Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Ndugu yangu, hiyo adhabu ya sasa ya miezi 15 aliyopewa Zuma si ya kesi ya msingi ya ufisadi ambayo bado inamsubiri, ila hii ni kwa kushindwa na kukataa ku'appear kwenye Zondo Commission' iliyokuwa inachunguza tuhuma za State Capture' ya mfanyabiashara Gupta,aliyekuwa kama ndo ana remote control serikali na ANC atakavyo,kwenye kila sekta...Kesi ya msingi ya ufisadi kwa Zuma bado inamsubiri....
Sawa nimekuelewa lakini si kwa kuirejea afrika kusini. Niirejee nchi ambayo fisadi Zuma anafungwa miezi 15?!!! Utofauti uko wapi na kutofungwa?
 
Magufuli alikuwa shetani ameondoka na damu nyingi sana za watu adhabu yake anatakiwa maiti yake imwagiwe tindikali au ichomwe na gesi ipotee kabisa kwa ardhi ya nchi hii.
Damu za majambazi/mafisadi na wagonjwa waliokufa kwa kukosa kufanyiwa operation kisa mgao wa umeme zipi nyingi…
 
WaTanzania hamueleweki!! Kuna thread ipo humu ikidai TANZANIA inahitaji watu wa private sector wenye exposure ndio wasimamie taasisi za umma ili ziwe na ufanisi. Leo tena oooh wafanya biashara wasiwe kwenye kusimamia hizi taasisi? Which is which.

Muda mwingine naona Magufuli alikua sahihi tu kufanya alichojisikia yeye hata kama ni mistake sababu waTZ hawaeleweki wanataka nini.
Kwanini wasimamie mali za UMMA kwanini wasitengeneze zao zifanye kazi kwa manufaa ya UMMA ? Ni sawa sawa unampa mtu kisima cha kijiji ili asimamie ugawaji maji wakati ungeweza kumuacha achimbe chake na auze kwa manufaa yake na ya UMMA, Practically ukimuachia huyu kuna uwezekano ataweka mfereji upeleke kwenye kisima chake ili auze...,
 
Ndugu yangu, hiyo adhabu ya sasa ya miezi 15 aliyopewa Zuma si ya kesi ya msingi ya ufisadi ambayo bado inamsubiri, ila hii ni kwa kushindwa na kukataa ku'appear kwenye Zondo Commission' iliyokuwa inachunguza tuhuma za State Capture' ya mfanyabiashara Gupta,aliyekuwa kama ndo ana remote control serikali na ANC atakavyo,kwenye kila sekta...Kesi ya msingi ya ufisadi kwa Zuma bado inamsubiri....
Alaa kumbe! Hapo sawa!
 
Mkuu labda unisaidie, hivi bodi inaweza amua mambo tu kiholela bila hata waziri au Rais/vyombo vya usalama kushauri otherwise prior to maamuzi? Mbona wakiboronga huwa wanatimuliwa? Maadam wanafanya kazi ndani ya sheria na kanuni basi wakizivunja watatimuliwa tu.

2. Ni kheri uchukue wafanya biashara wanaojua soko linahitaji nini na market patterns ni zipi kuliko profesa wa UDSM ambaye anajua theories tu lakini hana practical experience ya kuendesha taasisi pana kama TANESCO!!

3. Kingine Tanzania na dunia nzima inaendeshwa kwa ubepari ama market economy lakini ni ngumu sana kuchora mstari kati ya private sector na public sector.
Mfano tunajua kuna mawaziri ambao wana biashara na hisa kwenye sekta binafsi je Mwigulu au Jenista wawe disqualified kuwa viongozi serikalini kisa wana biashara binafsi? Au double standards ni pale mfanya biashara mkubwa tu anapokua kwenye bodi ya TANESCO ila akiwa mwanasiasa ni halali ???

VERDICT: Mimi siungi mkono mafisadi kuwepo kwenye bodi ila naunga mkono 100% kujaza watu wa private sector kwenye taasisi za umma ili waweze kuongeza ufanisi. Imagine TTCL inavyoendeshwa!! leo hii wakihamisha management nzima ya Vodacom/Tigo kwenda TTCL unadhani ufanisi hautongezeka?

kikubwa ni sheria za kudhibiti bodi, manunuzi, tenda, matumizi n.k ziangaliwe na zisimamiwe 100% trust me kutakua hakuna madhara hata Seth akipewa TANESCO!!
You could be right. Tatizo kubwa la utendaji wa mashirika ya umma Tanzania halitokani sana na incompetence ya watendaji wala BOD. Bali ni viongozi wa kisiasa wenye hulka ya ufisadi. Power sekta imeteseka sana na hili. Ni juzi tu tumetoka “kufunika” suala la Tegeta Escrow (ambalo suspected top villains ndio hao hao). Ndio maana wamehakikisha hakuna kesi mahakamani. Zipo scandals nyingine zilivyofunikwa hivyo hivyo.

