Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Uko sahihi hyo katiba ni nani anaitaka kabla umaskini haujaondolewa wanasiasa wanakuja na agenda zisizogusa Raia Moja kwa moja.
Lakini si hii hii ccm iko madarakani kwa miaka sitini? Walishindwa nini kuundoa huo umasikini mpk leo iwe issue ya dharura?
 
acha uongo professor katiba mpya ndio kila kitu.
 
Atuambie basi huo mwarobaini

Ova
Huku kenya tuna katiba mpya,kwa ujumla maisha ni mazuri sana,,kila mtu huku ana maisha ya kati,,usafiri mzuri,nyumba za kisasa na hospital za kupigana na magonjwa,,ndo maana viongozi wa nje wakipata corona huletwa Nsirobi,,katiba imetukomboa sana
 
After all hatuhitaji katiba iwe mwarobaini, hata ikiwa ngetwa-3 au ngoka-11 inaweza kupambana na changamoto tulizo nazo angalau kutuliza homa na maumivu ya kichwa....
 
chadema wataelewa tu sasa maana kila mtu waliyemtegemea atawageuka wanaonekana hawana subira
Hapana. Mimi siyo CHADEMA. Ila wewe hukuelewa. Maana yake ni kuwa Katiba Mpya pekee haitoshi, lakini ni ya lazima. Not sufficient but necessary.
 
umeonyeshwa africa ya kusini wana katiba bora lakini haijamaliza walichokuwa wanakifikiria hapa kilichopo siyo katiba mpya ni uchu wa madaraka tu
KILA KITAFUTWACHO KINA FAIDA. ANAYEKIPATA AWE NA SIFA NA IWE NI HALALI NA HAKI. KILA CHAMA CHA SIASA LENGO NI MADARAKA HATA CCM. SASA KWA KUWA WOTE HUTAKA NA WANAHAKI SAWA. APATAYE KWA KUWASHINDA WENGINE IWE NI KWA UHALALI NA HAKI INAYOONEKANA. WASHINDWAWO WAMSHIKE MKONO NA KUMPONGEZA ALIYESHINDA. HAPO NDIPO TUNAPOTAKA WOTE. NA NJIA NI KUPATA KATIBA MPYA AU KUREKEBISHA KATIBA ILIYOPO
 
Katiba Mpya itatupa Tume HURU ya Uchaguzi japokuwa sio Mwarobaini wa matatizo yetu ila itayapunguza kwa kiasi kikibwa.
Alafu ukishapata tume huru....
utakuwa unaokota pesa barabarani
 
Hata kama katiba mpya si mwarobaini, ukweli kwamba bado inahitajika uko palepale.

Hata mimi naamini katiba mpya si mwarobaini.

Na sidhani popote hapa duniani kuna katiba iliyo mwarobaini.

Katiba mpya inahitajika. Nasi wananchi tunapaswa kubadilika kifikra.
 
Ni kipimo gani kitakachotumika kujua kama mbunge ana-perform au laa?? Ni nani atakuwa mpimaji wa hiyo performance?

Hebu taja wewe nchi hizo zenye katiba nzuri na zinafanya vizuri tuzione
 
Lakini si hii hii ccm iko madarakani kwa miaka sitini? Walishindwa nini kuundoa huo umasikini mpk leo iwe issue ya dharura?
Umaskini Africa ni janga we lack visionary leader with good strategy ya kutuvisha as a result nchi zote tuliokuwa nazo maskini in 1960 Sasa zimekuwa developmental state, nchi ka china, Malaysia wamepita hatua kubwa tu. Swala ni kuamua
 
Hii ni kweli maana katiba mpyani kwa ajili ya maslahi yawachache sio kipaumbele Cha watanzania
 
Labda kweli kama raia wa kenya anaweza kupewa uongozi tz unataka kitokee kitugani hapo
 
Kuna kipindi alikua mstari wa mbele kuidai, leo hii anasema haina tija kwa sasa...
 
Hali za watu ziwe vizuri kisha ndio wanasiasa wapewe sinia la nyamaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa nyie wapeni ulaji halafu ndio mtaelewa kazi! Watapiga hela hadi wafie Madarakani

..nilidhani wanasiasa wameshapewa sinia la nyama kwa katiba hii mbovu tuliyonayo.

..unadhani walioko madarakani sasa hivi hawapigi pesa? unadhani wana mipango ya kuondoka madarakani hivi karibuni?
 
..nilidhani wanasiasa wameshapewa sinia la nyama kwa katiba hii mbovu tuliyonayo.

..unadhani walioko madarakani sasa hivi hawapigi pesa? unadhani wana mipango ya kuondoka madarakani hivi karibuni?
Sindio maana mivutano haiishi watu wanagombea collection plates wametuweka wananchi kama bonds! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…