Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Ni mihemko inawasumbua na chuki za ajabu labda uwape kazi ya kwenda kuangalia nani Ni largest producers wa hydroelectric power duniani na Afrika Alafu warudi Tena kuongea utumbo
 
Wewe ndiye hujui, tuliza akili yako ufundishwe. Athari za mazingira kwa binadamu zinazosabanishwa na umeme wa hydro ni kubwa kuliko hiyo bei rahisi ya kunulia unit moja TANESCO. Soma athari za Guri Dam la Venezuela ambalo ndiyo kubwa kuliko yote katika South America au Three Gorges Dam ya China
Point of correction, dam kubwa kuliko yote South America ni Itaipu kati ya Brazil na Paraguay.

Of course mabwawa yana matatizo sana kwenye ecology, lakini ndio dunia ilivyo. Hakunaga good choices peke yake. Kikubwa ni kuangalia gharama ipi unaweza kubeba vs ipi ni kubwa zaidi. Three Gorges dam haikuwa kwa ajili ya umeme tu, ni chanzo cha maji na flood control tool. Mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu, hilo dam ndio lilisaidia kupunguza athari zake. Na kwenye Yangtze river wanajenga dams nyingine, benefits kwao ni kubwa kuliko issues.

Kusema tuendelee kuchoma gesi ni bora kuliko maji, sijui unatumia kipimo kipi. Athari za dams ni localized, athari za fossil fuel ni global. Dunia inapata tabu leo, ni makaa walichoma wakubwa huko kwao miaka hiyo. Kama issue ni mazingira, ashauri kitu kingine sio gesi.

Tunaweza kukubaliana kutokubaliana, lakini ujenzi ndio umeanza tena + Njombe huko kuna Ruhuji 360MW + Rumakali 220MW kwenye pipeline.
 
8 Feb 2021
Kutoka Bungeni Dodoma Leo February 8 2021 Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ni miongoni mwa wabunge waliopata nafasi ya kuchangia mawazo namna uchumi wetu uzidi kupaa kwa kasi na kubainisha kuwa Kilimo na Gesi ndiyo vitakuwa kichocheo uchumi wa Tanzania kupaa kwa kasi kubwa

Na kutoa hoja mambo yapi yapewe kipaumbele katika Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 –2025/26) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/22.
 
HAKUNA PROFESSOR MUONGO KAMA PROFESSOR MUHONGO-H. KIGWANGALA
 
Point of correction, dam kubwa kuliko yote South America ni Itaipu kati ya Brazil na Paraguay.

Of course mabwawa yana matatizo sana kwenye ecology, lakini ndio dunia ilivyo. Hakunaga good choices peke yake. Kikubwa ni kuangalia gharama ipi unaweza kubeba vs ipi ni kubwa zaidi. Three Gorges dam haikuwa kwa ajili ya umeme tu, ni chanzo cha maji na flood control tool. Mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu, hilo dam ndio lilisaidia kupunguza athari zake. Na kwenye Yangtze river wanajenga dams nyingine, benefits kwao ni kubwa kuliko issues.

Kusema tuendelee kuchoma gesi ni bora kuliko maji, sijui unatumia kipimo kipi. Athari za dams ni localized, athari za fossil fuel ni global. Dunia inapata tabu leo, ni makaa walichoma wakubwa huko kwao miaka hiyo. Kama issue ni mazingira, ashauri kitu kingine sio gesi.

Tunaweza kukubaliana kutokubaliana, lakini ujenzi ndio umeanza tena + Njombe huko kuna Ruhuji 360MW + Rumakali 220MW kwenye pipeline.
Hali halisi ya mto Rufiji inaanzia mkoa wa Mbeya kupitia Iringa, Dodoma, Morogoro na Pwani. Mto Ruaha si ule wa miaka ya sitini, daraja la Mkapa lilijengwa kwa kiwango cha upana wa mto Rufiji miaka ya sitini ambapo sasa kiko chini ya nusu
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini ikila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Uelewa wako ni mdogo kuhusu hao uliowataja wanasimamia nini.
Lema na Tundu Lissu wanasimamia yanayofanana, lakini Muhongo huyo wenu.

Pia, sera ya CHADEMA ni elimu bure hadi chuo kikuu. Ccm ni elimu bure hadi form 4. Sasa CHADEMA hawafuti elimu bure feki ya Magu, bali wataiboresha na kupanua wigo hadi chuo kikuu.

