Punyeto ni nini na nini madhara yake?
Kujichua kunavyoweza kuyaathiri maisha yako! Kupiga Punyeto

Kitendo hiki cha mwanaume kujitosheleza kimapenzi kimekuwa kikiwatatiza wataalamu wengi, juu ya kufikia umoja wa hoja kuhusu madhara yampatayo mtu ajifanyiaye mchezo huo. Kuna baadhi ya wanasaikolojia akiwemo Muaustralia Wilhelm Reich wanaeleza katika makala zao kuwa hakuna madhara kwa mtu kujichua mwenyewe.


Lakini katika hali ya kawaida ushahidi mwingi uliotolewa na wahusika wa kitendo hicho umeonyesha kuwa, wanaume wafanyao mchezo huo, hukabiliwa hatimaye na maumivu ya kichwa na upungufu mkubwa wa nguvu za kiume sambamba na kupoteza msisimko wa kimahaba, hasa wakutanapo na wapenzi wao.


Licha ya tafsiri ya upigaji punyeto kuwalenga zaidi wanaume, lakini kitendo cha usagaji ambacho huwahusu wanawake nacho kinaingizwa katika maana sawa na ile ya mwanaume kujitosheleza mwenyewe, isipokuwa utofauti hupatikana katika zana na namna ya kujiridhisha.


Inatajwa katika makabrasha mengi ya watafiti kwamba, viwango vya upigaji punyeto hutofautiana, lakini vijana wenye umri wa miaka 18 – 22 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule na vyuo wameelezwa kufikia kiwango cha mara 4 kwa siku na wanaozidi umri huo kwa miaka minane hugota kwenye mara 8 – 10. (Wanaosoma shule za bweni zenye wanafunzi wa jinsia moja wanaongoza kwa kufanya kitendo hiki)


Kama utata wa watalaamu ulivyo katika kulitazama suala hili, ndivyo ilivyo kwa jamii, dini na makabila pia. Kuna baadhi ya dini zinakataza kabisa waumini wake kujichua kwa imani kuwa, umwagaji chini wa bengu za uzazi ni sawa na uuaji wa mtoto ambaye mwanzo wake ni mbegu hai.


Kwa mfano utamaduni wa kabila la Hopi huko Arizona na Namu, Wogeno pamoja na lile la Sambia nchini Guinea unakichukulia kitendo hicho kama njia halali kabisa ya kumaliza matamanio.


Lakini swali linabaki kuwa, je njia hii ni salama kiasi cha kuipa nafasi kuchukua umuhimu wa tendo asili la ndoa linalojumuisha jinsia mbili tofauti? Haya ndiyo makusudi ya mada hii.


Kwa haraka lazima jibu liwe hapana, kwani ukweli unabaki kuwa upigaji punyeto usiozingatia mipaka na elimu una madhara makubwa ya kisaikolojia, ambayo tayari wahusika wameshathibitisha kukutwa nayo kwa namna moja au nyingine.


Dunia ina ushahidi wa watu ambao walikuwa na nguvu za kiume kwa kiwango kikubwa, lakini walipojikita sana katika upigaji punyeto walijikuta wakikabili matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na hadi leo wameshindwa kupata ufumbuzi wa kuondokana na kasoro hiyo.


Katika hali ya kawaida kinacholeta shida ni nguvu zinazotumika wakati mtu anayejichua anapofikia kilele cha kujitosheleza, pamoja na zana zinazotumika kujichua.


Ifahamike kuwa kuna watu wanatumia mikono mikavu kujisaga, jambo ambalo huwafanya waharibu mishipa ya fahamu inayounganisha uume na mishipa iliyopo kwenye ubongo.


Uharibifu huu humfanya mwanaume aidha apoteze msisimko wa kujamiiana au aupate kwa kiwango cha chini sana na kumfanya ashindwe kuwa imara anapokutana na mwanamke, ambaye sehemu zake nyeti huwa ni laini tofauti na mikono aliyozoea kujichua nayo.


Jambo lingine la hatari linalomkabili mtu anayejichua ni upotevu wa hisia. Wakati wa kujichua kwa mfano, ili mwanaume afike kwenye kilele, lazima akuze hisia kwa kiwango cha juu mno, pengine kupita ukweli halisi atakaokutana nao pindi atakapokuwa na mwanamke faraghani.


