Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaibikaje wakati watakatishaji wa fedha wenyewe wameamua kupitisha Mzigo wao kwenye account yako bila ruhusa yako!? Au unazani hizo fedha zimekuja tu kwa bahati mbaya!?Huo ni wizi, usipende mterezo ipo siku utaaibika
[emoji28]Mimi ni mstaafu wa jeshi moja hapa nchini, niliwahi mrudishia mtu mmoja hela yake yote laki nane pamoja na ya kutolea niliongezea pale kibo complex
Sipendi dhuluma kabisa
[emoji1787]Hii mambo ya miamala bn!
Likizo moja hv mzee aliniachia office nkawa nafanya miamala jioni yy anafanya mahesabu, siku hyo mzee alinambia nimtumie mtu hela 450k nikamtumia mara ya kwanza hamna response nliyoona wala feedback nkarudia!
Jioni mzee akawa anapiga hesabu zake akanambia Kuna shoti ya 450k nkajua kbs hii imeenda kwa ile namba alonipa yeye! Nkamweleza aisee alichukia kinoma siku ya pili nikabadilishwa pa kwenda nkawa natembea na watu wa chenso tunakata miti, Kuna tawi la mti lilidondokea sehemu ya nyumba ya watu wakati tunaudondosha! Sikurudi home wiki[emoji16]
Mh!? Ndo kwanza tuko mwezi wa 6Mm nilitumiwa pesa tar.7/07/2023 nikajua ataomba muamala urudishwe Kumbe hakurudisha , Jana nikakumbuka nikampigia Simu kapokea nikamielekeza akasema Kweli nilikosea ila mm mwenye hapa nilipo nipo taaban ninaumwa kwahiyo nilishindwa hata kuirudisha hiyo pesa.Kwa nilivyokuwa naongea nae nikweli anaonekana yupo hoi,basi nimemrudishia ameshukuru kweli.
Niwaombe mtu akituma pesa kimakosa irejeshe
Sent from my Infinix X6511E using JamiiForums mobile app
Yeah mara nyingi ukiitoa alafu wakagundua makosa waliyofanya wenyewe wanakuita Tena kistaarabu tu kwenda kuelewana jinsi ya kulipa taratibu kutokana na kipato chako. Ilimtokea rafiki yangu mwalimu 2014. Walimuingizia 9Mil nikamshauri aitoe afanye yale anayoona yanafaa kwa wakati huo, wakisanuka yeye hana kosa, akaichomoa kwa awamu na kwenda kununua pikipiki 3 (Yalikuwa Ni maamuzi ya haraka haraka na ujana huu tena) akaniazima na laki 5😆Uwoga wako ndiyo Umasikini wako!! Hiyo ungechukua ukafanyie Mambo yako,alafu wakisanuka mnakaa chini mnaelewana kulipa Deni bila riba na kwa kuzingatia kipato chako pia!!!
Mungu ana njia nyingi sana za kumpa Mtu riziki yake amtakae,Sasa fikiria Kama Mwalimu ndiyo angekua anataka mkopo wa m9 hayo mashariti na riba angepewa na Bank mwenyewe angeshindwa!!Yeah mara nyingi ukiitoa alafu wakagundua makosa waliyofanya wenyewe wanakuita Tena kistaarabu tu kwenda kuelewana jinsi ya kulipa taratibu kutokana na kipato chako. Ilimtokea rafiki yangu mwalimu 2014. Walimuingizia 9Mil nikamshauri aitoe afanye yale anayoona yanafaa kwa wakati huo, wakisanuka yeye hana kosa, akaichomoa kwa awamu na kwenda kununua pikipiki 3 (Yalikuwa Ni maamuzi ya haraka haraka na ujana huu tena) akaniazima na laki 5[emoji38]
Kesho yake akapigiwa simu na branch manager, ananicheki mimi nikamwambia twende wote. Baada ya maongezi wakakubaliana wawe wanamkata kiasi kwenye mshahara wake wa ualimu. Yule cashier aliyekosea sijui walimchukulia hatua gani.
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?Mimi nilitumiwa kimakosa 250k alafu mbaya zaidi nipo kwenye kikao, simu na sms zikiingia simu inavibrate mimi wala sikuwa nahangaika nayo. Yule dada alipiga zaidi ya mara 20 na sms kibao mimi wala sikuwa najishugurisha na simu. Ulipofika muda wa lunch ndipo nikajiambia ngoja niangalie waliokuwa wananitafuta, gafra nakuta muamala wa laki mbili na nusu kutoka kwa wakala, pia missed calls number moja ikiwa inaongoza kunipigia mara nyingi. Nikaipiga ile number, masikini ya Mungu dada wa watu analia mama ake anaumwa sana Kigoma na mpaka muda huo ndugu wameshampigia sana simu wakimlaumu kwakuchelewesha hiyo pesa. Huruma ilinijaa, nikamwambia anipe number aliyokuwa anakusudia kuirusha hiyo pesa na kumuelewesha kuwa sikufanya makusudi kutopokea simu zake nilikuwa kwenye kikao. Yule dada alikuwa akiitikia kwa wasiwasi tu maana yalishapita zaidi ya masaa manne.
