Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Waalimu jamani shida snaaaa...yani kakodi boda kwendaa kutoa helaa isiyokuwa yakeee
Hapana mimi sio mwalimu ila ndivyo nilivyo ukikosea tu kunitumia kuanzia buku hata ufanye nini sikurudishii humu ndani musijifanye watakatifu wengi wenu mumewakopa tala na hamukulipa hadi leo je hiyo nayo sio dhulma? Hivi mimi na viongozi wa serikali wanaofisadi pesa ya umma tuna tofauti gani? Mimi na mzinifu tuna tofauti gani? Mimi na anaecheza kamari tuna tofauti gani? Mimi na ninyi munaokesha bar tunatofauti gani? Acheni unafiki
 
mwezi wa 4 mwaka huu nilituma 650,000 kimakosa-nimekuja kukumbuka dakika 5 zimekwisha jamaa amisha toa hela.dah niliumia sana
 
Mimi kuna mtu nilimuahidi kumchangia Harusi halafu sikumchangia... kiukweli roho iliniuma Sana kila ninapo kutana nae...
Kama ningejua ningemchangia tu...
Imeniumiza kuliko hela ambayo ningemchangia
Pole mkuu,chakufanya hiiyo hela uliyoplan kumpatia nunua zawadi ya mtoto kama tayari amepata mtoto kama bado nunua hata kitenge mpelekee.
 
22/8/2022 iliingia hela kimakosa kwenye Account ya KCB 765,000/= mpka Leo sijawahi tafutwa
 
Tatizo ukute unaludisha pesa kwa kigogo Fulani ,kumbe hio pesa ni ya mfuko wa shati Alikua anamtumia kimada ya kwenda club[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Karma is real
 
Mimi nisharudisha miamala mara 2, tena wa mara ya kwanza nilikuwa apeche alolo sina mia mbovu. Lakini yule niliyemrudishia kuna siku nyingine akaja kunitumia 18,000 akasema chukua hiyo mwanangu ile siku ulinisaidia sana.

Ila kuna tukio nilipiga utotoni linaniuma. Maza alikuwa anafanya kazi mbeya, wakati wa likizo alikuja home. Siku anataka kuondoka akanituma kijiji cha karibu nikachukue ulezi kwa mama fulani ili maza aende nao Mbeya kwa mtoto wa yule mama.
Nilipofika kwa yule mama akaniminia ulezi kwenye mfuko wa rambo nikaondoka na kibaiskeli changu.
Wakati narudi ule mfuko ukatoboka ukawa unamwaga ulezi, ikabidi nisimame ili kuweka sawa.

Ndugu zangu wakati naangalia vizuri kwenye tobo, nikakuta noti za 5000 nyingi. Ikabidi niufungue ule mfuko niupige sachi wote ili nipate hela zote. Baada ya kujiridhisha kuwa sijaacha kitu, nikaanza kurudi kwa mguu hadi mahali ulezi ulipoanza kumwagika ili kutafuta kama kuna hela ilidondoka.

Ile pesa kitu cha maana nilichofanya ni kulipa ada TZS 4000 tu mwaka 2000.
 
So sad mkuu inaumiza

Hii inatupa taswira kwanini watu mioyo imegeuka haina huruma unajiuliza kwanini kumbe vyanzo ni huku

Mtu kama huyu unafikiri atamuonea huruma mwizi anaepigwa? Au wale wa tuma kwenye namba hii? Jina fulani

Mara nyingine sio kuwa tumezaliwa na roho ngumu bali dunia inazikomaza roho
 
Uaminifu ni kitu muhimu sana kwenye maisha, wazungu wanaita "honesty"tatizo Ngozi nyeusi wengi wamekosa kitu hicho kutokana na malezi.
Hii kitu sijui source ni nini

Lakini malezi sidhani kama ni sababu ikumbukwe malezi ya western people ndio tunayoyaponda kwa kuwa ni mabovu na tabia chafu zinatoka kwao

Issue ya kuwa na credibility Africa tumeshindwa , nahisi ni mapokezi kutoka kwa waliotutangulia hata mifumo ya uongozi hatuongozwi na sheria ila sheria imewekwa kama kivuli cha kusingizia. Ukiingia kwenye uongozi unakuta watu wameweka mizizi imara ambayo huwezi kuitoa kirahisi na ukijaribu utakufa wewe
 
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?

Wakala akikosea anawahi kuwapigia wenye mtandao hela inazuiwa.
Huwezi jua mazingira ya mtumaji .Unaweza tuma hela ukiwa safarini au stendi unaendelea na safar Sasa wakala utampataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…