Rais Abdel Al Sisi wa Egypt atoa onyo mbele ya Museveni kwamba hawataruhusu maji ya Mto Naili kuguswa na yeyote

Rais Abdel Al Sisi wa Egypt atoa onyo mbele ya Museveni kwamba hawataruhusu maji ya Mto Naili kuguswa na yeyote

My Take
Tanzania ni Kati ya Nchi zilizosaini makubaliano ya Entebe kuhusu matumizi ya maji ya blonde la mto Nile, makubaliano ambayo yanapingwa vikali na Egypt.

Sasa tumejiandaa kiasi gani kuja kukabiliana na vitisho vya Egypt?
View attachment 3441320

Hao Jamaa Kwa biti wako vizuri.Pia soma Misri yasema haitakubali kupoteza hata mita moja ya ujazo ya maji Mto Nile, yaukataa Mkataba wa Entebbe | JamiiForums Misri yasema haitakubali kupoteza hata mita moja ya ujazo ya maji Mto Nile, yaukataa Mkataba wa Entebbe

View: https://www.instagram.com/reel/DNXHVdBIwng/?igsh=MTJ3eHZuYXlxOGMzNQ==

Huo mkataba waliosaini walipewa kwanza visungura ndiyo wakasaini nasikiaga tu mkataba mkataba au ndiyo ile ya kina chief mangungo wa msovero
 
Nakumbuka kwenye mtihani niliulizwa prove that EGYPT IS NILE AND NILE IS EGYPT.

Kwa kweli mto Nile ndio Kila kitu kwa Egypt,kwanini? Kwa sababu Egypt ni jangwa tupu ila imepakana na mto Nile
Huo mto kwao ndio maji ya kunywa,chakula(samaki),maji kwa ajili ya mashamba Yao nk.
 
Hizi ni sheria gani? Kama maji yameanza kwenye ardhi yangu, nisiruhusiwe kuyatumia ili mtu wa bondeni ayapate. Hakika nitayatumia na kiasi kinachobaki anatumia mtu wa bondeni.
Huo ujinga Lowasa aliukataa, akiwa PM aliamuru uvunaji wa maji toka Victoria uanze, wakati Jakaya alikuwa anaogopa baada ya kupigwa bit na Misri. Lowasa alisema Tz haitambui huo mkataba waliowekeana wamisri na wakoloni wa Tanganyika. Akasema wakamdai waliyetiliana saini. Tanzania haijwahi kuwa na mkataba wa maji na Misri. Wamisri wakanywea.
 
Huo ujinga Lowasa aliukataa, akiwa PM aliamuru uvunaji wa maji toka Victoria uanze, wakati Jakaya alikuwa anaogopa baada ya kupigwa bit na Misri. Lowasa alisema Tz haitambui huo mkataba waliowekeana wamisri na wakoloni wa Tanganyika. Akasema wakamdai waliyetiliana saini. Tanzania haijwahi kuwa na mkataba wa maji na Misri. Wamisri wakanywea.
Maji ya kunywa hayana shida bali kuyatumia Kwa miradi mikubwa kama mabwawa ya umeme na irrigation.

Nasubiria kuona jinsi Bashe atapeleka maji hayo Dom Kwa Ajili ya Kilimo Cha Umwagiliaji kama ambavyo Huwa anasema.

Unaweza sepeshwa mapema vinginevyo lazima upeleke proposal Yako kwao wakafanye assessment kwanza.
 
Ujumbe umelengwa Ethiopia na sio Uganda au Tanzania. Zamu yenu labda miaka ijayo mkionekana kuwa threat kwa Egypt kwa kuvuruga flow ya maji kwenda kwao.
Hao waarabu wa Misri wapunguze kuzaliana. Na pia waanze teknolojia ya kuyasafisha maji ya bahari ili kupunguza migogoro na ambao hawana bahari na chanzo pekee ni maji ya mito inayoingia Mto Nile. Misri wana bahari mbili kubwa (Red Sea na Mediteranian Sea). Waanze kuyasafisha kama wenzao wa Libya na Dubai walivyofanya.
 
Maisha ya Egyptians zaidi ya 120 million yanategemea R. Nile na hawana source nyingine ya maji ya uhakika. Unfortunately wao ndio wa mwisho maji kuwafikia.

Yakichezewa kwa kiwango cha kuhatarisha usalama wao watakoroma ndio.
hakika! na hili ni jambo ambalo hata kiubinaadamu tu ni la kukaa na kulijadili,kwa faida ya wote na na faida ya huo mto pia! #MajiNiUhai ila ukizama unakufa😁
 
Najua na Egypt ni Nchi ya Kikristo Coptic mmewaua hadi mmekuwa kero. na Bado kule Alexanria mnaendelea kuwaua ili waishe mmbaki nyie waislam, siku mtafushwa tu mrejee kwenu Saudia hivi nao pia ni Beguin au? hahaha
Punguza hii mentaliti yako kwa kutokujua uhalisia. Usikilize sana vya vijiweno na ondoa kabisa hisia mbaya nafsini mwako kuhusu wengine. Kwanza Misri siyo nchi ya Kiislamu, Ni Jamhuri ya Kiaarabu ya Misri. Misri wanaishi maisha kama ya Ugiriki na visiwa vya Cypus. Ni full suti na uhuru. Hadi night club zipo na maduka ya pombe yapo kwa kibali kama tu ilivyo huku kwetu lazima kuwa na leseni ya uuzaji vileo na masharti yake. Mimi nimewahi kufika na kulala na kuzurura miji karibu yote maarufu ya Misri kuanza Cairo, Alexandria na Aswan. Waarabu wa Misri hawana tofauti na wazungu kwa mtindo wao wa maisha. hamna anayebughudhiwa kuhusu ibada yake.
 
Hao waarabu wa Misri wapunguze kuzaliana. Na pia waanze teknolojia ya kuyasafisha maji ya bahari ili kupunguza migogoro na ambao hawana bahari na chanzo pekee ni maji ya mito inayoingia Mto Nile. Misri wana bahari mbili kubwa (Red Sea na Mediteranian Sea). Waanze kuyasafisha kama wenzao wa Libya na Dubai walivyofanya.
uko sahihi,lakini kumbuka,nchi ni watu sasa ukisema wasizaliane sijui kama ni sawa! na inawezekana ikawa gharama za kufanya hayo uliyopendekeza ni kubwa kuliko gharama za kuulinda huo mto! mwisho wa siku mi naoma hili si swala la kukomoana wala la kuleteana ubabe ni swala la kukaa na kukubaliana kila,mtu afaidike na hiyo rasilimali, haiwezekani jirani yako akate bomba we maji kwako yasije,kisa limeanzia kwake halafu we umuangalie tu😁🤝
 
Nimeitafuta mada hii,mtoa mada umepotosha sana.Hajasema yasiguswe na yeyote,aanachosema kuwe na matumizi kwa usawa kuzingatia kwamba wao Egypt hawana chanzo kingine,someni hapa...https://english.ahram.org.eg/NewsContent/1/1234/551101/Egypt/Foreign-Affairs/Egypt-will-never-allow-Nile-water-to-be-touched-El.aspx
 
Back
Top Bottom