Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Kikundi cha wasiojulikana inaenda kuanguka rasmi
 
Lazima tutamuongezea muda atake asitake. Hii nchi iliponywa Marchi 17.
FB_IMG_1636921569500.jpg


Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

View attachment 2010908
====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.


Yaani jamaa wanatumia hili gazeti kumtia mtu mikononi. Upepo unapimwa kwa raia kama kawaida....ajiandae kupambana na kesi au siyo.
 
Jenerali Ulimwengu ameamua rasmi hili gazeti liwe tabloid sasa kama ya Shigongo. Hakuna tena zile makala za kiuchambuzi mtu unasoma unaridhika. Sad!
Tatizo wakiandika Uchambuzi mnawafungia. Kuandika Hamza wa CCM Gazeti likala kifungo cha siku 30
 
Hilo alitumwa na JK kupunguza nguvu katiba mpya iliyokuwa imepiganiwa sana na kina Wayroba, Salim Ahmed Salim, Prof Kabudi kabla ya kuwehuka sambamba na Polepole, Judge mkuu Ramadhan, nk nk. Kwa kuwa Makonda hana akili ya kuwaza zaidi ya Leo, alikubali pia kumtukana Lowassa na pia mauaji na utesaji raia ambapo CIA wanao ushahidi kamili. Ameiba Mali za watu kuliko Sabaya na kijimilikisha. Akipona aachane na siasa aongoke kabisa!
Wachaaaaaaaaa! Kuna yule mwandishi pia aliyetoka jela kwa makubaliano na dpp naye kama alimtaja? Heehee unaweza ujutreee
 
Back
Top Bottom