habari zenu ndugu zangu?
Mimi siyo kijana na wala siyo mtu mzima,naweza sema ni mtu wa makamo, nina tatizo ambalo hapo awali sikulichukulia kama linaweza kuwa naathari zozote kwangu....
Miaka ya 1991 hadi 1997 nilianza masomo ya olevel kwenye chule zetu hizi za boarding ambazo zilikuwa za jinsia moja tu ya kiume, na wakati huo ndio nilikuwa kwenye kipindi chaukuaji na kujitambua kimwili, hivyo basi kwa kutokana na madiliko ya kimwili vijana wengi shuleni pale tulikuwa na tabia ya kijichua (ponyeto) kutokana na kuona wenzangu wanapunguza makali ya ukame kwa njia hiyo na mimi nilikuwa mmoja wao na hatimae kuwa mtaalamu wa tendo hilo...
A level niliendelea na tabia hiyo hadi nilipoingia chuo na kuchanganyana na jinsia tofauti na kupata wasichana wakushirikiana nao kwenye tendo la ngono.. Japo nilipata msichana/wasichana siku weza kuacha tabia ya kujichua kwani niliona napata raha zaidi kwenye kujichua kuliko kushiriki tendo ilo na mwanamke, hivyo niliendelea na tabia hiyo na ilifikia kipindi nikishiriki tendo lile na mwanamke siridhiki hadi nikamalizie kwa kujichua.....
Baada ya kumaliza chuo niliamua kuoa, baada ya kuoa sikuweza kuachana na tabia hiyo kwani mke wangu hana pumzi za kutosha kuniimili, yeye anaridhika mapema zaidi yangu, na hawezi kwenda mzunguko zaidi ya mmoja, hivyo kitendo hicho kilinifanya speed yangu ya kujichua iongezeke, pia waifu alilifahamu jambo hilo..
Mwaka 2005, tulipata mtoto wetu wa kwanza, kutokana na mke wangu kuwa kwenye kipindi cha malezi ndio speed ya kujichua iliongezeka maradufu, yaani ilikuwa kutwa mara 3 kama vile milo,nilijichua asubuhi/mchana na usiku... Niliendelea hivyo hadi leo hii hapa sijaweza kuacha hata kupunguza kiwango cha kujichua, na usiku nisipofanya hivyo sipati usingizi kabisa.
Sasa mtoto wetu amekuwa na ana umri wa miaka 6 na toka mwaka jana tumefanya mpango wa kumtafutia mdogo wake pasipo mafanikio, na hii inatokana na kwamba mbegu zangu hazipati mda wa kukomaa ili kuweza kupevusha yai la mwanamke, nimejitahidi kuonana na madaktari wametupima na wakaona mimi na mke wangu hatuna tatizo kabisa zaidi ya kwamba niliambiwa niache kupiga ponyeto kwani mbegu zangu hazipati mda wa kukomaa, na akasema mbegu za mwanaume zinachukua zaidi ya siku 5 kuweza kukomaa ziwe nauwezo wa kupevusha yai la mwanamke
tatizo
tatizo linakuja ni kwamba siwezi kukaa zaidi ya siku mbili pasipo kufanya ponyeto, kwani nikikaa siku mbili tu bila kufanya hivyo, siwezi kulala na misuli ya miguu inakaza sana kitendo kinachonifanya nipige ponyeto atakama sitaki... Wife sasa amekuwa mkali sana anataka mtoto, na ameanza kunitolea maneno makali sana.... Hapa nilipo sijafanya hicho kitendo kwa siku nne na niko kwenye hali mbaya sana miguu inakufa ganzi mara kwa mara misuli inakaza sana hadi inakuwa taabu kwangu, kusema kweli nimejaribu mbinu nyingi sana kuacha mchezo huu kwa kushirikiana na mke wangu lakini wapi....
Hivyo basi nimeona siyo vibaya nikashare na nyie tatizo langu najua kwa njia moja au nyingine mnaweza kunisaidia kiushauri au kiutaalamu zaidi... Ushauri wenu ni muhimu zaidi ndugu zanguni, naomba kuwasilisha kwenu wanajf