Punyeto ni nini na nini madhara yake?
Anahitaji ushauri, siyo laana hatupo duniani kumwombea mtu laana, ila kubadilisha mtu kutoka kufanya mabaya kufanya mema.
NARUDIA TENA KWA HEKIMA, NAOMBA UMWOMBE MSAMAHA MUNGU KWA KUMWOMBEA MWENZIO KIFO.

Mkuu muwache2 huyo yatamkuta2 na yeye japo kwa mwanae.
 
Panga Ratiba Yako.......




fanyakazi, au soma sana, nenda library, meki shua unakaa mezani ukisoma masaa mawili kwa bidii, ukitoka kazini au darasani, panga ratiba ya library na ya mazoezi, na
hakikishaunasali-omba dua kila siku dakika 5 tu

mazoezi: hapa zoezi liwe gumu...anza polepole

  1. kukimbia, pushapu, kuruka kamba, 30 saa kila siku.
  2. unyew maji mengi zaid ya litre3 kwa siku.
  3. usisahau kufanya zoezi la viungo ukiwa umekaa kila baada ya mazoezi
faida:

  • utachoka kwa hiyo ulalala vzr,
  • hutakuwa na muda kuwaza sex, maana ndio chnzo
  • usiwaangalie wanawake, shusha us wako ukiwaona, usipende kukaa nao karb
  • utafaulu
  • utapata kaz nzur
  • utaoa

Shukran sana mkuu. Naamini ushauri wako utanisaidia.
 
Ulaaniwe, ufe una faida gani duniani, uchafu mtupu! Ulaaniwe tena na tena, shetani mkubwa Lusiferi mwana haramu!


Ndugu yangu kua na hekima, jamaa kaomba ushauri afanyeje ili aiache tabia hiyo, sasa wewe unakurupuka na maneno yako ya kipuuzi ukute wewe mwenyewe unakesha na punyeto alafu hapa unazuga. Fikiria kabla ya kupayuka ndugu.
 
Faszar, kuna njia mbili:
1. Jikeep busy na mambo ya msingi kama kuangalia vipindi vya television, kusoma vitabu. Chochote kile ambacho ni constractive na ambacho kitaocupy mind yako. Acha kuangalia picha za kwenye mitandao kwani huwa zinapandisha hisia bure. Acha kukaa kwenye vikundi vyenye watu wanafurahia jambo hilo. Ukiwa kwenye net soma mambo mengine picha za ngono ni one of things zinazokupeleka zaidi huko. (Haya ni mazoezi unayoweza kufanya binafsi).

2. Kuna mwingine hawezi peke yake mpaka apate guid. Siku hizi wapo washauri wazuri tu na watakuongoza. Tumia viongozi wa dini, madaktari au mtu unayemwamini atakuongoza. Watakupa mazoezi na mambo ya kufanya.

Nakuhakikishia utaweza kama ukiwa serious. i am talking through experience kwani hiyo ndio shetani yetu sisi vijana wa miaka kati ya 15 had 30th.

Nashkuru sana mkuu. Ahsante
 
Anahitaji ushauri, siyo laana hatupo duniani kumwombea mtu laana, ila kubadilisha mtu kutoka kufanya mabaya kufanya mema.
NARUDIA TENA KWA HEKIMA, NAOMBA UMWOMBE MSAMAHA MUNGU KWA KUMWOMBEA MWENZIO KIFO.

hapa dunian hakuna mwema' mbona tuna lisahau hilo
 
AHSANTE SANA KWA USHAURI NATUMAI NIMENUFAIKA VYA KUTOSHA. NTAJITAHIDI NA NTARUDISHA MAJIBU BAADA YA KUFANIKIWA. Thanx 2 all pamoja na mlionilani na kuntukana.
 
Ulaaniwe, ufe una faida gani duniani, uchafu mtupu! Ulaaniwe tena na tena, shetani mkubwa Lusiferi mwana haramu!

