Hapa unajitekenya mwenyewe alafu unacheka. Umrandika b
Siasa tupu. Lete kifungu kutoka kwenye quran kuwa Muhammad anajua kusoma na kuandika basi na sio hizi ngonjera.
Utaelewa tu maana sijawahi kufundisha kafiri yoyote kuhusu uislam na mtume Muhammad asielewe
Kwanza Tambua Mwalimu wa mtume Muhammad ni malaika Jibril
First time Malaika Jibril anakuja Kwa mtume Muhammad ujumbe aliyomtea ni kuhusu kusoma na kuandika
Na hapo mtume analazimishwa asome Quran aliyokuja nayo malaika Jibril Aya 5 za Kwa kwanza kushuka na mtume aliweza kuzisoma hizo aya
Quran 96:1
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
Quran 96:2
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
Quran 96:3
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
Quran 96:4
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
Quran 96:5
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
Hapa mtume anaambiwa asiwe na wasiwasi kwani atafundishwa na hato sahau
Quran 87:6
Tutakusomesha wala hutasahau,
Quran 87:7
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
Quran 87:8
Na tutakusahilishia yawe mepesi.
Na hapa mtume ndio anafundishwa kusoma
Quran 75:16
Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
Quran 75:17
Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
Quran 75:18
Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.