Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Profesa Shivji ashangazwa na uteuzi wa wafanyabiashara kwenye uongozi wa TANESCO

Kwa mfano ungekuwa na bucha ungempa fisi aisimamie?
JIBU: Fisi nao wanamiliki mabucha!!

Reason; Mtumishi gani wa umma hana hisa au biashara kwenye sekta binafsi? Nitajie mmoja tu kati ya maofisa waandamizi wa taasisi za umma.
Kama hamna, jibu ni kwamba hakuna tatizo mtu wa sekta binafsi kuingia serikalini maana wao ndio wapo sokoni/walaji hivyo basi wataongeza ufanisi zaidi kuliko maprofesa wa UDSM wasio na practical knowledge
 
Idara ya umeme ni idara inayoendana na teknolojia na pia inahitaji watu wenye exposure (wafanya biashara wana exposure kubwa kuliko waajiriwa). Na shirika linatakiwa liendeshwe kibiashara na sio kupata hasara; katika kufanikisha hayo malengo ni vizuri bodi ikawa na watu wenye uelewa tofauti.
 
Ukiingia kwenye siasa biashara zako unakabidhi watu wengine na serikali ukifanya biashara na biashara zako lazima itangazwe ili watu wengine waweze ku scrutinise kama kuna upendeleo wa aina yoyote au ni biashara tu kama nyingine
Una umri gani ama unauzoefu gani?

Hivi unazani wafanya kazi wakishajua kuna mkono wa bosi kwenye jambo fulani hata kama huyo bosi hayupo hawatalifanyia kazi?

Nazani pia huelewi nini maana ya bosi.
 
JIBU: Fisi nao wanamiliki mabucha!!

Reason; Mtumishi gani wa umma hana hisa au biashara kwenye sekta binafsi? Nitajie mmoja tu kati ya maofisa waandamizi wa taasisi za umma.
Kama hamna, jibu ni kwamba hakuna tatizo mtu wa sekta binafsi kuingia serikalini maana wao ndio wapo sokoni/walaji hivyo basi wataongeza ufanisi zaidi kuliko maprofesa wa UDSM wasio na practical knowledge

Hio ni metaphor mkuu..

Aisee Tanesco is very sensitive…kwa skendo zilizotokea sio busara nzuri kurudisha sura ambazo zinafanania maumivu tuliopata…they are simply traumatizing us…business minded people wameisha mpaka warudie watu wa awamu ya nne…bring new people tuwe na majibu tofauti…

Kuna msemo wa kizungu…insanity is to keep doing the same thing the same way and expect different results…

Watu walishapewa nafasi ya kuongoza wapumzike wawape wengine nafasi kuzungusha gurudumu…sio nchi ya kifalme hii
 
Idara ya umeme ni idara inayoendana na teknolojia na pia inahitaji watu wenye exposure (wafanya biashara wana exposure kubwa kuliko waajiriwa). Na shirika linatakiwa liendeshwe kibiashara na sio kupata hasara; katika kufanikisha hayo malengo ni vizuri bodi ikawa na watu wenye uelewa tofauti.
Hiyo inawezekana endapo waliopo wangekuwa watu makini. Lakini hao watu wa bodi wote waliwahi kuiibia serikali
 
Mkuu kasome market structure na competition law/policy. Umeme ukiuzwa na private sector pekee kwa bei ya soko sidhani kama utakua una uwezo wa kulipa hizo bili. Hapo TANESCO yenyewe inauza umeme chini ya bei ya soko so bila kulindwa kwa monopoly yake then itabidi iende kibiashara zaidi ili ibaki sokoni so atakayeumia ni mteja unless iwe na business line pembeni inayoweza kuwa feeder ya kutoa pato la kucover gharama za uzalishaji!!

Btw mfano wako sio relevant maana wanasiasa 90% wanamiliki biashara hku uraiani mbona hawapigwi marufuku kuwa viongozi?
Mkuu point yako nimeielewa, na inawezekana Ila endapo tu kungekuwa na watu ambao sio wapigaji. Shida watu wapo kimaslahi yao na hii ishatokea Sana
Tanesco ndio sehemu yenye pesa nyingi za bure, hawapeani vyeo ili walete Maendeleo Bali ni kwa ajili ya kupiga na hii imeanza tokea awamu ya mkapa
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
unafananisha USA na Tandale?
nyie watu wengine sijui kwa nn mzee wako hakumwagia nje
 
Una umri gani ama unauzoefu gani?

