Duu hii ya Lipumba katoa kali ya mwaka. Sasa wale ndugu zangu wa kule kuvuka maji na pantoni za Azam waliomkimbia Zito na ACT yake na kurudi kwa mbwembwe CUF ya Lipumba itakuwaje?
Hivi ni mimi tu ndie ninayeona kuwa kama kampeni za uchaguzi wa 2025 zimeshaanza au nyie wenzangu mnaonaje? Yote kwa yote kama kampeni zimeanza au la tutaendela kujua zaidi mbele ya safari. Angalizo langu kwa mtia nia ni ajitahidi afanye yafuatayo ambayo yatamsaidia sana kushinda bila kutumia nguvu iwapo tu atayafuata lakini siyo hizo blah blah za wakina Lipumba:-
1. Arudi atathmini zile siku zake 100 za mwanzo kabisa alifanya nini mpaka asilimia kubwa ya watanzania wakubwa kwa wadogo, ccm kwa
wapinzania, wenye dini na wasio na dini wote wakawa wanaimba wimbo mmoja tu nchi nzima "anaupiga mwingi".
2. Atafute pesa aweke ruzuku kwenye mafuta bidhaa zishuke bei hapo atawagusa watu wote mpaka masikini wanaokula mlo mmoja kwa
siku ambao ndio wapiga kura wengi nchi hii.
3. Atafute pesa aweke ruzuku kwenye mbolea na pembejeo nchi ijitosheleze kwa chakula na kuwe na ziada ya kuuza nje. Hapa pia atagusa
maisha ya watanzania wengi kwani asilimia kubwa ya watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo kwa njia moja au nyingine.
4. Badala ya kutuma pesa kwenye ofisi za machinga kila mkoa ambazo kwa hakika zitaliwa na viongozi wajanja wachache na kumuachia
lawama yeye mtumaji. Ajikite ajenge masoko ya machinga kila wilaya sehemu ambazo ni rafiki kwa wafanyabiashara kufikiwa na wateja
wao badala ya kuwaacha kuwa wanateseka sasa hivi na kupoteza mitaji yao kwa migambo wa miji/majiji. Mitaji ambayo wameipata kwa
machozi, jasho na damu. Anaweza kujenga tu kwa awamu kuanzia sasa mpaka kufika 2025 walau atakuwa amefika sehemu kubwa ya nchi.
5. Alale mbele bila huruma na watumishi wabadhirifu wanaotafuna fedha za serikali bila huruma; fedha ambazo zinatokana na kodi na tozo
wanazotozwa watanzania masikini wa nchi hii ambao wamekubali yaishe ili nchi yao ijengwe. Hapa aanze na ripoti iliyo wazi ya C & AG kwa
kuwalaza bila viatu wale vinara MSD, TANROADS, TPA n.k. na hasa wale vinara wa BOT na washirika wao waliohusika na kuchanachana noti
kwa mkasi wakalamba 3.9 bilioni mchana kweupe. Asiwe na huruma na hawa watu kwani hili jambo linawatia sana hasira watanzania
ambao kodi na tozo zinawahusu kila sikuniendayo kwa Mungu.
6. Ajitahidi walau baadhi ya madawa muhimu yawepo kwenye hospitali zote za umma. Inajulika wazi kabisa sio rahisi kwa uchumi wetu sio
rahisi kwa dawa zote muhimu kupatikana kwenye hospitali za umma.
7. Afanye ziara ya kikazi na awe na dhamira ya kujifunza kweli kweli kwani elimu haina mwisho hapo kwa jirani zetu wa damu Zambia kwa
Hichilema.
8. ..............................................................................
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutengeneza taswira/sura yake kwenye mioyo ya wenye uhitaji kamwe hautasahaulika daima milele. Mtia nia akifika hatua ya kujenga taswira yake kwenye mioyo ya watanzania hasa wenye uwezo mdogo hata asipofanya kampeni atashinda tu tena saa nne asubuhi. Maana yale aliyoyatenda ndiyo yatampigia kampeni kwa watanzania kabla hata yeye mwenyewe hajasimama jukwaani kuomba kura.
Muda upo akimua kuanza sasa inawezekana kabla ya 2025 kwani bado hajachelewa.
Ni mtizamo tu.