Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Huu upumbavu wa kumjadili mtoa hoja badala ya kujadili hoja ndiyo umetufikisha kwenye huu upumbavu unaolitafuna taifa. Hebu mpinge kwa hoja zake labda unaweza kuwa na mawazo bora zaidi, vinginevyo shut up.

hoja inapokuwa dhaifu ndipo anapogeukiwa mleta hoja.

huwezi simamisha kengere mbili unaponda ufuaji wa umeme kwa njia ya maji.
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.
Sasa Lissu anaingiaje hapo wakati serikali ni ya CCM na ilani ni ya CCM!

Unless una maana CCM ing'olewe ikifeli hiyo 2025!! Maana Lissu hapitishi bajeti wala kusaini mkataba ufutwe.
 
Hii ni miradi inaitwa WHITE ELEPHANTS. Unaweza ukaimaliza lakini isikupe Desired Return on Investment.

Kwa mfano SGR hata ikimalizika kwenda huko Rusumo sijui ambako tuna target mzigo wa Rwanda, bado haina faida kwa vile throughout ya Rwanda ni less than 800k metric tons per annum.

Mzigo wa ndani ni very insignificant kwa vile Magufuli hakuwa na vision. Anajenga reli huku anaua sekta binafsi. Amefirisi akina Yusuf Manji, amewatisha kina Mo Dewji kwa kuwateka, amesababisha vifo vya akina Mufuruki na Shamte kwa chuki zake, Je anategemea local traders gani wasafirishe mzigo kwenye SGR?

Hiyo Stiglers Gorge ni upotevu wa Matrilioni ya hela tu kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo adui mkubwa wa hydro electricity. Kamwe hawezi kupata hizo megawatt 2100 kama alivyotamba kwenye maradio na matv.

Ameshia kuharibu baioanuai ya selous tu na kuteremsha hadhi ya pori tengefu
Ethiopia wako kwwnye conflict na Egypt kwa sababu ya grand Ethiopian Dam, na wenyewe wamekurupuka? Au hawana maono?
Hao wafanyabiashara watano uliowataja ndio tunawategemea waendeleze mradi wa SGR?
 
Huyu Professa aliebariki michongo ya IPTL leo ndio anaishauri serikali
Tukiwa objective Muhongo ameongea ukweli kabisa sema tu mtoa mada kachukua Kipande kinachofit maslahi yake.

Kaongelea 4th Industrial revolution na jinsi energy mix yaani maji yawepo ila gesi, geothermal, na wind n.k ziwepo pia.

Muhongo leo kaongea kama professor
 
Niliwahi kusema siku Magufuli anatoka madarakani, hasa iwapo huo mradi wa SG utakuwa haujakamilika utatekelezwa. Yale ambayo yalikuwa dhahiri kwangu yameanza kutokea.

Je ni kwanini niliwaza hayo? Kimsingi nilijua nchi hii haina sera wala mipango, bali kuna maslahi ya rais aliye madarakani na genge lake. Wakati vwa JK tuliimbishwa umeme wa Gas kama wendawazimu, na yakapigwa mashahiri yote. Tuliambiwa umeme wa gas ukikamilika tutakuwa na 5,000mg+. Cha ajabu wakati tukiimbishwa hayo mapambaio, Magufuli alikuwa waziri tena akawa anaunga mkono mradi ule. Alipoingia madarakani akaona hana maslahi binafsi na umeme wa gas. Akaona afanye mradi wa umeme kwa maji tuliokuwa tunaambiwa matatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Hii yote ni ili apate maslahi binafsi yeye na genge lake. Ndio hapo unasikia sijui taarifa ya upembuzi ni ya 1970 nk.

Sasa tuje kwenye ukweli, hivi unawezaje kuanzisha mradi mpya wa umeme ili kupata 2,115mg kwa 6.5t, unaacha umeme wa gas ambapo ungeweza kupata 5,000mg? Je angeweka 3t kwenye gas asingepata hizo 2,115mg, na 3.5t akiziweka kwenye viwanda?
Kaka hiyo gas yenyewe iko wapi kaka, gas ile tulisha pigwa tangu enzi za mkwere hakuna gas kule ile ni mali ya watu. Magu ameingia kakuta tayari hakuna chetu kule ndio mana akaona bora aje na huo mradi wa umeme wa maji.

Unaposema nchi haina sera maalum ni kweli sikupingi na sababu kubwa ni hawa viongozi wenye tamaa za kifisi fisi.

