Ahsante, mkuu ... Tatizo linalonikabili, mawazo yanazidi sana wakati niki-meditate, mpaka nashindwa kutulia. Jingine, kuna jamaa yangu alikuja kazini kwangu, katika mazungumzo yetu mimi na yeye, nikamgusia aina ya project ambayo natarajia kufanya, ile habari ikamvutia na yeye akasema ataifanya pindi mwezi huu ukiisha. Kwa kweli lazima nikiri kuwa sikupendezwa na ile hali ya kuibiwa idea yangu, nikabaki kujilaumu mwenyewe. Lakini la ajabu sasa, usiku nilipolala, akanijia mtu ndotoni, akaniambia unataka kuzuia jamaa yako asiifanye ile project ? Nikamjibu ndio, akaniambia chukua kipande cha kamba ya aina yoyote, nuia unachotaka kiwe, yaani nuia kwamba jamaa asiifanye ile project, kisha ifunge kitanzi uiweke sehemu, hatofanikiwa na hiyo project mpaka utakapoifungua hiyo kamba ..!! Kisha nikastuka usingizini ..!!! Je, na hii nayo ni kitu gani, mkuu ??