Mpiga punyeto hajitoshelezi mpaka amlete kwenye hisia mwanamke mrembo, amvike utundu wa kimahaba, ampe manjonjo mpaka mwenyewe atosheke na kiwango. Kwa namna hii mwanaume mwenye mazoea ya kufanya mapenzi kwenye hisia na wanawake warembo ambao hawezi kuwapata kwa hali halisi, atakapokutana na mwanamke wa wastani asiyekuwa mtundu kimapenzi, hawezi kuusisimua mwili na hivyo kujikuta uume wake ukishindwa kusimama kabisa au usimame kwa kiwango cha chini.


Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kiwango cha raha apatacho mwanaume mpiga punyeto. Kama nilivyosema hapo juu kuwa mwanaume anayepiga punyeto hukuza sana hisia, hivyo kwa kiasi hicho hicho ndicho anachoweza kupata raha anapofikia mshindo, kwa mantiki hiyo anapompata mwanamke halisi anaweza asisikie raha aliyozoea kuipata.


Kuna wanaume wengi ambao wameoa na wanafanya ngono na wake zao kila siku, lakini wakati huo huo wanajichua kujiridhisha zaidi, hili pia ni tatizo la kisaikolojia linaloweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume husika .


Madhara mengine ambayo mwanaume anayejichua mara nyingi kwa siku anaweza kukabiliana nayo ni kushindwa kuzalisha. Hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wake wa kizazi.


Kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa ulimwenguni imebainika kuwa, wanaojichua kwa kiwango hatarishi hukabiliwa na tatizo la kushindwa kuacha. Hii inatokana na ulevi wa mazoea waliojizoeza katika maisha yao.


Pamoja na ugumu huo bado watalaam wanasema kwamba uwezekano wa mtu kuacha kufanya kitendo hicho ni mkubwa endapo tu mhusika atafanya tathimini juu ya madhara tuliyotaja na hatimaye kukichukia kitendo hicho kutoka moyoni mwake.


Baada ya kuliona suala hilo kama tatizo, mtu aliyezoea kujichua anatakiwa kuanza hatua ya kuacha kwa kupunguza taratibu kiwango cha kujichua kwa siku. Hii ina maana kuwa kama alikuwa akijichua kwa mara 5 basi apunguze hadi kufikia mara tatu au mbili kwa siku.


Wakati akiendelea na zoezi hilo, mwanaume aliyedhamiria kuliweka kando wazo la kujitosheleza, anatakiwa kutafuta mwanamke ambaye anakidhi mguso wa hisia za mapenzi ndani ya ubongo wake ili amsaidie kuondoa tamaa ya mwili.
Hata hivyo, ni vema pia kuweka mkazo wa nia katika kupingana na ushawishi wa nguvu za mwili ambao hushindana na maamuzi ya moyo. Katika kuzishinda tamaa inashauriwa mwili uchoshwe kwa kazi au mazoezi.


Mwanaume anayetaka kuacha tabia hiyo anashauriwa kuepukana na hali ya kuwa upweke na kuishi ndani ya fikra za kimapenzi mapenzi, ikiwemo masuala ya kusoma na kuangalia majarida ya ngono, kuzungumzia mambo ya mapenzi zaidi na kuacha utani na kimahaba na wanawake.


Lakini pamoja na hayo yote utafiti uliofanywa mwaka 2003 na timu ya watalaamu walioongozwa na Graham Giles kutoka Chuo cha The Cancer Council cha Australia, ulibaini kuwa wanawake wanaojisaga kwa kiwango cha mara moja hadi mbili kwa siku wako kwenye nafasi kubwa ya kuepukana na kansa ya tezi ya uke.


Na kwa upande wa wanaume ambao hawajichui kwa kiwango cha zaidi ya mara 4 kwa wiki wanaweza kunufaika na upigaji punyeto kwa kupunguza mfadhaiko, kuongeza msukumo wa damu pamoja na faida zote apatazo mtu akutanaye na mwanamke kimapenzi (soma kitabu changu cha Saikolojia na Maisha kinachozungumzia kwa kina tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na jinsi ya kujitibu).




Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kiwango cha raha apatacho mwanaume mpiga punyeto. Kama nilivyosema hapo awali kuwa mwanaume anayepiga punyeto hukuza sana hisia, hivyo kwa kiasi hicho hicho ndicho anachoweza kupata raha anapofikia mshindo. Kwa mantiki hiyo anapompata mwanamke halisi anaweza asisikie raha aliyozoea kuipata.


Kuna wanaume wengi ambao wameoa na wanafanya ngono na wake zao kila siku, lakini wakati huo huo wanajichua kwa lengo la kujiridhisha zaidi, hili pia ni tatizo la kisaikolojia linaloweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume husika na kuwafanya wasione umuhimu wa kuwa na wake.


Matatizo haya ni kwa uchache, lakini yapo mengine ya kiafya, ambayo ni pamoja na kuumwa na kichwa, mgongo na kupoteza nguvu za mwili, hasa kwa wale wanaojichua kwa zaidi ya mara tatu kwa siku.


Madhara mengine ambayo mwanaume anayejichua mara nyingi kwa siku anaweza kukabiliana nayo ni kushindwa kuzalisha, hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wake wa kizazi.


Kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa ulimwenguni imebainika kuwa wanaojichua kwa kiwango hatarishi hukabiliwa na tatizo la kushindwa kuacha. Hii inatokana na ulevi wa mazoea waliojizoeza katika maisha yao.


Pamoja na ugumu huo bado wataalamu wanasema kwamba uwezekano wa mtu kuacha kufanya kitendo hicho ni mkumbwa endapo tu mhusika atafanya tathmini juu ya madhara tuliyotaja na hatimaye kukichukia kitendo hicho kutoka moyoni mwake.
Baada ya kuliona suala hilo kama tatizo mtu aliyezoea kujichua anatakiwa kuanza hatua ya kuacha kwa kupunguza taratibu kiwango cha kujichua kwa siku. Hii ina maana kuwa kama alikuwa akijichua mara 5 basi apunguze hadi kufikia mara tatu, mbili, moja, kwa siku na kuelekea kutofanya hivyo kabisa.


Wakati akiendelea na zoezi hilo, mwanaume aliyedhamiria kuliweka kando wazo la kujitosheleza, anatakiwa kutafuta mwanamke ambaye anakidhi mguso wa hisia za mapenzi ndani ya ubongo.


Hata hivyo, ni vema pia kuweka mkazo wa nia katika kupingana na ushawishi wa nguvu za mwili ambao hushindana na maamuzi ya moyo. Katika kuzishinda tamaa inashauriwa mwili uchoshwe kwa kazi au mazoezi.
Mwanaume anayetaka kuacha tabia hiyo anashauriwa kuepukana na hali ya kuwa upweke na kuacha kuamsha hisia za kimapenzi kwa kusoma na kuangalia majarida ya ngono, kuzungumzia mambo ya mapenzi zaidi.


Lakini pamoja na hayo yote utafiti uliofanywa mwaka 2003 na timu ya wataalamu walioongozwa na Graham Giles kutoka Chuo cha The Cancer Council cha Australia, ulibani kuwa wanawake wanaojisaga kwa kiwango cha mara moja hadi mbili kwa siku wako kwenye nafasi kubwa ya kuepukana na kansa ya tezi ya uke.


Na kwa upande wa wanaume ambao hawajichui kwa kiwango cha zaidi ya mara 4 kwa wiki wanaweza kupata faida sawa na zinazopatikana kwa mtu kufanya mapenzi.
Nakaribisha maswali kutoka kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume, wanawake wasiohisi wakati wa tendo na wenye tatizo la kujichua. Chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/52288-kujichua-kunavyoweza-kuyaathiri-maisha-yako.html
 
piga kistaarabu mkuu like mara 1 au 2 kwa wiki lakini iwe bao moja...so bao zako 2 kwa wiki maisha yanasonga,don't overdo it..piga puli kwa afya...
 
