Putin awafuta kazi majenerali nane na pia agombana sana na taasisi ya ujasusi ya FSB

Hata hujawaza kuwa hizi ni propaganda?
 
Mbali na wale 8 waliouawa kwenye mapambano.

Karibu Putin atabwaga manyanga.
 

Putin alikosea kumuua bwana Sergei mkuu wa Foreign Intelligence Bureau. Maana jamaa alikuwa na maoni tofauti na hiyo Vita.
 
Pro-americans & NATO be like...
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Navuta subira kuchangia chochote kwa sababu vikwazo vya kiuchumi sio mara ya kwanza Russia kuwekewa.. Na bado akashinda..
Taarifa nyingi tunazopata ni propaganda za magharibi, ila reality wanaijua warussia wenyewe...
 
Hata hujawaza kuwa hizi ni propaganda?
Kwa hiyo taarifa ambazo sio propaganda ni zipi kwamba Putin aliishaiteka Ukraine kitambo ila vyombo vya habari vya magharibi ndio vimekataa kutangaza na kwamba taarifa za mamluki toka Syria pia ni propaganda za vyombo vya habari vya nchi za magharibi.
 
ushaona aliyepost ni mkenya ni sawasawa na classical conditioning
kenyan post= propaganda
 
Putin atakua amegundua hao viongozi Ni mamluki wanauza Raman kwa ukrain
.........Ndio afahamu kwamba hivi vita vya kishenzi ni vyake yeye na karugaruga wake, warussia hawavitaki. Putin ni mtu anayetafuta sifa za kijinga sana, ana mambo ya kiswahili sana, utafikiri sio mzungu. Bure kabisa.
 
.........Ndio afahamu kwamba hivi vita vya kishenzi ni vyake yeye na karugaruga wake, warussia hawavitaki. Putin ni mtu anayetafuta sifa za kijinga sana, ana mambo ya kiswahili sana, utafikiri sio mzungu. Bure kabisa.
Waswahili ni hao wanaolazimisha ushoga na taratibu zao za maisha kwa watu wengine ambao hawazitaki
 
hongera Sana kwao majenerali hao kumwekea kigingi Putin lamana halipo analotaka
 
mara kapumzika wanasubir order , mara leo wameshambulia miji kadhaa , Ebu rudia kusoma ulichoandika kinaeleweka kweli?
 
Hiyo ya kusema "the Russian intelligence services has been infiltrated by the western moles" sidhani kama ni kweli ila ni akina Putin kujaribu kufunika madhaifu yao ya kiutendaji. Kuna mambo makuu matatu yaliyopelekea Putin na watu wake kubugi stepu:

1. Poor planning

2. Logistical challenges

3. Morale crisis

Hayo mengine ni porojo na mbwembwe tu.
 
mara kapumzika wanasubir order , mara leo wameshambulia miji kadhaa , Ebu rudia kusoma ulichoandika kinaeleweka kweli?
Soma elewa, kyiv ndo majeshi yako nje tu yanasubiri order, huko kwingine mashambulizi ya makombora yameendelea. Sio habari za kuokoteza, nilikuwa natazama Aljazeera na wamewafanyia interview hadi wakazi wa kyiv
 
..... Labda bado wanawasubiri wale mamluki toka Syria waje maanake kwao ndio wanawaona kama wataalamu wa Urban Warfare. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
..... Labda bado wanawasubiri wale mamluki toka Syria waje maanake kwao ndio wanawaona kama wataalamu wa Urban Warfare. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Vita ina propaganda nyingi, Ukraine wenyewe kuna mamluki wamezamia kusaidia, Uingereza ilikuwa inafuatilia mwanajeshi mmoja inasemekana ameondoka Uingereza kwenda kusaidia syria japo alizuiiwa.
We unaamini Ukraine hawasaidiwi?
 
Source ni M-Ukraine!

Halafu habari ilivyoletwa utadhani ni ya uhakika kabisa wakati siyo!

Halafu na watu hawasomi na kuelewa.

Wanasoma tu kichwa cha habari kilicho potofu halafu wanaanza kuruka ruka na kupiga vigelegele.

Ujinga mtupu.
Kwa mantiki hip Kwahio mkuu uelewa wako ni mpana kuliko wote humu?
 
Huyu Putin naona hana future kama rais wa Russia ni swala la muda tu kati ya haya mambo matatu moja litamuhusu:

1. Atapinduliwa

2. Atauwawa

3. Uchaguzi wa mwaka 2024 watamkataza asigombee

Kwa sasa "Approval Rating" yake itakuwa imeporomoka ni hakuna mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…