Pwani: Mashabiki wa Simba kutoka Mbeya, Wapata ajali Vigwaza!

Pwani: Mashabiki wa Simba kutoka Mbeya, Wapata ajali Vigwaza!

Pesa yao wamelipia nauli wakati wewe pesa yako kila mwisho wa wiki na mwezi unampelekea mwamposa au kuhani musa.

JITATHMINI

Mimi nasali kwa Yesu Mkuu

Sisali kanisa la Mwamposa wala Kuhani Musa wala kumuabudu Binadamu.

Mjue sana Mungu ili uwe na Amani ndivyo mema yatakavyo kupata.
Ayubu 22:21.
 
Na mwisho wa siku limekuuma, ndipo ujue hata nyie mnavyofanya huumiza hisia za watu vile vile. Mkuki kwa nguruwe..........
Uzuri mimi.sijawahi kufanya huo upuuzi na si muumini wa ushirikina na mdharau mtu yoyote anayeendekeza ushirikina awe Simba au Yanga.
 
Mbeya - Dar kisa mpira???

Tuache Ujinga watanzania.
Hizo hela muwe mnapeleka kwenye vituo vya watoto yatima
Dunia haipo kwa mfumo unaotaka wewe. Yaani watu wasipumzike, wasifurahie maisha, wasiburudike? Au wewe ni mlokole wale wa ukishangilia mpira utachomwa moto?
 
Hela mtu atafute mwenyewe halafu wewe umpangie jinsi ya kuitumia,hii mbona imekaa kimsule sukule.

Nipo hapa kwaajili ya kushauri na kuonya.

We kama unaona ushauri wangu wakuchangia watoto yatima misaada haufai.

MUNGU AKUBARIKI SANA.
 
Dunia haipo kwa mfumo unaotaka wewe. Yaani watu wasipumzike, wasifurahie maisha, wasiburudike? Au wewe ni mlokole wale wa ukishangilia mpira utachomwa moto?

Mimi pia nilikuwa mpenzi mkibwa sana wa mpira.

Lakini haikunifanya niwe mjinga.
Kushinda vijiweni kubishana.
Kuvaa nguo za kamali.
Kusafiri zaidi ya km 10 kisa mpira hapana.

Vitu vingine tuwe tunatumia akili ya kawaida tu.

MIGEMUKO YA USIMBA NA UYANGA INAPELEKEA VIFO NA AJALI ZISIZO NA MSINGI KABISA.
 
Hao jamaa hawawezi kuwasha Azam TV wakiwa mbeya na kuangalia mpira?????

Vitu vingine vya kijinga sana.....
 
UJINGA WA MTU MWEUSI.

Endekeza sana Ma mipira.

Nenda kwa Gari hadi Misri kaangalie Deby yao Alhly na Zamaleki.

Watu wanaweza kupoteza hadi Familia kisa simba na yanga, mtu anapata Ulemavu au anaacha Watoto yatima .

FICHA UJUHA
Siwezi kubishana na mtu miaka nenda rudi anatafuta ajira
 
Mimi pia nilikuwa mpenzi mkibwa sana wa mpira.
Hili ni suala lako binafsi, Naamini hukuingiliwa ulipokuwa shabiki.
Kushinda vijiweni kubishana.
Kuvaa nguo za kamali.
Kusafiri zaidi ya km 10 kisa mpira hapana.
Huyu ni wewe. Hushindi vijiweni sababu una sehemu nyingine inayokuhitaji.
Vitu vingine tuwe tunatumia akili ya kawaida tu.

MIGEMUKO YA USIMBA NA UYANGA INAPELEKEA VIFO NA AJALI ZISIZO NA MSINGI KABISA.
Wewe sema UMEOKOKA. Ndicho kilichokutokea. Mambo ya mpira, kamari ni dhambi kwako, usijifiche fiche.
 
UJINGA WA MTU MWEUSI.

Endekeza sana Ma mipira.

Nenda kwa Gari hadi Misri kaangalie Deby yao Alhly na Zamaleki.

Watu wanaweza kupoteza hadi Familia kisa simba na yanga, mtu anapata Ulemavu au anaacha Watoto yatima .

FICHA UJUHA
unataka kusema kwamba ajali zote zinasababishwa simba na yanga?
 
Hao jamaa hawawezi kuwasha Azam mbeya na kuangalia mpira?????
Kusafiri Kwa ajili ya kile unachopenda Wala sio jambo baya. Kitu ambacho napenda kukidiscourage ni hii desturi ya kusafiri usiku usiku Ili mfike siku ya mechi ikiisha muanze safari ya kurudi Kwa lengo la kupunguza gharama za hotel n.k. mechi ijumaa anzeni safari jumatano tembeeni mwendo wa usalama mnafika alhamisi mnapumzika ijumaa mnacheki game. Jumamosi mnarudi taratibu Kwa usalama. Kama bajeti haziruhusu bakini makwenu Tv zipo sio kurisk namna hii.
 
Kuna Vijana huwa wanaweka wake zao Bondi kisa simba na yanga.

Mwenye masikio na asikie.
 
Mkuu mbona akili zako finyu hivi.. wewe huna starehe au kitu unavhokipenda! Ajali huwapata watu wakiwa katika hekaheia za maisha Yao... Mshukuru Mungu upo mzima! Mpuuzi wewe!
Uko sahihi kabisa mkuu, wanapata ajali wanakwaya wakitoka kumuabudu Mungu ije kuwa hao Mashabiki. Ajali zipo kila siku na hazitozuia maisha ya kila siku kuendelea.
 
Nipo hapa kwaajili ya kushauri na kuonya.

We kama unaona ushauri wangu wakuchangia watoto yatima misaada haufai.

MUNGU AKUBARIKI SANA.
Kushauri ni jambo jema,lakini wewe unatoa hukumu kuwa wao wanachofanya ni ujinga,je kama wanatoa sadaka kama unavyoshauri inakuwa inawafunga wasifanye mambo mengine katika maisha yao?
Nipo hapa kwaajili ya kushauri na kuonya.

We kama unaona ushauri wangu wakuchangia watoto yatima misaada haufai.

MUNGU AKUBARIKI SANA.
 
Back
Top Bottom