punyeto ni dhambi. hivo elewa kuwa unatenda dhambi bila kujua. pia tatizo ni kwamba usifikilie ngono kwenye akili yako. nakushauri kama huna muke OA
kwa iyo ukioa unaacha kufikiria ngono..afu watu kibao wameoa lkn hi kitu watu wanapiga kama kawa
 
Habarini ndugu zangu. Mimi ni kijana mwenye miaka 29 sasa. nasumbuliwa na tatizo la kupiga punyeto kwa muda wa miaka 6 sasa. Nimeshajaribu njia nyingi ikiwa Kusali, kupiga mazoezi ya nguvu ya mwili, kujiweka busy ila bado nashindwa kuacha. Pamoja na kujua kwamba hii kitu ina madhara kiafya bado imeniwia vigumu kuiacha.Naombeni kwa mtu anayejua jinsi ya kuacha hii kitu anisaidie maana roho i radhi but mwili ni dhaifu.
Ahsanten waungwana.
 
haina madhara hata kidogo anayebisha aseme madhara yake humu ndani!!!!
 
kumbe wapenda kujipimia utamu lol. mwana hiyo kuacha kazi balaa
 
Ukiamua utaacha tatizo umejiendekeza na kunamipicha ya warembo utakuwa umeiload katika kichwa chako ilo ndo tatizo.dawa tafuta mke bana
 
Ndio nipo kwenye michakato wa kuoa. Ila dem mwenyewe kanipa masharti kuoana ni hadi 2014 mwishoni. Dem mwenyewe tupo nae mbali zaidi ya km1200. tunakutanaga angalau mara1 kwa miezi minne. kipindi nnachokuwa mwenyewe najitahidigi kuvumilia but nashindwa.Mbaya zaidi nikipataga hisia za huyo dem ama kuongea nae kwenye cm bac na do nae kwa njia ya nyeto
 
Kama ulivyoanza kidogokidogo anza kuacha vivyo hivyo, ikisha fikia adiction itakutesa hata wakati mwingine underpant yako ikikubana na kukusugua kidogo kama umeubana mpini utapata kichefuchefu na utashangaa unatapika mbele ya watu. madharaa yake ni makubwa zaidi mbali na makatazo ya vitabu vya dini hata kiafya is not recomended. mbona wako kibao kwa nini ukashushie bafuni kana kwamba ni ukame saaaana, au uko jeshini? unadhurumu haki ya watu.
 
Umekuwa teja wa kamchezo hako yaani your addicted to masturbation. T get out from everykind of addiction needs strong-will.
 
Habari zenu bandugu,
Once again nahitaji msaada wenu nikiamini hiki ni chuo cha mafunzo .
Jamani miaka kadhaa huko nyuma enzi za sekondari nilijikuta napenda sana huu mchezo wa punyeto(naomba kusahihishwa kwanza kama kuna jina muafaka kwa wanawake la punyeto).Enzi hizo niliamini ni njia mbadala ya kuniepusha na majaribu ya mafataki na kweli nilifanikiwa ,sasa baada ya kukua kimwili na kisaikolojia nikaachana nao kabisa huu mchezo.
Sasa kama miezi miwili hivi nimejikuta na majaribu ya kuurudia huu mchezo baada ya kua in distance love(relationship),naombezi msaada wa mawazo
(i)kuna njia yeyoye mbadala wa kuepuka hili au kama hakuna .
(ii)kuna madhara yeyote atayopata mwanamke anayejihusisha na hili,naomba nisisitize hapa nahofia zaidi madhara kwenye mahusiano yangu au ndoa hapo mbeleni if ikizoeleka hali hii maana hizi mada nazofatilia humu nyingi zimekua zikionyesha madhara upande wa pili kama kupungukiwa nguvu za kiume.sasa kuna kupungukiwa nguvu za kike au kuna madhara mengine.
Naomba ushauri toka kwa wadada kama wameexperience hii au wameweza vipi be in distance love kwa kuepuka hii kitu
Naomba ushauri kwa wanaume kama walifanikiwa kukutana na mwanamke aliyeathirika na hili tatizo I min addicted na walihandle vipi mahusiaono yao
Naomba kuwasilisha ,
NB,Kila side effect ije na constructive way forward kusolve
 
Back
Top Bottom