SAMIA NA MARIDHIANO, KAMARI YA KUELEKEA MAENDELEO MAKUBWA YA KUSHANGAZA YA NCHI
PROF. STEFAN DERCON - GAMBLING ON DEVELOPMENT
Explained : Why Some Countries Win Economically and Others Lose - Prof. Stefan Dercon
Source : SpiceFM
Rais Samia Hassan ameamua liwalo na liwe hata kama chama chake kitashindwa viti vingi vya ubunge au hata urais yote ni anataka kujenga maridhiano ambayo hatimaye yataweka uwanja mzuri wa Tanzania kupiga hatua kubwa ya Maendeleo ya Watu na Maendeleo ya Vitu hicho ndicho profesa Stefan Dercon anaelezea ndiyo njia sahihi nchi kuelekea kupata maendeleo endelevu.
Profesa Stefan Dercon katika mahojiano mbalimbali anasema uwezo wa kiuongozi kuwashawishi wadau wote ikiwemo wapinzani, wafanyabiashara, wasomi wa nchi n.k kufunguka kuelezea wanataka nchi yao iende vipi ndiyo muarubaini wa kutia chachu maendeleo yapatikane na siyo kuwa na staili ya kiongozi mfalme anayeamrisha na kuburuza watu kuwa njia hii ndiyo ya kuelekea kupata maendeleo.
Profesa Stefan Dercon anaongeza kuwa kiongozi akiweza kushawishi makundi yote ndani mwa nchi kisha akatumia staili hiyo kushawishi wadau wa Maendeleo kutoka nchi haijalishi kama ni kukopa kutoka IMF, World Bank n.k bali ni jinsi atakavyoweza kutumia rasilimali hiyo ya mikopo kwa kufuata maoni ya wadau wa ndani ndiyo itakayokuwa dawa ya kasi ya kweli ya maendeleo kupatikana tofauti na maamuzi ya mtu mmoja ambaye hataki kusikiliza wengine wana maoni gani mikopo na rasilimal8 fedha za kodi zitumike vipi.
Profesa Stefan Dercon anaongeza kuwa,nchi kama China uongozi wake ulitumia ushawishi kuwasikiliza wadau wa ndani kuwa nchi yao katika miaka 40 iliyopita waende vipi na ndiyo maana maendeleo endelevu yanaendelea katika nchi hiyo ya China na pia kukinusuru chama cha kikomunisti cha China kunusurika kupotea.
Picha toka maktaba.
Nguli huyu katika mihadhara yake mingi anasema uwezo wa kiuongozi ngazi ya kisiasa au kampuni ni jinsi kiongozi anavyoweza kuwa na ushawishi wa kuwaita wadau wote katika meza ili timu hiyo mchanganyiko iweze kuleta mawazo makubwa nchi iendelee mbele kubwa ni mazingira ya utulivu ambayo kiongozi anaweza kuyashawishi, basi hakuna lisilowezekana kubwa sana kupatikana lakini mabavu, kuziba uwazi, kukaba sauti za wengine zisisikike n.k nchi au kampuni haiwezi kuwa na maamuzi sahihi endelevu kwa kutegemea mtu mmoja.
Nchi zote kama China, Malaysia, Singapore, Dubai n.k kwa nje kunaonekana kama kuna kinara mmoja aliyesababisha mabadiliko makubwa ya haraka ya kiuchumi lakini sivyo hivyo bali kulikuwapo kundi kubwa la wadau waliishirikishwa na wanaendelea kushirikishwa kwa maneno mengine kuna 'maridhiano' ukipenda neno jepesi ndiyo imefanya na kufanya nchi hizo kuendelea kufanya makubwa.
TAASISI IMARA ZA KUSAIDIA MFUMO WA MAAMUZI
N.B
Wahafidhina na ma chawa mnaombwa mtulie mazungumzo ya maridhiano yataleta mambo makubwa ikiwemo katiba mpya (maridhiano), uchumi mkubwa utakaokuwa una mguso ktk kila waleti na pochi ya mtu mzima na familia zao pia utulivu na amani ya kweli katika nchi na kushawishi wadau wa maendeleo kutoka nje haijalishi masharti gani magumu ya mikopo michache tutakayo chukua lakini itatumika tulivyokubaliana ktk maridhiano na matokeo chanya yatapatikana bila kujali vyama au nani yupo Ikulu.