Duh! kweli jamii forums imevamiwa siku hizi aisee! Mwe! We raia am sure una matatizo makubwa ya kisaikolojia hivyo umekuja kumCrush tu mwenzio aliejitokeza kuomba ushauri ili ujifariji. Kwa kusoma comment zako nakuona kama hauko OK kabisa na wewe ndio unahitaji msaada wa haraka zaidi.. Umesema neno KUBAKA zaidi ya mara tatu kwenye mtiririko wa huu uzi mpaka navyoandika mimi kwa mtu anaefikiria au daktari wa afya ya akili lazima kengele ya hatari italia. Labda unisaidie kunielimisha kuna connection gani kati ya PUNYETO na KUBAKA.. Obvious una kitu unakificha au guilty flani example. kabla hujaokoka ulikuwa unapiga sana nyeto na kwa akili yako mbovu ukataka kubaka hivyo unadhani kila mtu yuko kama wewe kichwani.. Kila mwanaume kamili (sijui kuhusu wewe) kwa namna moja au nyingine alipitia stage ya kupiga nyeto at some point in his life hivyo hakuna cha ajabu hapa kama hukupitia hata mara moja utakuwa una matatizo ambayo ndio yamekupelekea kuokoka au kujifanya radical ili uweze kuyaficha.. Vitu vingine ukiona sio kwenye mstari wako unakula kona tu huna haja ya kuComment..
 
Ulaaniwe, ufe una faida gani duniani, uchafu mtupu! Ulaaniwe tena na tena, shetani mkubwa Lusiferi mwana haramu!
Usimlani Mtu mkuu CHUAKACHARA Muombee kwa Mungu aache huo uchafu na wala usimuite Mwana haramu jaribu kumuelimisha madhara ya kupiga Punyeto huenda akaogopa na kuacha kabisa kutumia Punyeto mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu@faszar Kujichua kunavyoweza kuyaathiri maisha yako!

Kitendo hiki cha mwanaume kujitosheleza kimapenzi kimekuwa kikiwatatiza wataalamu wengi, juu ya kufikia umoja wa hoja kuhusu madhara yampatayo mtu ajifanyiaye mchezo huo. Kuna baadhi ya wanasaikolojia akiwemo Muaustralia Wilhelm Reich wanaeleza katika makala zao kuwa hakuna madhara kwa mtu kujichua mwenyewe.

Lakini katika hali ya kawaida ushahidi mwingi uliotolewa na wahusika wa kitendo hicho umeonyesha kuwa, wanaume wafanyao mchezo huo, hukabiliwa hatimaye na maumivu ya kichwa na upungufu mkubwa wa nguvu za kiume sambamba na kupoteza msisimko wa kimahaba, hasa wakutanapo na wapenzi wao.

Licha ya tafsiri ya upigaji punyeto kuwalenga zaidi wanaume, lakini kitendo cha usagaji ambacho huwahusu wanawake nacho kinaingizwa katika maana sawa na ile ya mwanaume kujitosheleza mwenyewe, isipokuwa utofauti hupatikana katika zana na namna ya kujiridhisha.

Inatajwa katika makabrasha mengi ya watafiti kwamba, viwango vya upigaji punyeto hutofautiana, lakini vijana wenye umri wa miaka 18 – 22 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule na vyuo wameelezwa kufikia kiwango cha mara 4 kwa siku na wanaozidi umri huo kwa miaka minane hugota kwenye mara 8 – 10. (Wanaosoma shule za bweni zenye wanafunzi wa jinsia moja wanaongoza kwa kufanya kitendo hiki)

Kama utata wa watalaamu ulivyo katika kulitazama suala hili, ndivyo ilivyo kwa jamii, dini na makabila pia. Kuna baadhi ya dini zinakataza kabisa waumini wake kujichua kwa imani kuwa, umwagaji chini wa bengu za uzazi ni sawa na uuaji wa mtoto ambaye mwanzo wake ni mbegu hai.

Kwa mfano utamaduni wa kabila la Hopi huko Arizona na Namu, Wogeno pamoja na lile la Sambia nchini Guinea unakichukulia kitendo hicho kama njia halali kabisa ya kumaliza matamanio.

Lakini swali linabaki kuwa, je njia hii ni salama kiasi cha kuipa nafasi kuchukua umuhimu wa tendo asili la ndoa linalojumuisha jinsia mbili tofauti? Haya ndiyo makusudi ya mada hii.

