Putin awafuta kazi majenerali nane na pia agombana sana na taasisi ya ujasusi ya FSB

Putin awafuta kazi majenerali nane na pia agombana sana na taasisi ya ujasusi ya FSB

Putin = Magufuli; makamanda kumbe walikuwa wanaogopa kumwambia ukweli kwa sababu ya ubabe wake kwani anapenda kuambiwa yale yanayompendeza tu matokeo yake sasa wanaagizia mamluki toka Syria baada ya kuona askari wake wanaogopa kuingia kwenye miji.

Kuwafukuza hao majenerali kutazidi kushusha marali ya wapiganaji wake ambao wanazidi kupoteza maisha na zana.

Hatua watakayoingia baada ya hapa ndio itakuwa balaa kwa warusi maana itakuwa ni Urban Guerrilla Warfare.
Hata hujawaza kuwa hizi ni propaganda?
 
Ngoja kwanza….ni nani aliyesema kuwa Putin kawatimua hao makamanda? Source ni nani/ nini?

Siyo Ukraine kweli waliosema hivyo?

I smell propaganda here…

Oleksiy Danilov, head of Ukraine's security council, said 'around eight' Russian commanders have been fired since the start of the conflict as Moscow scrambles to change strategy after its attempted 'shock and awe' blitz fell flat.”
Mbali na wale 8 waliouawa kwenye mapambano.

Karibu Putin atabwaga manyanga.
 
Haya maamuzi ameyafanya baada ya aibu ambayo imemkuta Ukraine, hakutegemea hivi kabisa, FSB walimshauri vibaya kwamba ataingia na kuchakaza kwa siku chache na kumaliza mchezo, leo mambo yameshindikana, amepoteza wanajeshi, vifaru, mindege na zana zingine nyingi tu na bado Kiev inazdi kumtunishia misuli hadi ametishia kutumia nyuklia, ila hapo pa nyuklia ndipo amesubiriwa sana, siku akizifyatua, atakachofanyiwa kitatumika kama funzo kwa Iran na Korea Kaskazini na mataifa yote ambayo hutishia tishia mambo ya nyuklia.

=======

  • Eight Russian generals sacked over Ukraine invasion failings, Kyiv said today
  • Head of security council said Moscow has changed tactics after early defeats
  • Putin also said to be furious at secret services for misleading him over resistance
  • Moscow expected Ukrainian military to fold, but has met determined fighters

Vladimir Putin has sacked his top generals and is 'raging' at the FSB after failed intelligence and poor strategy saw his troops handed a series of embarrassing defeats in the opening days of the war in Ukraine.

Oleksiy Danilov, head of Ukraine's security council, said 'around eight' Russian commanders have been fired since the start of the conflict as Moscow scrambles to change strategy after its attempted 'shock and awe' blitz fell flat.

Putin alikosea kumuua bwana Sergei mkuu wa Foreign Intelligence Bureau. Maana jamaa alikuwa na maoni tofauti na hiyo Vita.
 
Pro-americans & NATO be like...
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
IMG_20220312_163304.jpeg
 
Navuta subira kuchangia chochote kwa sababu vikwazo vya kiuchumi sio mara ya kwanza Russia kuwekewa.. Na bado akashinda..
Taarifa nyingi tunazopata ni propaganda za magharibi, ila reality wanaijua warussia wenyewe...
 
Hata hujawaza kuwa hizi ni propaganda?
Kwa hiyo taarifa ambazo sio propaganda ni zipi kwamba Putin aliishaiteka Ukraine kitambo ila vyombo vya habari vya magharibi ndio vimekataa kutangaza na kwamba taarifa za mamluki toka Syria pia ni propaganda za vyombo vya habari vya nchi za magharibi.
 
Ngoja kwanza….ni nani aliyesema kuwa Putin kawatimua hao makamanda? Source ni nani/ nini?

Siyo Ukraine kweli waliosema hivyo?

I smell propaganda here…

Oleksiy Danilov, head of Ukraine's security council, said 'around eight' Russian commanders have been fired since the start of the conflict as Moscow scrambles to change strategy after its attempted 'shock and awe' blitz fell flat.”
ushaona aliyepost ni mkenya ni sawasawa na classical conditioning
kenyan post= propaganda
 
Putin atakua amegundua hao viongozi Ni mamluki wanauza Raman kwa ukrain
.........Ndio afahamu kwamba hivi vita vya kishenzi ni vyake yeye na karugaruga wake, warussia hawavitaki. Putin ni mtu anayetafuta sifa za kijinga sana, ana mambo ya kiswahili sana, utafikiri sio mzungu. Bure kabisa.
 
