Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Huyu Profesa kutoka Oxford anatupenda sana watanzania, kuliko alivyotupenda Magufuli! Anatuonea huruma - anatamani bwawa la Nyerere lifukiwe lisiendelee tuepushe deni! Dodoma kuhamia kusitishwe, watu (na ofisi) warudi Dar na SGR tuifumue tuuze vyuma chakavu angalau turudishe nusu hasara! Huyu ni Profesa amefanya utafiti ameona tutaingia matatani! Ameona hatupaswi kufanya jambo lolote la maendeleo hapa tutakuwa masikini sababu ya maendeleo! Tumuamini, maana ni Profesa, tena ni mzungu!
 
Umenikumbusha! Ni mzungu sawa na Tony Blair. Ni mshauri mzuri sana na ni vizuri kupendwa na wazungu. Yawezekana hata hili ni matokeo ya Royal tour!
 
Mradi wa kuhamia Dodoma unaweza kusitishwa kwa muda wa miaka 10 mingine ikamilike kwanza, majengo hayaharibiki.

Hili walifanyie kazi maana ulimwengu wa kidigitali kambi / ofisi popote hivyo waliobaki Dar es Salaam wasihamie Dodoma ili serikali ipate nafuu ya matumizi haya yasiyo ya lazima.

Pia hakuna ulazima wa ofisi zote kuhamia Dodoma .
 
Sasa kama mmelipwa,muacheni huyo father apumzike kwa amani asee
Kwa kuna aliyeenda kufukua kaburi lake? Nani amekwambia huko aliko amepumzika kwa amani na watu wanapotema nyongo zao kuhusu madhila aliyowasababishia kunamkosesha amani huko alikozikwa.
Acha watu wateme nyongo, they are not breaking country's laws.
 
Ushauri wa mkoloni?It has never been so akward.Huo sio ushauri,Ni ndoano.
 
Huyo profesa ushuzi mwenye wivu hana lolote. Ndio hayo maprofesa yanapenda kuona Africa ipo nyuma siku zote
 
Wenye taaluma zetu bora za uchumi tulishauri hili siku nyingi Sana.

 
Wenye taaluma zetu bora za uchumi tulishauri siku nyingi mno.

 
Hili jambo Rais analijua maana na yeye alikuwepo.kwenye utawala wa Magufuli aliona ambavyo hiyo miradi yake Ili u stress Uchumi na ku paralyse sekta zingine..

But naunga mkono hoja ya Kukopa ila watafute mikopo yenye masharti nafuu zaidi kuliko kutumia mapato ya ndani..

Ukiangalia Kwa Sasa Afya ya uchumi Ina nafuu kuliko tulikotoka na Bado naamini strategy ya Rais ya kuvutia wawekezaji walau inamlipa .

Mfano ndani ya miaka 2 ,mapato ya TRA yameongezeka Kwa bil.750 kutoka 1.2T Hadi 1.95T ,hii inaonesha uchumi unafanya vizuri.
 
Hakuna ilani iliyosemaga itajengwa bwawa wala haipo,pili kwenye Sgr ilani ilisema ujenzi ungekuwa wa ppp na machina alishapewa tenda Mwendazake ndio alibadili ndio maana mzigo unakuwa mkubwa
 
Through my doctorates of philosophy in economics,
Katika kutekeleza miradi hii ya pupa, tuigawe katika makundi mawili, ile itakayoleta tija haraka na ile ambayo tija yake itachukuwa muda mrefu, tukazane na hiyo ambayo italeta tija haraka au faida, ile ambayo tija yake iko mbali itekelezwe polepole mno, mfano, midege mikubwa tuiuze, na fedha ziingizwe kwenye SGR. ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
[emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957] ameshafanga hiyo kazi,,Sunak mwenyewe ni Mchumi
 
Nyerere aliwahi kutuambia ukiona beberu anakusifia sana jiulize umekosea wapi. Pia magufuli aliwahi kunukuliwa kwamba ukiona beberu anakukosoa basi jua umemtandika penye mshono. Sasa huto samaiah achague mwenyewe, kusifiwa au kukosolewa na beberu.
Zote ya zote yakuambiwa changanya na zako!, namwamini Rais wangu sioni PA kumyumbisha.
 
Viability ys Stieglers Gorge project ilikuwa derived na Consultants wa mebeberu hawo hawo zamani za 1986. The original idea ilikuwa ni kuunganisha Inga Zaire na Caborra Basa Msumbiji into one power pool wateja wake katika nchi hizo. Hii ingetukwamua for centuries na mabeberu wakaona hivyo. Wakakataa kutekeleza (yaani wakavunja mkataba) kwa sababu "it's too big for you", essentially sababu hizi hizi anazotoa huyu. Watatupiga vita hadi majogoo. Hawaja kataa na unfortunately jirani zetu Kenya wanatupiga vita sana. Kumbukeni, mathalani, kwamba SGR yao ni ya dizeli hawawezi kucompete. Pia kumbuka kuwa hawana umeme wa uhakika bila gesi ya Tanzania (na powerpool ya Stieglers)kwa hiyo you can imagine how they are feeling hasa baada ya oilpipeline ya Uganda kwenda Tanga. Bahati mbaya humu humu tunao CHADEMA ambao wako tayari to throw any spanner in the works ili wapate tumehuru.
 
Goodies enumerations indeeds!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