Wafute tu miradi yote waanzishe mipya wapige hela
 
Nasubiri kumsikia Andrew Chenge na Jaji Werema, yule mwindaji wa Tumbili.
 
tukisitisha ujenzi wa hivyo vinu,ni mwanao ndiye atakuja kuona madhara ya kutokuwa na vyanzo vingi vya nishati.kwa sasa wewe unaangalia kitambi chako na akili yako scope hake mwisho ni kkutwa jion,zaidi ya hapo haioni kitu.

reli inajengwa iishi miaka zaidi ya 100,unazungumzia faida ndani ya miezi 3,kwani mnafikirije wenzetu mbona mko slow namna hii!!!!

tanzania inakua ndugu zangu,miaka 10 tu ijayo itakuwa na uhitaji wa kila kitu kwa ukubwa zaidi,iwe heri kwa tanzania mama asisitishe miladi kwa kuogopa kelele za watu kama nyinyi,ni hatari kwa taifa lijalo.

CAG ametumia pua yake na kipara,kutoa tathmini ya miladi,miladi yote inaonekana kuwa haina tija,ni kweli haina tija!!!au tumechoka kufikiri??
Kwani ameongelea reli mkuu??? Hivo vinu vya stigler gorge life span yake ni miaka mingapi compared na pesa iliyowekezwa??? Uchumi wa dunia unahama kutoka hydro power plants inahamia kwenye gesi na nuclear sisi tunawekeza trillions of money kwa vitu ambavyo lifespan yake haitafika 30 yrs to come!! Hicho kinachofanyika sasa kilitakiwa kifanyike miaka 50 iliyopita.
 
Kaka hiyo gas yenyewe iko wapi kaka, gas ile tulisha pigwa tangu enzi za mkwere hakuna gas kule ile ni mali ya watu. Magu ameingia kakuta tayari hakuna chetu kule ndio mana akaona bora aje na huo mradi wa umeme wa maji.

Unaposema nchi haina sera maalum ni kweli sikupingi na sababu kubwa ni hawa viongozi wenye tamaa za kifisi fisi.

Wafute tu miradi yote waanzishe mipya wapige hela
Gesi ya nchi hii inakuaje mali ya watu??? Kama rais aliingia madarakani akakuta tayari gesi ya mtwara ni mali ya watu ni akina Nan hao ambao alishindwa kuwatambua mpaka aanzishe mradi mwingine ambao pengine alikua na maslahi nao!! Kwani tukisema rais wenu alikua dhaifu tunakosea???
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.


NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Nadhani kwa waliona uwezo wa ku-google wafanye hivyo ili kuthibitisha usemi wake,naona kila aliyekuwa na visasi moyoni
anaanza kutema cheche.
 
Naona unawaza kizamanizamani tu!

Yaani Tesla waje waweke kiwanda cha magari ya umeme hapa Tanzania yatengenezwe hapa halafu yapelekwe Marekani kwenye soko?
Kufuata hayo madini yako.

Au hata matumizi makubwa ya nickel na graphite huyajui?

Hebu acheni kuandika hoja as if unaandika a fiction book.
Mkuu King Bill,

Nakuhakikishia, bila wasiwasi wowote, wewe na mimi tuweke huo mjadala hapa kuhusu uwekezaji wa aina hiyo.

Hapo utakuwa na haki ya kusema "hata matumizi makubwa ya nickel na graphite" siyajui.

Ni kipi hasa kilichokufanya uwe na uhakika kwamba matumizi ya madini hayo siujui? Wewe ni kipi ulichoweka hapa kuonyesha kwamba unao ujuzi wa matumizi yake.

Nakupa changamoto, anza huo mjadala hapa tuuchangie, tuone kisichoweza kufanyika kwa kutumia hayo madini na mengine zaidi ya hayo.
 
More than 70,000 MW of hydropower have already been developed in Canada. Approximately 475 hydroelectric generating plants across the country produce an average of 355 terawatt-hours per year — one terawatt-hour represents enough electricity to heat and power 40,000 houses.(HUKU NI CANADA,KWA WADAU WETU WA MAENDELEO)
Sisi tunataka tuanze na kujenga ghorofa wakati hata mbavu za mbwa hatuna uwezo wa kuijenga?
maprofesa hebu kuweni walinzi wa taaluma zenu
 
Back
Top Bottom