Waswahili ni hao wanaolazimisha ushoga na taratibu zao za maisha kwa watu wengine ambao hawazitaki
 
hongera Sana kwao majenerali hao kumwekea kigingi Putin lamana halipo analotaka
 
Nlikuwa natazama aljazeera, Majeshi yako langoni la kyiv yamekaa tu yanasubiri order.
Wananchi wametaharuki, wengine wametoka wako ready kulinda mji. Kama hakutakuwa na msaada wa maana, Russia akianza mashambulizia anauchukua. Na leo kashambulia miji kdhaa kwa makombora.
mara kapumzika wanasubir order , mara leo wameshambulia miji kadhaa , Ebu rudia kusoma ulichoandika kinaeleweka kweli?
 
Kuwafukuza majenerali ni sehemu ya plan B ya Putin kwani amefanya "ovehaul" ya kila kitu.

Pia wakurugenzi wa FSB nao wamewekwa kuzuizini baada ya kugundulika kuwa majasusi wa Russia walio ndani ya Kyiv wengine ni mapandikizi au Moles wa nchi za magharibi na walikuwa wazitoa siri za kijeshi.

Vita ni ujasusi ulotukuka kama Nyerere alivyowapa kazi PK na M7 Iddi Amin akashughuliwa.

Kanali Mahfudhi alikuwa amejaa taarifa za kutosha kuweza kusonga mbele na vikozi vya JWTZ.

Sasa Russia wachukua vijana ambao wengineo ni kwasababu baba au babu alifanya kazi KGB bila kwenda vyuoni kwenye fresh talents.

Ila Russia ni watu wa kuchagama, watashinda hii vita kwa taabu kibabe.

Ila mkuu, usiamini sana hizo habari za kutoka huko Magharibi.
Hiyo ya kusema "the Russian intelligence services has been infiltrated by the western moles" sidhani kama ni kweli ila ni akina Putin kujaribu kufunika madhaifu yao ya kiutendaji. Kuna mambo makuu matatu yaliyopelekea Putin na watu wake kubugi stepu:

1. Poor planning

2. Logistical challenges

3. Morale crisis

Hayo mengine ni porojo na mbwembwe tu.
 
mara kapumzika wanasubir order , mara leo wameshambulia miji kadhaa , Ebu rudia kusoma ulichoandika kinaeleweka kweli?
Soma elewa, kyiv ndo majeshi yako nje tu yanasubiri order, huko kwingine mashambulizi ya makombora yameendelea. Sio habari za kuokoteza, nilikuwa natazama Aljazeera na wamewafanyia interview hadi wakazi wa kyiv
 
Nlikuwa natazama aljazeera, Majeshi yako langoni la kyiv yamekaa tu yanasubiri order.
Wananchi wametaharuki, wengine wametoka wako ready kulinda mji. Kama hakutakuwa na msaada wa maana, Russia akianza mashambulizia anauchukua. Na leo kashambulia miji kdhaa kwa makombora.
..... Labda bado wanawasubiri wale mamluki toka Syria waje maanake kwao ndio wanawaona kama wataalamu wa Urban Warfare. 😀😀😀
 
..... Labda bado wanawasubiri wale mamluki toka Syria waje maanake kwao ndio wanawaona kama wataalamu wa Urban Warfare. 😀😀😀
Vita ina propaganda nyingi, Ukraine wenyewe kuna mamluki wamezamia kusaidia, Uingereza ilikuwa inafuatilia mwanajeshi mmoja inasemekana ameondoka Uingereza kwenda kusaidia syria japo alizuiiwa.
We unaamini Ukraine hawasaidiwi?
 
Source ni M-Ukraine!

Halafu habari ilivyoletwa utadhani ni ya uhakika kabisa wakati siyo!

Halafu na watu hawasomi na kuelewa.

Wanasoma tu kichwa cha habari kilicho potofu halafu wanaanza kuruka ruka na kupiga vigelegele.

Ujinga mtupu.
Kwa mantiki hip Kwahio mkuu uelewa wako ni mpana kuliko wote humu?
 
Huyu Putin naona hana future kama rais wa Russia ni swala la muda tu kati ya haya mambo matatu moja litamuhusu:

1. Atapinduliwa

2. Atauwawa

3. Uchaguzi wa mwaka 2024 watamkataza asigombee

Kwa sasa "Approval Rating" yake itakuwa imeporomoka ni hakuna mfano.
 
Back
Top Bottom