Hata uweke private sekta yote kwenye mgt na BOD ya TANESCO kama viongozi wa juu kisiasa wamelenga kufanya yao kama walivyofanya kupitia IPTL sahau habari ya ufanisi. Hapa, baadhi ya wateule kwenye hiyo BOD wanatia shaka mapema kwamba wana conflict of interest.

Labda pengine tusihangaike sana na hilo. Tupiganie kwanza katiba itakayodhibiti mikono ya wanasiasa kuingilia moja kwa moja shughuli za utendaji za mashirika ya umma na kutengeneza mazingira ya “state capture” ili kufanikisha ufisadi mkubwa.
 
Kujiandaa na service charge kila mwazi kwenye manunuzi ya umeme
 
Tatizo nilionalo mimi ni huko kuingiza watu ambao ama tayari wanasemwa semwa kwa kutilia shaka uadilifu wao au wale ambao kutokana na mgongano wa kimaslahi wanaweza kuleta ushawishi kwa bodi na menejimenti ili kupata upendeleo kwenye taasisi zao binafsi.

Wanazoziongoza lakini suala la shirika kujiendesha kibiashara mbona hata wakati wa Magufuli tuliambiwa shirika sasa linajiendesha kibiashara na kudaiwa kwamba sasa shirika halipokei tena ruzuku toka serikalini au ilikuwa changa la macho ili kumpamba mzee wa misifa?
Tanesco haijawahi kujiendesha kibiashara
Ndiyo maana ukinunua umeme kuna 3% ya REA
 
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.

Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.

Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.

"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."

Unaweza kusoma mwenyewe hapa.

View attachment 1954110

Tumepigwa tena!!! Ivi ni kweli mama samia hajui ichi anachokifanya? Huu ni usumbufuwa kiwango cha lami na nilijua kumleta makamba kwenye hii wizara wana leo jambo Mungu ibariki Tanzania
 
Acheni kelele, anzeni kusafisha Machemli kwa Walalahoi wenzangu, wale wa daraja la kati anzeni kuangalia angalia Majenereta yenu yapo sawa!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daaah ukweli unao umiza.
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Kwahyo marekani ndio Tanzania
 
Kuendesha TANESCO kibiashara inahitaji usimamizi wa professionals siyo ma cadre wa chama.
 
Halafu eti nae anatarajia kuingia ulingoni twenty twenty five!!
Hatoamini macho yake akipa 2% ashukuru Mungu, kama mbowe hata gombea nitachora hata panya kwenye hilo karatasi
 
Hivi huyo profesa ana mchango gani kwenye nchi hii mpaka sasa au analeta siasa zake za kikomunisti. Atupishe tujenge nchi
Bila shaka hata ukiambiwa kalia msumari utakalia. Maana kichwani uko black (..)
 
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.

Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.

Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.

"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."

Unaweza kusoma mwenyewe hapa.

View attachment 1954110

Kuna Old and Modern era's kikubwa tusubiri ufanisi ndio tupime
 
Waza maendeleo ya nchi usiwe uchaguzi kila wakati
Maendelea gani ndugu yangu sasa hivi hakuna maendelea ya nchi tena maana kinachotwa kwa maskini kinapelekwa kwa mafisadi. Tunaye mtegemea atutete anarembua macho tuu.
 
Kwanini wasimamie mali za UMMA kwanini wasitengeneze zao zifanye kazi kwa manufaa ya UMMA ? Ni sawa sawa unampa mtu kisima cha kijiji ili asimamie ugawaji maji wakati ungeweza kumuacha achimbe chake na auze kwa manufaa yake na ya UMMA, Practically ukimuachia huyu kuna uwezekano ataweka mfereji upeleke kwenye kisima chake ili auze...,
Mkuu kasome market structure na competition law/policy. Umeme ukiuzwa na private sector pekee kwa bei ya soko sidhani kama utakua una uwezo wa kulipa hizo bili. Hapo TANESCO yenyewe inauza umeme chini ya bei ya soko so bila kulindwa kwa monopoly yake then itabidi iende kibiashara zaidi ili ibaki sokoni so atakayeumia ni mteja unless iwe na business line pembeni inayoweza kuwa feeder ya kutoa pato la kucover gharama za uzalishaji!!

Btw mfano wako sio relevant maana wanasiasa 90% wanamiliki biashara hku uraiani mbona hawapigwi marufuku kuwa viongozi?
 
Ni hakika kabisa watu walio na exposure wanastahili lakini suala la conflict of interest lina angalizo la kipekee katika jicho la maadili
Ni mwanasiasa gani serikalini hapa TZ hana biashara au hisa kwenye private sector?? Mwigulu ni mfanyabiashara ila ndio anaongoza wizara ya uchumi je naye atapendelea biashara zake?? Au mtumishi wa umma ni sawa akiwa mfanyabishara ila mfanyabiashara sio sawa akiingia kwenye sekta ya umma??
 
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.

Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.

Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.

"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."

Unaweza kusoma mwenyewe hapa.

View attachment 1954110

y

True say
 
Back
Top Bottom