Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Nice
 
Kuna kipindi wakati natafuta kazi nilikuwa choka mbaya..siku nikaitwa kwenye interview..sikuwa hata na jero.

Aisee naona 50K inaingia kwenye simu. Mara mhusika ananipigia kuwa kakosea. Nikamuambia nitamrudishia nikaitoa nikaenda fanya usaili.

Baada ya wiki tatu nikawa nimeajiriwa. Nikalipwa pesa ya kuhamishwa. Nikailipa ile pesa. Jamaa hakuamini. Nikamuambia ile pesa alikosea kwa kusudio la Mungu.
 
Sadaka yako ilikua ya kweli.

Sadaka zinapaswa ziwe zinatolewa kwa watu wenye uhitaji kama huyo, na sio sehwmu zisizo sahihi ambapo kuwafikia walengwa huwa ni tatizo.
Aseee sadaka ya kweli Mungu anakupa zaidi na zaidi,iliwahi nitokea mara mbili

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Ulimkarabati kama kisauti alivyomkarabati Analyse πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mungu anisamehe sana inawezakana ndo mana ridhiki zangu haziji

Watu walishawahi kosea kwangu =
150,000
95,000
80,000
Hizi 50,000 na zaidi ya mara 4

Sikuwahi kurudisha hata mia nliishia kuwablock

daah kuna mtu nakumbuka nilkosea kutuma hela kwakwe sh 52,000 ilikuwa namtumia mchepuko, nikapiga huduma kwa wateja kwasababu ile no ilikuwa Mtandao tofaut na mm.

niliambiwa nisubili masaa 72, ilikuwa jmos basi nikampigia yule jamaa nikamwambia nikosea kutuma hela kwakwe aniludishie walau 30,000 tuh, jamaa kweli akarudisha 30,000 nikamshukuru.

Nimekaa j3 sina mpango wowote naona messag ya muhamala unaiangia kwenye simu yangu hela imerudishwa, walah sikulemba nikaihamisha ile hela jamaa alipiga mara 3 sikupokea ila hakupiga tena
 
Mm nilitumiwa pesa tar.7/07/2023 nikajua ataomba muamala urudishwe Kumbe hakurudisha , Jana nikakumbuka nikampigia Simu kapokea nikamielekeza akasema Kweli nilikosea ila mm mwenye hapa nilipo nipo taaban ninaumwa kwahiyo nilishindwa hata kuirudisha hiyo pesa.Kwa nilivyokuwa naongea nae nikweli anaonekana yupo hoi,basi nimemrudishia ameshukuru kweli.

Niwaombe mtu akituma pesa kimakosa irejeshe

Sent from my Infinix X6511E using JamiiForums mobile app
 
Mimi mara 2 nilitumiwa hela Kwa makosa ...sikuigusa Hadi mhusika alipopiga simu ikarudishwa
Na huu ndio utaratibu sahihi.ukijichanganya tu wale wazee wa tuma kwenye namba hii wanapita nawewe.
 
07/07/2023??????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…