Hivi unazani wafanya kazi wakishajua kuna mkono wa bosi kwenye jambo fulani hata kama huyo bosi hayupo hawatalifanyia kazi?

Nazani pia huelewi nini maana ya bosi.
Ukiwa shallow minded utaamini kama ulivyo eleza, ndio maana wa "Conde" aliamua tofauti.
 
Hiyo inawezekana endapo waliopo wangekuwa watu makini. Lakini hao watu wa bodi wote waliwahi kuiibia serikali
Tatizo kubwa sisi ni wasikilizaji, hatujaona vielelezo vya kisheria vikimtambulisha fulani ameiba sehemu fulani, kama kuna sehemu walishtakiwa na wakaonekana wanamakosa hayo sawa, tofauti na hapo yanakuwa ni makelele tu ya kisiasa ya kumchafua y ili x aonekane mzuri.
 
Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL unawatu wa Biashara na ni shirika la umma linalofanya biadhara Prof. Anataka kutuambia nini
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Una hoja za maana mkuu, lkn soma between lines.
Seth au Ruge ukiwateua kuwa boardmember wa Tanesco wakati huo wana kesi nayo unategemea nini?
USA na Tz ni nchi zenye sera tofauti
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Trump alivyoingia madarakan tu,hakujihusisha tena na mambo ya biashara zake,kama sikosei alizikabidhi kwa watoto wake wa kiume Donald Jr na Erick Trump.
 
Mfanyabishara kuwa mjumbe wa bodi it's dangerous maana kutakuwa na conflicts of interest, pia wakiendesha kibiashara means ndio mwanzo wa kubinafsisha shirika plus watu wengi binafsi kuingia mikataba na Tanesco mwishowe kesi zisizoisha plus kuwalipa watu mabilioni.Tunzeni hizi thread ..maana mchwa wako kazini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Trump aliongoza kwa kipindi kimoja na Mbowe hajaupata urais. Sasa hoja yako ni nini?
 
Binafsi nina endelea kusubilia Kwa hamu kuona Tanesco itakavyo endeshwa kibiashara pasipo kuingiliwa na wanasiasa .Kuona jinsi bei ya kuunganisha umeme itakavyo endelea kubaki 27,000/= bila kujali mteja ana hitaji nguzo au laaa huku Tanesco iki unganisha wateja Kwa wakati Kwa bei hiyo hiyo.
 
Hilo sahau ndugu, kwa bei hiyo serikali ilibeba gharama nyingine kwa wananchi wake, sasa wanataka liendeshwe kibiashara ujue bei ya umeme mjini na vijijini litakuwa sawa
 
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.

Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.

Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.

"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."

Unaweza kusoma mwenyewe hapa.

View attachment 1954110

Ukiona kiwiliwili cha samaki kimeoza ujue kichwa chake kimeoza zaidi!
 
Usiseme hakuna wakati bado haijafanyika hebu punguza pressure kunywa maji mengi alafu tafakari upya kiongozi
HAIWEZEKANI. Unadhani Ben na Jakaya hawakujaribu? Unawakumbuka NETGROUP SOLUTIONS wewe? Unadhani kwanini genge la wezi waliamua kuanzisha akina DOWANSA, SYMBION n.k? Mbona mashirika mengine yalikwenda na maji kirahisi tu! Hata kuwa Agency tu inashindikana.

TAFAKARI
 
Ukifuatilia kwenye mitaa ya Twitter huyo Prof wamempiga spana vizuri wakitoa na mifano hai ya S.O.Es zinazoendeshwa kibiashara zinavyofanya vizuri kwa huduma na biashara
Hao wanafiki wasubiri baada ya miaka 2 Kama hawajala matapishi yao, tatizo la watu wa Twitter wameelemea kwenye ushabiki wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa mambo.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom