Hii ndio orodha ya wanasiasa na viongozi ambao ninaamini kama akampokea mikoba Rais Samia basi nchi itasonga mbele Kwa Kasi sana:
1. Mzee.Abdulrahman Kinana
2. Prof. Palamagamba Kabudi
3. Dkt Bashiru Ali Kakurwa
4. Dkt. Hussein Mwinyi
5. PM Kassim Majaliwa
Nitarudi Kwa ajili ya Part 2 kuwaelezea na kuelezea Kwanini nchi inawahitaji zaidi
Hawa wote hawafai,
Mwinyi anafanya mambo ovyo ovyo kama vile hana washauri,
1. Unguja mjini kuna masoko makuu matatu,
Soko la Kwerekwe, la Darajani na la Mombasa, soko la kwerekwe alilibomoa 2022 hadi sasa halijakamilika, soko la mombasa nalo kaliangusha chini, hala kwa miezi kadhaa soko la Darajani nalo alilifunga,
Una jiuliza huyu ni rais wa aina gani?
Je huyu ana washauri kweli?
Jenga soko la kwerekwe limekamilika lifungue, kisha jenga la Mombasa then uhamie na kuwlekeza nguvu kwenye masoko mengine mapya,
Leo hii unawatesa wafabiashara wa masoko yote, umewaweka sehemu, jua na mvua pamoja na tope ni zao,
Halafu uje umpe nchi kubwa kama Tanganyika yule?
Atauza visiwa na rasilimali zote kwa wageni.