Aluponipa tu number muda huo huo nikairusha ile fedha bila kupunguza hata senti tano pamoja na kukatwa hela ya kurushia kwenye akaunti yangu. Nilipigiwa simu mpaka na ndugu zake wa huko Kigoma wakinishukuru sana na kuniombea baraka tele. Yule dada tuliendelea kuwasiliana bila kujuana baada ya muda mawasiliano yakafifia na kupotezana mpaka leo.
Somo; HUWEZI JUA HIYO PESA ILIYOKOSEWA DESTINATION IKAJA KWAKO ILITAKIWA KUFANYA NINI, KWAKUIRUDISHA UNAWEZA UKAWA UMEOKOA MAISHA YA MTU AU KUMTOA MTU KWENYE TATIZO LINALOMKABILI NA MUNGU AKAKUBARIKI.
ChaiNilikoseaga kutuma laki 8, bahati alipokea mstaafu wa Jeshi la magereza ni mtu mzito sana, kesho yake alinipa yoote pale kibo complex, imagine alitoka Gongo la mboto kwaajili yangu.
We tunza meseji hiyo hela atairudisha tu.Kuna watu wapuuzi hii dunia basi tu Uchungu nilionao Mungu ndo anajua [emoji24][emoji24]. Juzi tar 19/06/2023 Nilikua nalipia ticket yangu ya ndege off to Amsterdam muda wa booking ulikua unakaribia kuisha nimebakiza 5 minutes, fare yangu iwe cancelled nikatuma pesa mara 2, Jm travel services, muamala wa kwanza million 1 na laki 6, na wa 2 million 1 na laki 6, nimeshtuka yote imeenda message zilichelewa kurudi.
Nikapiga simu tigo nikawambia nimekosea kutuma mara 2 inatakiwa wakate muamala mmoja, imagine tigo wakathibisha miamala yote imefika kwa muhusika hawawezi kurudisha niwasiliane na Jm travel services.
Nikapiga simu nikatumiwa ticket yangu lakini muamala hawakurudisha na hapo ni jioni saa 10 na mimi Natakiwa kuondoka usiku saa 5 na KLM.
Nimepiga simu mpaka saa 2 usiku wanajibu kua wanashughulikia mpaka sasa sijapokea hela yangu, na sina uwezo wa kuwafikia jamaa namtafuta whatsp ni muhindi anasema wanashughulikia dah [emoji24][emoji24][emoji24].
Mungu yupo huyu muhindi japo sibagui watu ila nikirudi bongo ntamuwashia moto. Ndo akiba Nilikua nategemea inisaidie safarini lakini ameamua kunidhulumu sawa tu.
Note nina vielelezo vyote
Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:724726 Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 1,892,567. Muamala: 36246309377. 19/06/23 15:55.
Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:BWTAZM Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 289,167. Muamala: 86426520238. 19/06/23 15:56.
Kwa kipindi hicho angelipa milioni kumi na sita ikiwa ni pamoja na riba!Mungu ana njia nyingi sana za kumpa Mtu riziki yake amtakae,Sasa fikiria Kama Mwalimu ndiyo angekua anataka mkopo wa m9 hayo mashariti na riba angepewa na Bank mwenyewe angeshindwa!!
Kisha kaa na nafsi yako kisha jiulize Jr ungekua wewe ungerudisha? Alafu bakia na majibu yakoNilikoseaga kutuma laki 8, bahati alipokea mstaafu wa Jeshi la magereza ni mtu mzito sana, kesho yake alinipa yoote pale kibo complex, imagine alitoka Gongo la mboto kwaajili yangu.
Huyo jamaa alikuwa mjinga alichokatakiwa kufanya ni kununua muda wa maongezi wa elfu 5 tu kwa kupitia hiyo laki 7 hapo ingekuwa imekula kwakoNilikosea kutuma laki 6 kwenye namba tofauti nikampigia jamaa mwenye namba alivyopokea tu akaanza kucheka, nikamuomba anirudishie hata laki 4 akawa ananizungusha mara subiri kidogo niko sehemu mbaya nikiwa poa nitairudisha, nahisi alikuwa ana buy time akaitoe, ghafla akili ikanijia nikatumia simu nyingine kuwapigia TigoPesa wakai block ile transaction na ndio muda huohuo nahisi jamaa alikuwa ameshafika kwa wakala akanipigia anacheka akasema bahati yangu! Next day jioni pesa ikarudishwa kwenye Account yangu.