Prof. Kabudi ataka Elimu ya Biblia itolewe shuleni kuanzia Chekechea hadi Sekondari na Biblia zigawiwe Bure ili kulinda Maadili

Jukumu la kufundisha maadili ni wazazi hayo mambo mengine mbwembwe tu

Ova
hakika malezi ya msingi ya makuzi na kimaadili ni ya wazazi,
malezi ya kiroho na elimu akhera ndiyo wakapate huko kwenye madhehebu yao ya kidini.

elimu dunia wakapate mashuleni.

wakikaidi kuzingatia taasisi hizo bas ulimwengu utawafunza na kuwanyorosha ๐Ÿ’
 
Usingesoma somo la dini usingeweza kuainisha hivyo.
 

Una uelewa mzuri kuhusu theology. Pia comparative religion (which moves together with the comparative law)
 
Nachoweza changia ni kwamba elimu yote inanzia kwenye Biblia. Hakuna andiko la kisayansi ambalo halija quote Biblia.
 
bible knowledge hakya mungu nlilipenda somo hilo,mwalimu gimbagu why ulihama shule mapema ungali bado tulikuhtaji?
maneno ya kwenye biblia kwa lugha ya kiingereza yalikuwa yananichanganya tu
 
maneno ya kwenye biblia kwa lugha ya kiingereza yalikuwa yananichanganya tu
bible ukiisoma vizuri,nakuhakikishia somo kama history na english hautafeli kamwe. Kiingereza kinachotumiwa ktk bible kinamfanya msomaji atumie maarifa makubwa na fikra pana kuelewa. Hivyo past tenses na kiingereza chako lazima kikue na ufaulu ktk masomo hayo uongezeke.
 
kweli mkuu, aliyekuwa anafundisha alikuwa mmalawi...basi nikawa siokoti kitu..nikija kwa biblia ya kiswahili naona nayamudu narudi tena kwa kipindi cha kiingereza..mwisho nikanyosha mikono juu..maana walinitisha kwamba nikifanya mtihani wa necta tu, nitatakiwa kuenelea kulisoma ngazi zote, nikaogopa
 
CCM ndiyo chanzo kikuu cha maadili mabuvu waanze wao kuacha tabia ya unyumbu wa kisiasa, a.k.a kujizima data, yaani kuahirisha kufikiri kizalendo, (uchawa)

Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya baadhi ya wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumika kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki)
 
Kwny mchakato wa katiba mpya, nilimuheshimu mno Kabudi na kudhani anajitambua. Lakini baadae nilikuja kupata wasiwasi sana.

Hivi anavyosema mtaala wa biblia uzingatiwe mashuleni, hajui kuwa mh raisi ni muislamu?

Na uprofesa wake, hajui kuwa nchi hii kuna imani zaidi ya kumi?

Zote ziingizwe kwny mitaala?

Ni uprofesa wa aina gani huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