Kwa haraka lazima jibu liwe hapana, kwani ukweli unabaki kuwa upigaji punyeto usiozingatia mipaka na elimu una madhara makubwa ya kisaikolojia, ambayo tayari wahusika wameshathibitisha kukutwa nayo kwa namna moja au nyingine.

Dunia ina ushahidi wa watu ambao walikuwa na nguvu za kiume kwa kiwango kikubwa, lakini walipojikita sana katika upigaji punyeto walijikuta wakikabili matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na hadi leo wameshindwa kupata ufumbuzi wa kuondokana na kasoro hiyo.

Katika hali ya kawaida kinacholeta shida ni nguvu zinazotumika wakati mtu anayejichua anapofikia kilele cha kujitosheleza, pamoja na zana zinazotumika kujichua.

Ifahamike kuwa kuna watu wanatumia mikono mikavu kujisaga, jambo ambalo huwafanya waharibu mishipa ya fahamu inayounganisha uume na mishipa iliyopo kwenye ubongo.

Uharibifu huu humfanya mwanaume aidha apoteze msisimko wa kujamiiana au aupate kwa kiwango cha chini sana na kumfanya ashindwe kuwa imara anapokutana na mwanamke, ambaye sehemu zake nyeti huwa ni laini tofauti na mikono aliyozoea kujichua nayo.

Jambo lingine la hatari linalomkabili mtu anayejichua ni upotevu wa hisia. Wakati wa kujichua kwa mfano, ili mwanaume afike kwenye kilele, lazima akuze hisia kwa kiwango cha juu mno, pengine kupita ukweli halisi atakaokutana nao pindi atakapokuwa na mwanamke faraghani.

Mpiga punyeto hajitoshelezi mpaka amlete kwenye hisia mwanamke mrembo, amvike utundu wa kimahaba, ampe manjonjo mpaka mwenyewe atosheke na kiwango. Kwa namna hii mwanaume mwenye mazoea ya kufanya mapenzi kwenye hisia na wanawake warembo ambao hawezi kuwapata kwa hali halisi, atakapokutana na mwanamke wa wastani asiyekuwa mtundu kimapenzi, hawezi kuusisimua mwili na hivyo kujikuta uume wake ukishindwa kusimama kabisa au usimame kwa kiwango cha chini.

Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kiwango cha raha apatacho mwanaume mpiga punyeto. Kama nilivyosema hapo juu kuwa mwanaume anayepiga punyeto hukuza sana hisia, hivyo kwa kiasi hicho hicho ndicho anachoweza kupata raha anapofikia mshindo, kwa mantiki hiyo anapompata mwanamke halisi anaweza asisikie raha aliyozoea kuipata.

Kuna wanaume wengi ambao wameoa na wanafanya ngono na wake zao kila siku, lakini wakati huo huo wanajichua kujiridhisha zaidi, hili pia ni tatizo la kisaikolojia linaloweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume husika .

Madhara mengine ambayo mwanaume anayejichua mara nyingi kwa siku anaweza kukabiliana nayo ni kushindwa kuzalisha. Hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wake wa kizazi.

Kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa ulimwenguni imebainika kuwa, wanaojichua kwa kiwango hatarishi hukabiliwa na tatizo la kushindwa kuacha. Hii inatokana na ulevi wa mazoea waliojizoeza katika maisha yao.

Pamoja na ugumu huo bado watalaam wanasema kwamba uwezekano wa mtu kuacha kufanya kitendo hicho ni mkubwa endapo tu mhusika atafanya tathimini juu ya madhara tuliyotaja na hatimaye kukichukia kitendo hicho kutoka moyoni mwake.

Baada ya kuliona suala hilo kama tatizo, mtu aliyezoea kujichua anatakiwa kuanza hatua ya kuacha kwa kupunguza taratibu kiwango cha kujichua kwa siku. Hii ina maana kuwa kama alikuwa akijichua kwa mara 5 basi apunguze hadi kufikia mara tatu au mbili kwa siku.

