Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford

Profesa Stefan Dercon amekubaliana na comments nyingi ambazo wana JamiiForums wamekuwa wakitupia hapa tangu enzi za Rais John Pombe Magufuli yupo madarakani.


Sasa kwa kuwa maoni ya nguli huyu wa chuo kikuu cha Oxford umewekwa gazeti, ushauri kwa serikali iwe inachukua hatua haraka maoni ya wanaJF badala ya kusubiri ushauri wa kutoka nje ambao umekuja umechelewa na nchi ina mzigo mzito wa "mamiradi"

Professor of Economic Policy ... Risk, crop choice, and savings: Evidence from Tanzania. S Dercon. He has worked extensively in Ethiopia and Tanzania, as well as in India, Peru, ..

SPICE FM

Prof. Stefan Dercon ni mjuzi wa mazingira ya Tanzania kwa kina na pia ameandika kitabu cha Gambling on Development / Kucheza Kamari ya Maendeleo ...

PROF. STEFAN DERCON - GAMBLING ON DEVELOPMENT
Explained : Why Some Countries Win Economically and Others Lose - Prof. Stefan Dercon


Source : SpiceFM
 
Hata siku moja wazungu Hawata kubali kuona nchi za Africa zina piga hatua kujikwamua kutoka kwenye Utegemezi.

Wao wanataka muwe watumwa wao ili waje wawekeze wao na kuwanyonya.

Ni MTU mjingatu Atamshabikia huyu beberu bila kutafakari kwamba ndani ya miaka 50 ijayo kama hamja jipanga kwenye miundo mbinu basi idadi ya watu itapata taabu sana maana watu wanongezeka na wanataka huduma.
 
Sijawahi kuona nchi inapata maendeleo bila kuwa na uwekezaji ktk miundombinu na miradi ya maendeleo. Kamwe haiwezekani. Kukopa hela za covid sawa, kukopa za miundombinu dhambi....

Akili za kuambiwa changanya na zako... Mabeberu na makaburu, hata na vibaraka wao, wanahaha sana kuona miradi kabambe kama bwawa la Nyerere, madaraja, ndege na viwanja vyake, SGR nk inasonga mbele.

Siku zote tajiri atataka maskini aendelee kuwa maskini ili abaki kuwa tegemezi na fursa kwa kumpatia huduma muhimu.
 
3 May 2022

Book talk: ‘Why do some countries gamble on development, and others don’t?’ with Stefan Dercon


In the last thirty years, the developing world has undergone tremendous changes. Overall, poverty has fallen, people live longer and healthier lives, and economies have been transformed.

And yet many countries have simply missed the boat. Oxford’s Stefan Dercon’s new book, “Gambling on Development: Why some countries win and others lose”, asks why it is that some of the previously poorest countries have prospered, while others have failed.

Stefan argues that the answer lies not in a specific set of policies, but rather in a key ‘development bargain’, whereby a country’s elites shift from protecting their own positions to gambling on a growth-based future. Despite the imperfections of such bargains, China is among the most striking recent success stories, along with Indonesia and more unlikely places, such as Bangladesh, Ghana and, tentatively, Ethiopia.

Gambling on Development is about these winning efforts, in contrast to countries stuck in elite bargains leading nowhere. At the talk, he is joined by David Pilling (Financial Times), Melinda Bohannon, (Director of Strategy at FCDO) and Ricardo Soares de Oliveira (Oxford University).

The event will debate some of the themes of the book: how economics and politics are deeply connected, how naïve policy prescriptions distract, how international policies and aid can help or distort, but also the remarkable role played in some countries by leading groups and individuals to drive progress, and the failures of local elites elsewhere. This talk is in conjunction with the Oxford Martin Programme on African Governance

Source : Oxford Martin School
 
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

View attachment 2497178
Ngoja wafuasi wake waje!!
 
Huyo Proffesor wa Oxford kwa nini asimshauri waziri mkuu wa Uingereza Rish Sunak jinsi ya kurekebisha uchumi unaoyumba kwa sasa!

Kutokana na mradi mkubwa wa upanuzi wa mfumo wa treni za mwedokasi nchini kwake Uingereza!

Sio kila msomi ni muelewa wa mambo anayoshairi.kina Dk Musukuma wapo hata Ulaya!

Huyu amewekwa hapo,kuna Kitu tunaenda kupigwa na Msoga Team verry Soon!

Mark my words!
Shikamoo voicer.ukiona beberu linatia mapoz ya ajabu ajabu ujue kuna demu kapack pembeni
 
Hakuna namna miradi yote lazima iishe tuu especially SGR, bwawa la umeme na Busisi, yale mandege sijali hata wakitaka waje wayachukue tuu
Magu amemuachia mama msala maana ana jinsi maana hii miladi imeshakula pesa nyingi sana za mikopo na ili tuimalizie inabidi tuendelee kukopa. Huu ni msala babu kunwa
 
Huyu Magufuli inawezekana alikuwa na IQ kubwa sana kiasi kwamba vilaza wengi humumuelewi .RIP
Huenda alikuwa Kiasi kikubwa cha akili yaani Intelligence Quotient (IQ) akakosa kabisa kiwango cha Kihisia yaani Emotional Quotient (EQ) na Kiwango cha Kijamii yaani Social Quotient (SQ)

Kumbuka watu ambao wana EQ ya juu na SQ huwa wanaenda mbali zaidi maishani kuliko wale walio na IQ ya juu.
 
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

View attachment 2497178
Yule bwana angekuwepo angesema mabeberu hawataki tuendelee, na angepigiwa makofi.
 
Kama hakuacha amani ambayo ingemsindikiza huko aliko kwa amani, atapumzikaje kwa amani? Yaani kama kaburi lake lina masikio, kwa aliyoyafanya, kelele hizi zitamnyima amani

Na bahati baya hawezi kuamka kuomba radhi na kutubu.
Atubu kwa kuwatumbua nyie vyeti feki au kwa kipi?
 
Back
Top Bottom