Rais Abdel Al Sisi wa Egypt atoa onyo mbele ya Museveni kwamba hawataruhusu maji ya Mto Naili kuguswa na yeyote

Rais Abdel Al Sisi wa Egypt atoa onyo mbele ya Museveni kwamba hawataruhusu maji ya Mto Naili kuguswa na yeyote

Toa hoja tu boss wangu juu ya haki yetu ya kuyatumia maji hayo . Hasa kwa mataifa ya Afrika Mashariki. Lakini swala la Tanzania kutotishwa na yeyote either militarily , economically, nk ondoa kichwani.
Sisi tuna deal na Lake Victoria la hakuna wa kutuzuia.
 
Yaani wabongo bwana.. eti tuko Hadi Lebanoni!
Lebanon tuko kwa kulinda amani chini ya UN.
Pia embu tumieni akili basi Egypt haina Ballistic missiles za kutembea zaidi ya 2000km. Ina short range ballistic missiles peke yake.
Pia tambua wa kumfuata mwenzake ni Misri hapa Tanzania sio Tanzania.
Sasa jiulize wewe hiyo Misri Ina capabilities za kufunga safari kuja hadi ukanda wa Afrika mashariki kushambulia kijeshi!?
Muda mwingine panueni akili basi.
Atapitia anga lipi na atapitia marine borders zipi hadi kufikia Tanzania!?
Utambue hapo hapo ana ugomvi na Ethiopia.
Ungeniambia taifa ambalo lina air supremacy na missile powers hapo ningekuelewa.
Mathalan Iran ingekua nafasi ya Misri hapo ningekuelewa.
Nchi haina air supremacy wala missile power.
 
Watanzania hatuna hata ADS na fighter jet za kueleweka uko misri wataenda kwa miguu? Hapa ndo utajua ujinga wa Watanzania
Atakayemfuata mwenzake ni huyo Egypt sio Tanzania.
Pia hiyo Egypt haina capability ya kutoka North Afrika hadi East Afrika kamwe hawana hiyo ability.
Ni zaidi ya 3000km kutoka hapa hadi Misri. Hawana ndege hiyo ya kuruka umbali huo kutoka Misri hadi Tanzania. Pia hawana makombora ya masafa marefu hata siku moja.
Sasa jiulize wewe kwa kichwa chako huyo Misri atawezaje kumpiga Tanzania!?
Na akithubutu kutumia njia ya maji anatakiwa apite sehemu ambazo nchi zina ugomvi naye ikiwemo Somalia.
Je Kenya atamruhusu aweke manowari zake kwenye mipaka yake ya maji?
Vipi Ethiopia mwenye ugomvi naye!?
Narudia hakuna silaha ya Misri inayoweza kupiga Tanzania kwa umbali wa zaidi ya km 3000.
Ili atupige ni lazima afike TZ.
Na sasa jiulize akifika hapa kama ataachiwa.
 
Ndio hizo sheria zinaruhusu kupangia watu matumizi ya maji yaliyo kwenye mipaka yao?
Ni Mikataba ya kikanda Mkuu
Kuna makubaliano ya kimataifa, unaruhusiwa kutumia maji lakini sio kusababisha matumizi mabaya ili jirani apate shida

Zamani miaka ya 60 kulikuwa na sheria iliyotungwa lakini ilikuwa haina nguvu sana.
Ila sasa kuna sheria ngumu na lazima zifuatwe

Hata Lake Victoria imo kwenye sheria hizo na Tanzania tulisaini sheria hiyo
 
Ni Mikataba ya kikanda Mkuu
Kuna makubaliano ya kimataifa, unaruhusiwa kutumia maji lakini sio kusababisha matumizi mabaya ili jirani apate shida

Zamani miaka ya 60 kulikuwa na sheria iliyotungwa lakini ilikuwa haina nguvu sana.
Ila sasa kuna sheria ngumu na lazima zifuatwe

Hata Lake Victoria imo kwenye sheria hizo na Tanzania tulisaini sheria hiyo
Ngoja tuone.
 
Hizi ni sheria gani? Kama maji yameanza kwenye ardhi yangu, nisiruhusiwe kuyatumia ili mtu wa bondeni ayapate. Hakika nitayatumia na kiasi kinachobaki anatumia mtu wa bondeni.
Hata chanzo cha mafuta cha Iran kiko Zanzibar, hebu anzisha uchimbaji wa mafuta uone kitakavyonuka. Na ndiyo maana cheki Iran ndiyo katoa misaada mingi bongo. Yaani wese lililopo Zanzibar linaweza kuifanya Tanganyika na Zanzibar kuwa matajiri kuzidi marekani
 
Natumia na kuzuia yasiondoke. Yaani Mungu anipe maliasili halafu paka anizuie. Hiiiiii baghosha
Kama nakuona vile ungekuwa rais wa Uganda mashavu yalivyokuvimba baada ya huo ujumbe wa rais wa Egypt🤣🤣
 
Edward Ngoyai Lowasa aliwavimbia waarabu wote wanaotumia mto Nile na maji yameletwa Shinyanga, mpaka Kahama hata Tabora na Dodoma yatafika. Yule jamaa alikuwa Mwamba aloooh. Aliwaambia hatuwezi kuamuliwa maji yaliyo kwetu. Sasa hiki kizee kinakoromewa na maarabu uchwara kinanywea kama jani la mchicha mbele ya jua. Shame on Museveni.
Hasira zake kina malizia Kwa wapinzani wake🤣😅😅
 
Hana uwezo huo uyo fala.

Ila tukirudi nyuma bado maji ya ziwa Victoria nchi za weusi hatuyatumii ipasavyo kama Misri wanavyoyatumia kurutubisha uchumi na ajira kwenye taifa lao.
 
Back
Top Bottom