Hata tukienda kwa zamu viongozi waadilifu wanaweza kupatikana tu. ni zamu yetu na lazima na makamo wa rais awe na akili, sio mtu anachagua alimradi siku akija kufa anatuachia msala. chalamila alisema jambo la maana sana kipindi kile.
Zamu kwani Ikulu ni msalani ndugu mtanzania?
Zamu kwani Ikulu ni chumba cha daktari ?
Zamu kwani Ikulu ni kitanda cha kahaba?
Zamu? Nini maana ya zamu?
Zamu zimesaidia nini mpaka sasa?
Hii dhana ya zamu imetuleta hapa tulipo. We feel entitled it’s undeniably pathetic!
Kwamba kila mmoja anajiona na haki na zamu ya kuingia Ikulu and then what? Kutimiza zamu ama kuwavusha watanzania regardless ni zamu ya nani?!
Haya tunaomba ratiba ya zamu za Hindu, Buddha Non Believers ni lini kwa mujibu wa kalenda zenu?! Au ndio wamechagulishwa pande kwa lazima?! Kimya kimya?!
Mamlaka ya Urais yanatakiwa kuongozwa na watu wenye nia ya dhati kabisa ya kuwapeleka watanzania katika nchi ya ahadi.
Watu wenye maono na malengo ya kweli juu ya Tanzania ya miaka 100 ijayo na sio miaka 10 eti zamu!
Hebu tushirikiane katika ujenzi wa nchi tusonge mbele. Ubaguzi ni dhambi!
Ikulu - Nyumba kuu/ Nyumba takatifu /Nyumba ya Mkuu
Ikulu ni mahali patakatifu na sio lango la wanyang’anyi. - Mwalimu Nyerere