzinyuzi na unaweza ukanywa nyingi ukazidisha kiwango, na pia huongezwa sukari ambayo siyo nzuri
Matumizi yoyote kupita kiasi ni hatari kwa afya yako,, lakini yeye hajazungumzia unywaji wa juice kupita kiasi badala yake kasema tu unywaji wa juice ni hatari kwa afya yako.
 
Matumizi yoyote kupita kiasi ni hatari kwa afya yako,, lakini yeye hajazungumzia unywaji wa juice kupita kiasi badala yake kasema tu unywaji wa juice ni hatari kwa afya yako.
Sawa, uhatari wake ndiyo huo nilivyoeleza.

Matunda hata ufanyeje huwezi kula mengi lazima utashiba.

Lakini juisi glasi moja inatengenezwa na matunda mengi halafu haina zile nyuzi nyuzi ili lishe ibalansi
 
•Sio wote wanaotengeneza juice wanachuja, hivyo fibre iko pale pale.
•Sio wot wanaongeza sukari kwenye juice, yaani embe, nanasi na parachichi unaongeza sukari ya nini.

Prof kuna vitu anatakiwa aeleze umma vizuri, akiongea kwa mikato anapotosha jamii.
Tatizo mmekazana kumjadili Janabi badala ya kujadili alichokisema.

Nimegundua Watanzania wengi ni wajinga sana haswa kwenye suala la lishe.

Sishangai, Mbeya na Iringa kuongoza kwa utapiamlo wakati ni mikoa inayoongoza kwa kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.

Na hata nguvu za kiume zimegeuka kuwa bidhaa adimu kwa sababu ya lishe duni na ujinga.
 
Kumbe zipo zinazochimbwa bwashee🤔🤔

Sikia, hizo kitu zikishadondoka, mmea ukikauka, kule chini kwenye shina kuna viazi.

Ukiamua kuacha, mvua ikinyesha vinaota tena halafu vinazaa, na hivyo mzunguko unadumu.
 
Tatizo mmekazana kumjadili Janabi badala ya kujadili alichokisema.

Nimegundua Watanzania wengi ni wajinga sana haswa kwenye suala la lishe.

Sishangai, Mbeya na Iringa kuongoza kwa utapiamlo wakati ni mikoa inayoongoza kwa kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.

Na hata nguvu za kiume zimegeuka kuwa bidhaa adimu kwa sababu ya lishe duni na ujinga.
Kwahiyo ukweli usisemwe pale anapopuyanga????

Ujinga unaotaka kuongelea unao wewe Ambaye una sikiliza kila neno kutoka kwake na kulikubali kama lilivyo hata kama ni tata.

SHAME ON YOU!!!!
 
Dona ina sumu na inaharibu uwezo wa kufikiri wazungu wameprove.
Sasa kama wewe unaamini hao wazungu kuhusu dona mbona unam challenge Dr Janabi juu ya lishe kwa ujumla? Maana hayo anayosema yametoka kwa hao wazungu pia, na uki Google utayakuta
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Tatizo mmekazana kumjadili Janabi badala ya kujadili alichokisema.

Nimegundua Watanzania wengi ni wajinga sana haswa kwenye suala la lishe.

Sishangai, Mbeya na Iringa kuongoza kwa utapiamlo wakati ni mikoa inayoongoza kwa kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.

Na hata nguvu za kiume zimegeuka kuwa bidhaa adimu kwa sababu ya lishe duni na ujinga.
Sijui kama ulielewa nilichokujibu, sio juice zote zinachujwa hivyo fibres zipo kama kawaida, sio juice zote huwekwa sukari, hayo ya kumjadili Janabi unaleta wewe.

Hata hivyo, yeye kuwa Prof hakumfanyi kuwa exceptional, lazima ajadiliwe akikengeuka.
 
Hivi ndivyo vichekesho ambavyo vinapatikana Bongo.

Prof. wa kwenye media, professor Janabi siku moja nilimsikia anasema kuwa kama unavaa nguo yenye kiuno size 37 wewe ni mgonjwa. Inamaana huyu Prof. hajui kuwa kuna watu naturally wana maumbo makubwa?

Kama mwili wako una umbo dogo ukinenepa na kuvaa suruali size 32 yawezekana uko over weight. Kuna mtu mwingine akivaa suruali size 34 kulingana na mwili wake hapo tunasema anaumwa na amekonda.
Huyu Janabi hata BMI ya form 2 ina maana kaisahau?

Zaidi ya yote ni kwamba kila mtu aishi apendavyo. Hata gymnast na athletes wengi wanakufa chini ya miaka 55, hivyo maisha hayana kanuni.
Umepanic punguza kula hamna namna ukweli haukimbiwi
 
Back
Top Bottom