Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Dah! nilipokea 900k ya jamaa amepiga zake mchongo mkapa foundation nikaforward kama ilivyo jamaa hadi leo haamini kama nilimpa ile hela...
 
Huo ni wizi, usipende mterezo ipo siku utaaibika
Unaibikaje wakati watakatishaji wa fedha wenyewe wameamua kupitisha Mzigo wao kwenye account yako bila ruhusa yako!? Au unazani hizo fedha zimekuja tu kwa bahati mbaya!?
 
Hii mambo ya miamala bn!

Likizo moja hv mzee aliniachia office nkawa nafanya miamala jioni yy anafanya mahesabu, siku hyo mzee alinambia nimtumie mtu hela 450k nikamtumia mara ya kwanza hamna response nliyoona wala feedback nkarudia!

Jioni mzee akawa anapiga hesabu zake akanambia Kuna shoti ya 450k nkajua kbs hii imeenda kwa ile namba alonipa yeye! Nkamweleza aisee alichukia kinoma siku ya pili nikabadilishwa pa kwenda nkawa natembea na watu wa chenso tunakata miti, Kuna tawi la mti lilidondokea sehemu ya nyumba ya watu wakati tunaudondosha! Sikurudi home wiki😁
 
[emoji1787]
 
Mh!? Ndo kwanza tuko mwezi wa 6
 
Cha mtu rudisha.
Siku jamaa kaacha dollar 100 tu sio nyingi kwenye bus nikaokota.
Nirudishe nikakabidhi?
Shetani akasema hiyo hela ya bia tu kwa leo
Rara nayo mbere.
Nikatimua.
E bana miaka mi2 iliyofuata nilipoteza cm 5, Hela usiombe
 
Uwoga wako ndiyo Umasikini wako!! Hiyo ungechukua ukafanyie Mambo yako,alafu wakisanuka mnakaa chini mnaelewana kulipa Deni bila riba na kwa kuzingatia kipato chako pia!!!
Yeah mara nyingi ukiitoa alafu wakagundua makosa waliyofanya wenyewe wanakuita Tena kistaarabu tu kwenda kuelewana jinsi ya kulipa taratibu kutokana na kipato chako. Ilimtokea rafiki yangu mwalimu 2014. Walimuingizia 9Mil nikamshauri aitoe afanye yale anayoona yanafaa kwa wakati huo, wakisanuka yeye hana kosa, akaichomoa kwa awamu na kwenda kununua pikipiki 3 (Yalikuwa Ni maamuzi ya haraka haraka na ujana huu tena) akaniazima na laki 5😆
Kesho yake akapigiwa simu na branch manager, ananicheki mimi nikamwambia twende wote. Baada ya maongezi wakakubaliana wawe wanamkata kiasi kwenye mshahara wake wa ualimu. Yule cashier aliyekosea sijui walimchukulia hatua gani.
 
Mungu ana njia nyingi sana za kumpa Mtu riziki yake amtakae,Sasa fikiria Kama Mwalimu ndiyo angekua anataka mkopo wa m9 hayo mashariti na riba angepewa na Bank mwenyewe angeshindwa!!
 
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?

Wakala akikosea anawahi kuwapigia wenye mtandao hela inazuiwa.
 
We tunza meseji hiyo hela atairudisha tu.
 
Mungu ana njia nyingi sana za kumpa Mtu riziki yake amtakae,Sasa fikiria Kama Mwalimu ndiyo angekua anataka mkopo wa m9 hayo mashariti na riba angepewa na Bank mwenyewe angeshindwa!!
Kwa kipindi hicho angelipa milioni kumi na sita ikiwa ni pamoja na riba!
 
Nilikoseaga kutuma laki 8, bahati alipokea mstaafu wa Jeshi la magereza ni mtu mzito sana, kesho yake alinipa yoote pale kibo complex, imagine alitoka Gongo la mboto kwaajili yangu.
Kisha kaa na nafsi yako kisha jiulize Jr ungekua wewe ungerudisha? Alafu bakia na majibu yako
 
Huyo jamaa alikuwa mjinga alichokatakiwa kufanya ni kununua muda wa maongezi wa elfu 5 tu kwa kupitia hiyo laki 7 hapo ingekuwa imekula kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…