Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?


Hili nalo ni kweli
Binadamu ni wa ajabu sana
Nami nimekuelewa na wa hivyo ni mbaya zaidi
Na sio kumkaripia Mkuu bali ni kueleweshana tu
Hata kama unamtegemea kwa mambo mengi Basi urafiki ufe kwani yeye sio mgawa riziki
 
Nabaki nawe katika hili
 
Mkuu mbona jibu ni rahisi mpigie simu au kutana nae umwambie laivu kabisa masuala ya kumtongoza mke wangu uache.
Vipi kaka mke mwenyewe ndiye alimtega tega jamaa kwa nia 'aliwe tunda kimasihara' jamaa akaona aogope vya watu. Baada ya bidada kuhisi atamwambia mwenye mali ikabidi awahi kulisanua!!

Hawa ma delila; hususani wa siku hizi sio wa kuamini hata dakika moja.
 
Mvumilie mpaka yeye atako oa na wewe umgongee mke wake
 
Tangaza kiama kwani kuua tsh ngapi....huyo sio rafiki tena
Ni adui yako namba moja, ingekuwa sio rafiki yako ungefanyaje. Kill him immediately kabla hajageuka mwiba kwako.
Rudia kusoma upya kisa cha Adam na Eva/Hawa. Inaonekana hujajua ulimi wa wanawake. Yuko tayari ajigalagaze na kilio juu kuthibitisha hisia za maumivu huku moyoni anacheka au kinyume chake. Akiamua kukutungia uongo huchomoki. Hili ni trela tu kuna mengi nyuma ya kufunguka kuwa anatongozwa.

Siku ukiyajua yaliyotangulia utaomba mods wafute huu uzi.

Binafsi namshauri mtoa mada ajifunze utulivu. Ayajue mengi kuanzia tabia za wote wawili, achunguze hisia na lugha za miili ya wawili wao (face/facial expression) ukute jamaa nayehisiwa mwizi yuko romantic zaidi yako, anakuja na vijizawadi vya hapa na pale vidogo tu lakini vinasindikizwa na vijimaneno vitamu, mkazo wa macho, structure ya mwili na utulivu wakati wa maongezi, outings pindi haupo karibu hadi kufuli zake mama yoyo kavaa nawe hujawahi kufanya haya kwa kuyaona kawaida. Sasa jamaa anahisi mama atanogewa uwakamate au kuna mzinguano tu wa kawaida kimahusiano na kwa kuhisi mjuba utajua mama akaamua amuwahi kulinda imani ya mume.

Tusikuchoshe na ushauri, uliingia ukijua yapo, pambana.
 
Nipe dili mkuu, hela hiyo mzee
 
Huo haukuwa mtego ungekuwa mtego huyo mwanamke alikubali vipi kuhamishwa gesti, kuchukuliwa simu, kuingia chumbani na kugegeduliwa, hiyo inawezekana kweli?
Jamaa liongo hilo achana nalo
 
hii lazima niue , sitaniii huyu jamaa namuaa
 
Upo sahihi.
Mwanamke anatongozwa kila siku kama anajiheshimu atakuwa mwaminifu na atajua namna ya kukwepa mishale.

Jamaa amwambie rafiki yake najua ww na mke wangu mna mazoea ya kijinga na mmefikia hatua ambayo ni mbaya, Endeleeni tu halafu amuache jamaa aanze kujitetea. Kwenye utetezi atajua tu ni kweli mke aliyosema au kuna mengine.
 
Vile kaamua kuwahi kumharibia maana anajua siku mkukutana na rafiki yako atakueleza tabia ya mkeo wako ya kuchepuka.

Ameamua akukosanishe naye kiakili.

Mwambie mkeo nitamuuliza, ila na mkeo mkanye aache kujilengesha.

Anyways kazi za kuwatenganisha wana familia ni mwanya wa kumkaribisha shetani.

Be strong.
 
hii chaiii
 
Sahihi kabisa ndugu, unawezakuta huyo Rafiki yako alimtongoza Mkeo kwa muda mrefu mno ilihali kila akikataliwa unakuta pengine naye ni king'ang'anizi, sasa hapo utamwachia tu Mkeo aendelee kupambana na hali yake ilihali tayari ishakuwa usumbufu endelevu kwake?
 
Mkuu una hekima. Nimejifunza hapa.
 
Fata huu ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…