Wakati akiendelea na zoezi hilo, mwanaume aliyedhamiria kuliweka kando wazo la kujitosheleza, anatakiwa kutafuta mwanamke ambaye anakidhi mguso wa hisia za mapenzi ndani ya ubongo wake ili amsaidie kuondoa tamaa ya mwili.
Hata hivyo, ni vema pia kuweka mkazo wa nia katika kupingana na ushawishi wa nguvu za mwili ambao hushindana na maamuzi ya moyo. Katika kuzishinda tamaa inashauriwa mwili uchoshwe kwa kazi au mazoezi.

Mwanaume anayetaka kuacha tabia hiyo anashauriwa kuepukana na hali ya kuwa upweke na kuishi ndani ya fikra za kimapenzi mapenzi, ikiwemo masuala ya kusoma na kuangalia majarida ya ngono, kuzungumzia mambo ya mapenzi zaidi na kuacha utani na kimahaba na wanawake.

Lakini pamoja na hayo yote utafiti uliofanywa mwaka 2003 na timu ya watalaamu walioongozwa na Graham Giles kutoka Chuo cha The Cancer Council cha Australia, ulibaini kuwa wanawake wanaojisaga kwa kiwango cha mara moja hadi mbili kwa siku wako kwenye nafasi kubwa ya kuepukana na kansa ya tezi ya uke.

Na kwa upande wa wanaume ambao hawajichui kwa kiwango cha zaidi ya mara 4 kwa wiki wanaweza kunufaika na upigaji punyeto kwa kupunguza mfadhaiko, kuongeza msukumo wa damu pamoja na faida zote apatazo mtu akutanaye na mwanamke kimapenzi (soma kitabu changu cha Saikolojia na Maisha kinachozungumzia kwa kina tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na jinsi ya kujitibu).


Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kiwango cha raha apatacho mwanaume mpiga punyeto. Kama nilivyosema hapo awali kuwa mwanaume anayepiga punyeto hukuza sana hisia, hivyo kwa kiasi hicho hicho ndicho anachoweza kupata raha anapofikia mshindo. Kwa mantiki hiyo anapompata mwanamke halisi anaweza asisikie raha aliyozoea kuipata.

Kuna wanaume wengi ambao wameoa na wanafanya ngono na wake zao kila siku, lakini wakati huo huo wanajichua kwa lengo la kujiridhisha zaidi, hili pia ni tatizo la kisaikolojia linaloweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume husika na kuwafanya wasione umuhimu wa kuwa na wake.

Matatizo haya ni kwa uchache, lakini yapo mengine ya kiafya, ambayo ni pamoja na kuumwa na kichwa, mgongo na kupoteza nguvu za mwili, hasa kwa wale wanaojichua kwa zaidi ya mara tatu kwa siku.

Madhara mengine ambayo mwanaume anayejichua mara nyingi kwa siku anaweza kukabiliana nayo ni kushindwa kuzalisha, hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wake wa kizazi.

Kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa ulimwenguni imebainika kuwa wanaojichua kwa kiwango hatarishi hukabiliwa na tatizo la kushindwa kuacha. Hii inatokana na ulevi wa mazoea waliojizoeza katika maisha yao.

Pamoja na ugumu huo bado wataalamu wanasema kwamba uwezekano wa mtu kuacha kufanya kitendo hicho ni mkumbwa endapo tu mhusika atafanya tathmini juu ya madhara tuliyotaja na hatimaye kukichukia kitendo hicho kutoka moyoni mwake.
Baada ya kuliona suala hilo kama tatizo mtu aliyezoea kujichua anatakiwa kuanza hatua ya kuacha kwa kupunguza taratibu kiwango cha kujichua kwa siku. Hii ina maana kuwa kama alikuwa akijichua mara 5 basi apunguze hadi kufikia mara tatu, mbili, moja, kwa siku na kuelekea kutofanya hivyo kabisa.

Wakati akiendelea na zoezi hilo, mwanaume aliyedhamiria kuliweka kando wazo la kujitosheleza, anatakiwa kutafuta mwanamke ambaye anakidhi mguso wa hisia za mapenzi ndani ya ubongo.

Hata hivyo, ni vema pia kuweka mkazo wa nia katika kupingana na ushawishi wa nguvu za mwili ambao hushindana na maamuzi ya moyo. Katika kuzishinda tamaa inashauriwa mwili uchoshwe kwa kazi au mazoezi.
Mwanaume anayetaka kuacha tabia hiyo anashauriwa kuepukana na hali ya kuwa upweke na kuacha kuamsha hisia za kimapenzi kwa kusoma na kuangalia majarida ya ngono, kuzungumzia mambo ya mapenzi zaidi.