Msipaniki Magu anavyovuliwa nguo, maovu yake yanaanikwa. Yeye si alikuwa mbabe?
 
With its elephants and giraffes crossing the savannah, its hippos wading in shallow waters, its lions weaving through the grasses on the lookout for prey and its black rhinos recently seen by biologists, the Selous Game Reserve is teeming with life.

But an ecological disaster threatens it today: the Stiegler Gorge dam project is to be built on the Rufiji River in the heart of the World Heritage Site. 1500 km² of forest and savannah would be submerged.

The dam would cause damage downstream to the delta and in the mangrove forests. 200,000 people would be affected, especially farmers and fishermen.

Of deforestation permits were issued to 17 companies. The Egyptian construction consortium El Sewedy Electric and Arab Contractors has started construction in July 2019 and completed its first phase in November 2020. Banks CRDB Bank Plc, United Bank for Africa and Afriexim Bank involved in the project at $ 3 billion.

Environmentalists fear the final destruction of the already degraded protected area and oppose the project . A uranium mine is already threatening to destroy part of the reserve. The elephant population has collapsed. UNESCO therefore placed the Selous reserve in 2014 on the list of “World Heritage in Danger” .

President Magufuli, who died in March 2021, wanted to appear as a non-criticism man of action. A member of the government had even threatened opponents of the project with jail .

The people of Tanzania need a better supply of electricity. But the Stiegler Gorge dam project is not a solution.

Let us ask the new president Samia Suluhu Hassan to stop this crazy project....
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Jamani ubinadamu kazi. Hawa viongozi vigeugeu sana
 
Huyu ni mpigaji tu akae kimya! Hajatoa mchanganuo wowote kwann gasi ndiyo mkombozi na siyo HEP.

Tumekuwa na gas miaka mingi mbona umeme haujashuka bei!

Magufuli anaweza akawa amechemka mengi ila Bwawa la Nyerere nitamuunga mkono 100%. Serikali iangalie namna ya kuendeleza mradi huu!!

Miradi mingine inaweza ikapigwa chini ila Bwawa la Nyerere chonde chonde tupambane hii project ikamilike!!

Mugongo anafahamika tu alitudalalia kipindi akiwa waziri wa nishati hatujasahau bado!

Akasema Mtanzania anaweza kutengeneza juice tu ili agawe vitalu kwa wazungu! Kwamba mtanzania hana haki ya kumiliki rasilimalimzake! I hate his decision and statement to Tanzanian since that time! Mpaka unajiuliza huo Uprofesa wake alinunua au aliokota?

Au ndo kule kusoma na kuelimika na kusoma na kubakia na makaratasi mkononi wakati kichwani ni tope tupu?☹️☹️☹️
 
Tena bila hofu anadanganya mchana kweupe eti fossil fuels ndiyo inayotumika...Mwisho wa hizi dirty energies ni 2030 kwenye global resolutions...Aache kutulisha matango pori
Anawainjoy maboya tu
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Magufuli atawafufukia nyie Wanaa wakubwa..
 
Hali halisi ya mto Rufiji inaanzia mkoa wa Mbeya kupitia Iringa, Dodoma, Morogoro na Pwani. Mto Ruaha si ule wa miaka ya sitini, daraja la Mkapa lilijengwa kwa kiwango cha upana wa mto Rufiji miaka ya sitini ambapo sasa kiko chini ya nusu
Hilo la kutumia analysis ya mwaka 1970 ni weakness. Ngoja tuone tutakapofika, lakini as an insurance, bado tunahitaji kuendelea kuwekeza kwenye umeme wa gesi kama backup lakini isiwe main option.
 
Mwendazake alifanya makosa sana kuminya uhuru wa watu kuzungumza mwisho akajiona yupo sahihi sana na kila aliyepinga mawazo yake alikuwa ni upande wa beberu.

Hoja hizi angezijibu yeye kama angeacha watu huru.
 
Jina lake tu linadhihirisha alivyokuwa mnafiki Yani Tanzania tunashida kubwa Sana wanafiki wamejaa kila Kona Magufuli ametuzindua na kifo chake ndio mwanzo wa vuguvugu la ukombozi wa kweli.
 
Back
Top Bottom