Watanzania na waafrika kwa ujumla tumekubali kuwaona wanasiasa wa vyama tawala kuwa ndio miungu na wenye hatma ya kila kitu kumbe ni kakikundi ka watu wachache wanaotumia vyombo vya kimabavu kujinufaisha kwa kucheza na akili za watu hasa kundi kubwa la watu wajinga.
Kabudi analeta siasa za ukanda kwa manufaa ya madaraka lakini anavunja umoja wa watanzania kwa makusudi.
Kwake Uwaziri ni bora na muhimu kuliko Taifa letu la Tanzania.
Yote ni kwa sababu tumeshindwa kuwa na Sera za kitaifa na utaifa.
Kwa kauli kama hiyo ya kijinga kabisa alipaswa kupumzishwa na kufutwa kabisa kwenye uwanja wa siasa. Lakini atapigiwa makofi na wanaCCM wanaowaza madaraka tu.
Mara nyingi kakundi kadogo kwa wapenda madaraka ndani ya CCM Mara nyingi kanacheza na siasa za Ukabila ,ukanda na Udini. Akitokea Raisi Muislam wanawaambia Watu kuwa waslam ndio wanaotoa kura za CCM. Akitokea Rais Mkatoliki wanajarubu kwa siasa za chini chini kuwa wao ndio wenye hatma ya Taifa hili ,yote kwa yote wanacholenga ni madaraka tuu mana madaraka ndiyo nafasi ya kuvuna mapesa mengi na kuishi maisha kama Peponi. Hofu yao kubwa ni kuishi maisha nje ya madaraka. Ndio maana hata nchi zenye vurugu na umaskini wa namna gani bado kuna wenye madaraka na wanayoyagombania na kuyapigania kijanja janja kwa kutumia Udini ,ukabila na ukanda.
Kabudi atapata laana kubwa Mpaka kizazi cha tatu na cha NNE kwani, kutokana na siasa a kilaghai ,kishamba na za kuwagawa watanzania anazozipigania kwa manufaa ya kusaka Pesa na kujihakikishia heshma ya uwaziri. Kwa nini hajifunzi kwa Dr. Mwinyi alikaa kwenye uwaziri kwa miaka mingi,kwa heshima kubwa bila kuwabagua,kuwagawa ,kuwapumbaza na kuwajaza ujinga watanzania?
.....Hivi kura za CCM anazipata kupitia Uchaguzi gani??
Ule wa kuiba na kubadili masanduku ya Kura? Au ni ucahguzi ule wa kupita bila kupingwa,Au ule wa kumuua Alfonce mawazo mchana kweupe? Au ni uchaguzi ule wa kuua albino? Au uchaguzi wa kutumia waganga wa Kienyeji na kila aina za uchawi? Kabudi amezipata kura za CCM kwenye kanda ya ziwa kwa kigezo gani cha kidemokrasia?
Shame on him!! Laana ya wazaramo,wamakonde,wahehe,wamatumbi, wazigua, wamasai (waliokataa ukoloni,) waliopigania Uhuru wa nchi hii iwe juu yake!!!
Hivi wabunge wa CCM wa majimbo nchi nzima ni wachache kuliko wale wa kanda ya ziwa pekee?
Hivi madiwani wa CCM kutoka kanda zingine ni wachache kuliko wale wanaoteuliwa kwa nguvu ya Jeshi la polisi na wakurugenzi toka kanda ya ziwa???
Kabudi anawafundisha nini vijana wa Tanzania juu ya umoja na mshikamano kama Taifa moja?
Ujinga wetu ndio nguvu yao!!
Uchaguzi wenyewe hakuna halafu bado tu mtu anakuja na lugha za kuchochea Ukanda na ukabila kwenye Taifa letu.
Watanzania tungekuwa werevu tungewaonyesha hawa watu kwa wazi kuwa hatupendi siasa za makada uchwara wa CCM za kutugawa.
.......Kama siasa za wakati huu zitaendelea naiona Tanzania ya kikabila au kidini ikija kwa kasi. Watu wameshajua kuwa kuitawala Tanzania kwa matakwa ya kakundi ka watu wasiozidi watano inawezekana tena kwa urahisi tu kutokana na jaa ,na mtutu wa bunduki. Kumbe Mzee yule rks angetaka kuifanya nchi ile enzi zile kuwa nchi ya dini yake angeweza kitahisi sana. Angewatuliza tu waliokua wanamkosoa na kumtukana kwa mtutu . Kisha akaeneza vitishi na kuteua wapambe waliofikiriwa kuwa ni wasomi ili jamii iwaamini. Lakini Baba wa nchi bado alikuwepo hivyo asingekaa kimya na kuona nchi yake inagawanywa kidini au kikanda kwa sababu ya madaraka , pia kanisa lile lililokuwa linaongozwa na Mwanya lingekemea na hata kutishia kuingia barabarani au msituni na kumtoa Mzee yule. Lakini hata hivyo nao pia wangeweza kutiwa misukosuka,mabomu,risasi ,kutishwa na hata njaa au kuitwa wakimbizi wasio raia wa nchi hii ili tu wabaki watu waoga wasiokuwa na uwezo wa kuhoji ,kukosoa na kupinga viongozi wasio na chembe ya utaifa.
Ni vema Mh. Rais akamweka Pembeni Prof. Kabudi kwa heshma ya nchi hii na historia ya makabila yaliyopigania Uhuru wa nchi hii na wale waliojitoa kupoteza Uhuru wa kihistoria wa nchi ya Tanganyika na Ule wa Nchi ya Zanzibar na kuunda Taifa jipya lenye umoja la Tanzania.
Kuwang'ang'ania watu aina ya Kabudi ni kuwanyima watanzania wenye nia njema kabisa na nchi hii nafasi ya kuonyesha uwezo wao wa kupewa dhanania ya madaraka.
Sent using
Jamii Forums mobile app