Lakini pamoja na hayo yote utafiti uliofanywa mwaka 2003 na timu ya wataalamu walioongozwa na Graham Giles kutoka Chuo cha The Cancer Council cha Australia, ulibani kuwa wanawake wanaojisaga kwa kiwango cha mara moja hadi mbili kwa siku wako kwenye nafasi kubwa ya kuepukana na kansa ya tezi ya uke.

Na kwa upande wa wanaume ambao hawajichui kwa kiwango cha zaidi ya mara 4 kwa wiki wanaweza kupata faida sawa na zinazopatikana kwa mtu kufanya mapenzi.
Nakaribisha maswali kutoka kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume, wanawake wasiohisi wakati wa tendo na wenye tatizo la kujichua. Mkuu@faszar

chanzo https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/52288-kujichua-kunavyoweza-kuyaathiri-maisha-yako.html
 
Naombeni ushauri wenu wakuu, me ni kijana wa mika 20 sasa but nimeshndwa kutmza hata wiki bila ya kutopga punyeto. Nifanyeje ili niache hii tabia mbaya. Nisaidieni plz.

Hii ni addiction kama pombe au dawa za kulevya mkuu, na ina athari kubwa sana kisaikolojia. Mimi nina ushahidi wa mtu ambaye alikuwa anafanya kwa muda mrefu, karibu miaka 5 hivi, mwishowe akawa anashindwa kutekeleza majukumu anapokutana na mwanadada halisi,..akaishia kulazimika kuanza kutumia viagra...its deadly mzeya!

Cha msingi jiweke busy na shughuli nyingi, ukichoka sana mwili una njia yake ya ku-release hicho kibubu,,,au tafuta mke (sio girlfriend sababu utakuwa ni uzinzi) akusaidie kuacha hii mambo..
 
Ulaaniwe, ufe una faida gani duniani, uchafu mtupu! Ulaaniwe tena na tena, shetani mkubwa Lusiferi mwana haramu!

Wewe unajiona una busara wakati umeandika ***** tu hapa. Kama hukuwa na ushauri si ungepita tu, sio lazima uchangie kila kilichopo humu jf. Tazama wadau wengi wanakuzodoa na post yako halafu unajitahidi kutafuta sababu nyepesi kujustify mchango wako, eti atabaka!! Kubali umekurupuka, next time ujisahihishe. Mwerevu akivuliwa nguo huchutama!
 
Wewe unajiona una busara wakati umeandika ***** tu hapa. Kama hukuwa na ushauri si ungepita tu, sio lazima uchangie kila kilichopo humu jf. Tazama wadau wengi wanakuzodoa na post yako halafu unajitahidi kutafuta sababu nyepesi kujustify mchango wako, eti atabaka!! Kubali umekurupuka, next time ujisahihishe. Mwerevu akivuliwa nguo huchutama!

Wapi hao unaowasema, msimamo wangu ni huo! Huu ni upuuzi wa matendo kama hayo. Ni sawa na kuendekeza madawa ya kulevya eti ni addiction, sawa na pombe eti ni addiction, ni uovu ambao siwezi kuuendekeza. msimamo wangu ni huo katika upuuzi kama huo. Methali zako ni zako. Naamini hivyo kuwa hayo ni matendo ya kujitakia, ukizini ukapata ukimwi wakati uanambiwa athali za kuzini na unajua ukimwi ni nini, sitakuhurumia eti ni addiction. Full stop!
 
Ulaaniwe, ufe una faida gani duniani, uchafu mtupu! Ulaaniwe tena na tena, shetani mkubwa Lusiferi mwana haramu!

Ingekua laana yako kweli inafika basi wangelaaniwa kaka zako wengi sana!! Usikurupuke, punyeto ni kawaida sana, Kama anapiga Mara moja kwa wiki mi namuona anafanya healthy masturbation.wapo wanaopuchuka Mara mbili kwa siku.
 
Back
Top Bottom