Kunatofauti kati ya mwanamke na mwanaume kila mmoja ana hulka zake
Hapa tatizo sio AKILI KUBWA bali ni mwanamke kutokua na hulka za kike na kuwa na hulka za kiume
Ni nadra sana kukuta wanawake wamekaa wenyewe wanajadili vita vya Gaza au Ukraine au wanajadili teknolojia mpya ya screen za tv au simu..... lakini haya ndio mazungumzo ya wanaume
Nyoka akiingia ndani ya nyumba ni hulka ya mwanaume kushughulika naye wakati mke na watoto wanakimbilia sehemu salama..... sio kwasababu mwanamke hawezi
Sema nivile mambo ya usawa wa kijinsia yamekuja kuvuruga kabisa huo utaratibu
Sasa kama wanawake wanasema hawajaolewa kukufulia au kukupikia unadhani wataelewa ulichoandika hapa mkuu
Hawa ndio wale wanasema mimi nikitoka out na wenzangu nampa taarifa mmewa wangu na sio kumuomba ruhusa au kumuaga
Wapo wanawake wana akili kweli kweli lakini bado wana hulka za kike
Na kuna wanawake hawana akili lakini lina hulka za kiume...... unakuta kazungukwa na wanaume wanabishana simba ya ngapa hadi ushangaa, simu anajua hadi ku root afiche mafile, social media zote anazo na maparody kibao
Just imagine kila siku yeye ndio anatoa style mpya kunako 6x6 😂😂😂😂