Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

I agree, 360 trillions Tshs ilikuwa mbinu za majadiliano, ili waweze kupata walicho plan kwenye majadiliano yale, kumbuka Barrick Gold yale ni mabeberu haswa ya dunia hii, yaani majambazi makuu, sasa mbinu za majadiliano lazima ziwe kubwa mno...
Tueleweshe vizuri. Kama kusema tunadai try. 360 ilikuwa mbinu ya majadliano, je, kutuaminisha juice ya Madagascar inatibu corona ilikuwa mbinu ya nini? Au kudanganya mbuzi, papai na oil zimekutwa na corona ilikuwa mbinu ya nini?
 
Maana yake ni kwamba hii nchi inaongozwa kwa ulaghai, uwongo na kwa ujinga mkubwa.

Hilo la trillion 360 mmeambiwa na profesa jalala ilikuwa ni uwongo, je kuna mangapi ambayo yamekuwa ya uwongo, na hawajakiri kwa sababu hamjahoji?

Kwa ujumla, awamu ya 5, ilikuwa ni ya uongozi na hadaa, na wajinga/wendawazimu waliokotwa sana kwa zile hadiyhi. Sisi wengine tulijua kutoka mwanzo kuwa ulikuwa ni uwongo na uwendawazimu kusema kuwa Acacia walikuwa wanadaiwa kodi ya ya sh. Trilion 360. Mpumb.avu pekee yake ndiye angeweza kuamini. Ni sawa uambiwe kuwa kuna mwizi ameiba tani 1000 za cement, amekutwa amezipakia kwenye guta,na wewe ukaamini. Wewe utakayeamini ni lazima uwe mwendawazimu.

Wote walioamini kuwa Acacia walikuwa wanadaiwa sh trilioni 360, hakika wote, wana uwendawazimu wa aina fulani.

Hata bilioni 700 walizokubali Barrick kuipa Tanzania ndani ya miaka 7, walitamka wazi kuwa ni msaada, wala siyo deni la kodi, na haitalipwa mara moja.

Hata ukiangalia ule mkataba wa Barrick na Swrikali, utagundua kuwa, mwishoni ni Serikali ndiyo iliyoamua kuibembeleza Barrick, ndiyo maana Barrick ilitoa masharti magumu, na Serikali ikaridhia.

Awamu ile iliwatumia maprofesa punguani kuwahadaa wajinga na neno 'profesa', kumbe ni maprofesa wa hadaa.
 
Wewe ni kada wa CCM?
A. Ndiyo
B. Siyo
C. Sijui
D. Chagua kati ya A, B na C.

By the way, swali lako liko nje ya mada na nje ya maelezo uliyo - quote. Utakuwa una upungufu wa sehemu ya ubongo ya kuchakata muunganiko wa maneno.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
Ni kweli huenda alikuwa na lengo hili, lakini je hii ilikuwa Ndiyo taaluma na namna sahihi ya kushughulikia tatizo hili linalogusa masuala ya kidiplomasia?
 
Target ya trillion 360 ili kupata billion 700 (something less than 6% out of 100%) ambazo haziwezi kuwa enforced- Just a favor? Ni ujinga mtupu kwa macho ya mwenye akili.
Kwenye madai ambayo hayakuwepo, ni fiction, hiyo pesa kwangu ni nyingi sana, bado naendelea kumpongeza Kabudi.
 
Yuko sahihi, ni sawa na mfanyabiashara anayeweka cha juu ili ukija kulia akupunguzie bei bado usishuke chini ya target yake, muhimu ijulikane hicho kilichopatikana hapo hata kama kidogo, bado hakikutegemewa kupatikana.
Mfanyabiashara umtajie mteja bei ni milioni 36 kisha uwaaminishe dunia nzima na kupiga risasi waliokukosoa kisha uje ukubali elfu 70, kweli? Mbinu?
Kwa kawaida kodi hukokotolewa (calculated) sasa cha juu inawekwaje kwenye calculation?! Siyo kama bei ya duka la Mangi ambapo bei hutamkwa tu.
Hata duka la mangi hataji tu bei hovyo hovyo, ni bei ya kununulia anajumlisha na faida yake ambayo mteja anaweza ku afford, hata kama kuna punguzo ni kidogo sana
Sio milioni 36 kwa elfu 70
 
Ni kweli huenda alikuwa na lengo hili, lakini je hii ilikuwa Ndiyo taaluma na namna sahihi ya kushughulikia tatizo hili linalogusa masuala ya kidiplomasia?
Kama hao jamaa waliona wameonewa kwanini hawakulalamika badala yake wakatupa kidogo chake, kwa hii hatua yao nao iliwafanya wakakubali kushiriki huo utapeli, kwangu nao wanastahili lawama.
 
Kwa hiyo Kabudi ametuthibitishia leo kwa niaba ya serikali ya Tanzania kuwa hiyo ripoti ya makinikia iliyosema TZ tunawadai Barrick zaidi ya 300Trilion ilikuwa ni Uongo na Ulaghai wa kutafuta kuvuna pesa za mabeberu kwa njia haramu.

Kuna haja ya kwenda Chato kulipiga pingu kaburi la Magufuli na kulitandika viboko au kuligeuza choo cha umma cha kitaifa ili watu wawe wanakwenda kujisaidia haja kubwa na ndogo kitaifa.
 
Kibongo bongo ni sawa, kama vile mtu anauza kitu elf 25 mwisho unanunua elfu 3.
Si tulipewa zile 700b? Na hisa 16%, umesahau?

Kama hicho kiwango alichosema anakiri ilikuwa uongo, una uhakika gani kuwa tulipewa hizi 700b, na hisa 16%? Tulikuwa tunasema kila siku kubwa Magufuli alikuwa rais muongo na mpika data mkubwa, sasa mitume wake wanaanza kujitokeza kudhibitisha tulichokuwa tunasema.
 
Kibongo bongo ni sawa, kama vile mtu anauza kitu elf 25 mwisho unanunua elfu 3.
Si tulipewa zile 700b? Na hisa 16%, umesahau?
Kibongo bongo ni kama mtu unamtajia bei ya kitu ni milioni 36 kisha unakuja kumuuzia elfu 70
 

Huu wizi ndio unaitwa siri za serikali!
 
Wenye akili walimwelewa na hadi sasa wanamwelewa kabudi. Wajinga ndio hawaelewi.
Kuna kitu 'mbinu za majadiliano' kwa wale lazima kitu kielezwe kwa kingereza ndio wakubali kuna fani..negotiation skills, strategy etc, etc. Nendeni mkamueleze huyo kichaa lissu aliyediriki hadi kumdharau mwalimu wake wa sheria chuo kikuu Prof Kabudi.
 
Lissu alipinga mno zile ripoti huenda aliona kasoro ila akahukumiwa kumiminiwa risasi.
JokaKuu Tindo Mag3 zitto junior
Huenda Lissu hakuwa mbali sana na ukweli.
JokaKuu Mag3 zitto junior Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…