Profesa Janabi: Aliyewaambia Watu wawe Wanakunywa Maji Lita 5 kwa Siku kawadanganya sana

Profesa Janabi: Aliyewaambia Watu wawe Wanakunywa Maji Lita 5 kwa Siku kawadanganya sana

Maji mengi yanaupotezea mwili madini muhimu wanasema it washes electrolytes... Vinginevyo unywe mineralsed water
Usisikilize sana ma Dr wwe kwanza sikiliza mwili wako unataka kupokea nini kwa wakati huo,kama mwili unataka maji upe maji,kama mwili unataka chai upe chai, kama mwili unataka juice upe juice, kama mwili unataka kupumzika upumzishe!!
 
Amesema professa mwenye akili nyingi sawa tumelipokea::= siku tutaambiwa kunya kiasi tusimalize napo ni afya haki yanani
Janabi hivi sasa ni sawa na commedian tu.
Yeye kila wanachoeleza wenziwe yeye analeta vingine ili aonekane ana akili.
Ukimuona siku za karibuni anatisha maana afya imemong'onyoka eti anafanya diet
 
Mkuu uko sahihi!
Niseme tu unywaji wa maji unategemea na hali ya hewa ya mahali mtu alipo!
Kipindi cha joto sana mtu anaweza kujikuta anakunywa maji mengi tofauti na kipindi cha baridi.
Na niseme tu hakuna kipimo rasmi cha maji ambacho mtu anaweza kunywa kumaliza kiu chake.
Mtu anakunywa kiasi cha maji kulingana na mwili unavyohitaji.
Harafu vile vile mwili wa mtu ndiyo unaweza kujia ni kiasi gani cha maji unachotaka ili kukata kiu.
 
"Unatakiwa kunywa Maji pale tu Mwili wako ukikuambia au ukijisikia kuwa una Kiu.

Na hata kama usiposikia Kiu na kutokunywa Maji bado Afya yako itakuwa imara.

Huwa nashangaa mno kuwaona na kuwasikia Watu wakisema kuwa Mwanadamu kwa Siku anatakiwa Kunywa Maji Lita 5 hii si sahihi na wengi wanaokunywa Maji ya Ujazo huo hujikuta wakiwa wameibua Magonjwa mengine Miilini mwao" amesema Profesa Mwenye Akili Nyingi Janabi muda mfupi tu uliopita alipokuwa Mubashara ( Live ) ITV na Radio One katika Kipindi nilichokisahau Jina ila Mtangazaji Miongozaji wake Julieth Robert kutokana na Urembo wake na Sauti yake tamu sijamsahau.

Haya sasa endeleeni tu Kufakamia Mimaji Lita 5 na Kubeba Michupa yenu hovyo barabarani kama Wendawazimu mkijidanganya kuwa mnaimarisha Afya zenu wakati akina GENTAMYCINE tunaokunywa Glasi Tatu ( 3 ) tu za Maji tunaendelea kuwa Werevu (Intelligents) na Afya zetu Kuimarika kila Uchao na Kuonekana bado ni Vijana wakati sasa tunaelekea Saa 12 Jioni.

Kazi Kwenu.
Mwambie hicho kizee chako hicho kisitupigie kelele, maji tunanunua kwa pesa yetu; aachane na maisha yetu. Yeye mbona ananyooka tu na hatujamsema?
 
Back
Top Bottom