Profesa Janabi: Aliyewaambia Watu wawe Wanakunywa Maji Lita 5 kwa Siku kawadanganya sana

Una mashaka na uelewa na medical doctor professor?
 
Miili ya wanadamu hawawezi kulingana kiasi cha mahitaji hasa ya maji.

Kuna watu hawaruhusiwi kunywa zaidi ya nusu lita ya maji kuanzia maji yaliyopo kwenye mlo wao hadi anayoyanywa kama maji yasivuke nusu lita (wanateseka sana)

Kuna watu hata lita 5 ni kidogo kwao

Na kuna watu watakunywa kiasi chochote kinachohitajika bila kulazimisha.

Maji yapo kwenye matunda, mlo wa siku, vinywaji na maji yenyewe. Utajikuta tu unapata kiasi unachohitaji.

Ila glasi 8 au lita 5 kama lazima hii ni propaganda ya hali ya juu. Kwanza inachosha viungo vya ndani ya mwili kufanya kazi isiyo ya lazima.
 
wazee,
mchongo pesa pia inalipa
 
Word...
 
Nashukuru mkuu, japo maelezo ni mengi, jibu la swali langu hakuna.
Je wingi wa maji ni lita ngapi?
Chief Wingi wa Maji unategemeana kati ya mtu na mtu, Umri,Uzito, Wingi wa shughuli au kazi anazofanya ,Na sehemu Ya kimazingira anayoishi..

Mkuu unywaji wa mji mengi Husababisha Kitu kinachoitwa kitaalamu Water intoxication au Hyponatremia .....

Kwasababu unapokunywa maji zaidi ya mwili unachohitaji Unaenda kudilute Sodium na madini mwngine mwilini..
Sasa bahati mbaya kama wewe si mlaji wa vyakula vya kuongeza mineral (Balance diet) unaweza ukasababisha matatizo..
Alichosema GENTAMYCINE ni sahihi sana kwamba ni muhimu kusikiliza mwili wako nini unataka...Mwili kam ukitaka maji Utatoa signal na wewe utakunywa kwa ajili ya Hydration....
Kwa mfano una kilo 40,Una miaka 18 maji lita tano we ya nini?
 
Ungesoma comment yangu ya kwaanza kabisa, hicho ulichoandika kimo mule.

Naunga mkono unywaji wa maji kutokana na kilo zako.. ila usinywe mpaka upate kiu kwa maisha yetu haya mbona mtihani saana.

Dr. Nipe hasara za mtu asiyekunywa maji..
 
Maji mengi yanaupotezea mwili madini muhimu wanasema it washes electrolytes... Vinginevyo unywe mineralsed water
Ni kweli, lakini kuna wataalam wanaoelekeza namna ya kunywa maji.
wanasema lita 1 ya maji unatakiwa uinywe ndani ya masaa 4, na usinywe kwa mkupuo, kunywa kiasi cha kizibo cha maji kwa wakati mmoja mara kwa mara ndani ya masaa 4. Kwa style hii maji mengi yanabaki mwilini na unaweza usiyatoe kabisa.
 
Kuna route km 5 za mwanadamu anatakiwa kuzifanya akikosa mojawapo lazima aumwe au magonjwa nyemelezi.
1.kula Chenye rutubisho nyingi,kuna hadi mama mtilie wanapigisha draft la msosi,nyama/samaki kidogo,mboga jani kidogo,maharage,dagaa kidogo.
2.mazeozi kuna watu hata kutembea umbali wa 30min mtu anaona mateso lkn anashinda hospital wkt magonjwa mengine angejitibu mwenyewe.
3.kupata muda wa kulala at least 6hrs iliubongo upumzike and reset. And mwili upumzike.
4.uwe na furaha aka stress release unaweza kwenda sehemu or do what make you happy baada ya mihangaiko migumu ya dunia. At least once per weekend.
5.change mazingira unapnga nyumba km ndio ya urithi hama hata mkoa ukapate new ideas or nenda katembee mimosa mingine like likizo vile
 
Nakuunga mkono, unywaji wa maji uendane na uzito wako lakini pia tukumbuke tunatumia vinywaji vingine kama cola, soda au vileo ambavyo kwa namna au nyingine ni vyema tuzingatie unywaji wa maji ili tusiipe kazi sana figo katika kazi yake


Unakuta mtu anapiga liquid chupa hata nane kwa siku na zaidi! , Kweli na hapo unywe maji vikombe viwili??
 
Ni sahihi kabisa mkuu
 
nashukuru nimefahamu. Ila kuna matumizi ya water therapy wale wa asubuhi.
 
Ungesoma comment yangu ya kwaanza kabisa, hicho ulichoandika kimo mule.

Naunga mkono unywaji wa maji kutokana na kilo zako.. ila usinywe mpaka upate kiu kwa maisha yetu haya mbona mtihani saana.

Dr. Nipe hasara za mtu asiyekunywa maji..
Nimekuelewa Sana uko sahihi na kingine kuhusu Tanzania Asilimia kubwa Sana Hatuna Mineral Water..
all we have is Purified water.
na ndo maana utakuwa Sijui Afya pure water ,Kili pure water e.tc..
Na ndo Maana pengine amegusa Kundi la watu wengi Tanzania wanaotumia Tap water,Purifying water na Distillied water..
Hasara za mtu asiyekunywa Maji cha kwanza kuliko vyote Ni Dehydration hivyo vingine vinavyofuatia ni complication ya Dehydration
 
Hapo tumeelewana mkuu.
 
GENTAMYCINE tunaokunywa Glasi Tatu ( 3 ) tu za Maji tunaendelea kuwa Werevu (Intelligents) na Afya zetu Kuimarika kila Uchao na Kuonekana bado ni Vijana wakati sasa tunaelekea Saa 12 Jioni.
Mkuu hapa mbona umetushupalia sana! Japo hii elimu tumepata kweli, si unajua ujinga bado ni mwingi na shule zetu nyingi ni za kuingia darasani! 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…