Raha ya mwanamke awe na akili za kitoto sio unakuwa na mwanamke akili nyingi mpaka anafatilia mpaka vita vya Ukraine

Muhimu tu asiwe mjuaji na mbishi, maana mtu wa namna hiyo nae hafai kuishi nae. Awe na akili, mbunifu, mwenye kuijali familia yake, awapasie watoto uwezo wake, elimu na maarifa yake.

Unaishije na kiazi ndani.
 
Mume: Mke wangu unamjua messi
Mke: Unamzungumzia huyu jirani yetu wa hapo kwa mangi. Hata hivyo simjui sana ni nani babaa

Sometimes tuvitu kama hutu tunaleta raha sana kwa baadhi ya wanaume kama mimi. Sipendi mwanamke mjuaji kupitiliza. Kuna mambo ya kike ya yeye kuyajua zaidi ila si kujua kila kitu kutoka kwenye kitu
 
Challenge ya nini katika ndoa? Ndoa sio siasa kwamba unahitaji mpizani ili ujipange vizuri. Na mke usimfanye kua business partner au consultant wa biashara zako, mke sio kitega uchumi kwa familia .
Ndiyo maana nasema unaogopa maisha.
 
Mkuu vuta picha mume wa Samia kisaikolojia ya mfumo dume anakua na wakati gani?

Ndio maana mwamba hata kwenye sherehe ambazo tunatarajia kumuoa first gentleman lakini jamaa haonekani 😂
Samia ni mke wa tatu ujue. Mwamba anaendelea na maisha poa tu hata hajui kuwa Samia hayupo nyumbani.
 
Unaogopa maisha tu.
 
Unakuta mwanamke anajua hadi kupekenyua hadi hidden files kwenye simu ya mume wake😂😂😂😂anajua hadi kwenda kutafuta picha zilizofutwa huko kwenye bin anazirudisha.😂😂
Mwanamke kasomea cyber security
 
Kwamba kuna namna moja tu ya kuishi na ikiwa haukubaliani nayo basi unaogopa maisha?
This is a logical non sequir fallacy.

Inawezekana hakuna namna moja tu ya maisha lakini ukiogopa mke mwenye akili unayaogopa maisha.

Kwanza ukizaa na mke asiye na akili unaongeza nafasi ya kuwafanya watoto wako wasiwe na akili pia.

Mwishowe unamuangalia mtoto wako amekuwa mjinga mjinga, unasema "Hapa nimepoteza mbegu tu".
 
This is alogocal non sequir fallacy.

Inawezekana hakuna namna moja tu ya maisha lakini ukiogopa mke mwenye akili unayaogopa maisha.

Kwanza ukizaa na mke asiye na akili unaongeza nafasi ya kuwafanya watoto wako wasiwe na akili pia.
Kwahiyo hata kuogopa mke asiye na akili pia ni kuyaogopa maisha kwa muktadha wa kuogopa kuwafanya watoto wako wasiwe na akili.
 
Mwanamke wa hivyo anaboa raha ya Mwanamke ajue vitu vingi mkae mbishane mcheke mfurahi , nakubadilishana mawazo🤔🤔🤔

Sio unakua na mwanamke yeye kama goigoi tu kila kitu😂
Akishika remoti ya tv basi ameweka sinema zetu..kamaliza ikifika usiku anahamisha azam 2..
 
Kweli lakini...Demu mjuaji sanaa anaboa
 
Kunatofauti kati ya mwanamke na mwanaume kila mmoja ana hulka zake

Hapa tatizo sio AKILI KUBWA bali ni mwanamke kutokua na hulka za kike na kuwa na hulka za kiume
Ni nadra sana kukuta wanawake wamekaa wenyewe wanajadili vita vya Gaza au Ukraine au wanajadili teknolojia mpya ya screen za tv au simu..... lakini haya ndio mazungumzo ya wanaume

Nyoka akiingia ndani ya nyumba ni hulka ya mwanaume kushughulika naye wakati mke na watoto wanakimbilia sehemu salama..... sio kwasababu mwanamke hawezi

Sema nivile mambo ya usawa wa kijinsia yamekuja kuvuruga kabisa huo utaratibu

Sasa kama wanawake wanasema hawajaolewa kukufulia au kukupikia unadhani wataelewa ulichoandika hapa mkuu
Hawa ndio wale wanasema mimi nikitoka out na wenzangu nampa taarifa mmewa wangu na sio kumuomba ruhusa au kumuaga

Wapo wanawake wana akili kweli kweli lakini bado wana hulka za kike
Na kuna wanawake hawana akili lakini lina hulka za kiume...... unakuta kazungukwa na wanaume wanabishana simba ya ngapa hadi ushangaa, simu anajua hadi ku root afiche mafile, social media zote anazo na maparody kibao
Just imagine kila siku yeye ndio anatoa style mpya kunako 6x6 😂😂😂😂
 
Anayeogopa mke mwenye akili anaogpa changamoto atakazozipata kuishi naye .

Anayeogopa mke asiye na akili viyi hivyo anaogopa changamoto za kuishi na watoto wajinga wajinga.

Kuna asiyeogopa maisha hapo? Yote ni sehemu ya maisha siyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…