Mimi ni kijana mwenye miaka 22 na huu ndio ukweli wangu kuhusu swala linalonisibu naomba msaada.
Nilivyotimiza umri wa miaka 13 ndipo nilipoanza kubalehe na nyeti yangu kuwa kubwa hapa ndipo nilipogundua kua nimebalehe.
Takribani siku zinavyokwenda na kukaa mtaani ndio nikajua kitu kinaitwa punyeto pamoja na picha za ngono. Kiukweli nikawa nafurahia sana.
Naangalia picha zile na baadae kupiga punyeto, niliendelea na michezo hiyo mpaka nikawa addicted na sikuwahi kumuwaza msichana kwani nilikuwa namuogopa. Miaka ikazidi kwenda ndipo mwaka 2009 nikaanza kuhisi utofauti.
Nikisimama uume wangu hauna nguvu na niliogopa sana. Baada ya tukio hili nikawa sina raha, nikawa naenda kwenye tiba za asili nanunua dawa lakini wapi hazikusaidia.
Nilitamani sana kuacha punyeto lakini ikawa haiwezekani kwani nikikaa hata siku tatu haziishi lazima nifanye mchezo huo.
Kwa ufupi nikawa addicted kama mlevi wa unga na nikiamka nikilala nawaza ngono tu japo nguvu sina. Nilipataga wanawake ila nikawa siwezi kusex sana sana ntafanya mara moja na saa nyingine nishindwe kabisa.
Huu ni mwaka wa tatu sina mwanamke maana wengi walinkimbia. Maisha yangu ni picha za x na nyeto.
Kila siku usiku na asubuhi lazima nifanye hivyo japo sina nguvu wala hisia kwa mwanamke ila nikiangalia x napata hisia na uume wangu husimama na hushiriki tendo la punyeto.
Huu ni mwaka wa tatu sasa mie ni punyeto tu kila siku usiku na asubuhi. Mpaka sasa kitendo hicho kimepoteza dira ya maisha yangu kwani kuna effects kibao ambazo nimezipata na natamani kulia.
1.Sina uwezo wa nguvu za kiume
2.Uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu sina
3.Japo nna umri wa miaka 22 naanza kuota kipara
4.Nachoka sana, muda mwingi nalala tu
5.Vision yangu ya macho imepungua haiko vizuri kama mwanzo
6.Nmepoteza uaminifu kwangu mwenyewe kwani najihisi nisiyestahili chochote, yaani sijiamini hata kidogo.
Mbaya zaidi sina kazi na kiuchumi siko vizuri, shuleni nilikuwa nina akili sana ila kumbe nilikua nashuka kutokana na kuvuruga kichwa ila sikujua.
Jamani punyeto ni mbaya effect yake ni ya longterm huwez kuexperience mwanzoni mpaka baada ya miaka mitano na kuendelea. Yaaani najihisi nimezeeka ama baby aliyepo katika mwili wa kijana.
Naomba msaada wenu