Mimi sikuelewi, kwani maji yanayo zalisha umeme kutoka kwenye DAM si yanapita tu na kuingia mtoni kama kawaida hata yanayo zidi yamewekewa njia ya kutelemka kutoka juu kuingia mtoni licha ya haya maji yanayo pitia kwenye turbines za kuzalisha Umeme, Wamisri wametumia haya maji ya mto Nile kwa karne na karne kwani wao wana hati miliki ya Mto Nile hawataki Mataifa mengine wayatumie, kwa nini hawayazuii kuingia kwenye Bahari ya Mediterranean??
Wafrica wasikubali ku-entertain matakwa ya Waarabu waache Mataifa yote ambayo mto Nile unapitia nao wafaidike na mto Nile na sio wao tu kwa visingizio mbali mbali, kuna wakati niliwahi kumsokia Trump kwenye kipindi chake cha kwanza cha utawala akisema atawasaidia Wamisri kubomoa DAM la Ethiopia kwa kutumia mabom ya Bunker Busters, kisa kwa kuwa DAM lilijengwa na Wachina, hapakuwepo sababu nyingine ya msingi vingine vilikuwa ni visingizio tu, lengo hasa lilikuwa ni kupiga vita miradi iliyo jengwa na Wachina.