Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Godwine

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2010
Posts
1,371
Reaction score
283
Ningependa kujua ikiwa ikatokea bahati mbaya amefariki katika ajali au namna yoyote iwayo, nani ateyeshika nafasi ya uongozi wa taifa letu?

======

37(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.
20210318_003730.jpg
20210318_003749.jpg
 
Ningependa kujua ikiwa ikatokea bahati mbaya amefariki katika ajali au namna yoyote iwayo, nani ateyeshika nafasi ya uongozi wa taifa letu?

Uko serious kuuliza the obvious? Kama ni yes basi makamu wa rais ndo atakalia kiti kwa muda utakaokuwa umebaki!
 
Ningependa kujua ikiwa ikatokea bahati mbaya amefariki katika ajali au namna yoyote iwayo, nani ateyeshika nafasi ya uongozi wa taifa letu?

Nadhani mkuu unawaandaa watu kuikubali hali iwapo punde atakufa.. nawewe ushaukwaa ushehe nini... katiba iko wazi juu ya hilo na hata na hata atakaemwachia nae akifa..chukua muda kidogo uipitie utajifunza mengi.
 
Sio siri mie amenichosha huyu Vasco!:frown::frown::frown:
 
Nadhani mkuu unawaandaa watu kuikubali hali iwapo punde atakufa.. nawewe ushaukwaa ushehe nini... katiba iko wazi juu ya hilo na hata na hata atakaemwachia nae akifa..chukua muda kidogo uipitie utajifunza mengi.

kijana lazima tujipange kwani tunaweza kukabiliwa na matatizo kwani tamaduni zetu bado zipo tusijeambiwa kwamba ni jaji mkuu au spika wa bunge tukaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, sio kwamba tunapenda tatizo litokee lakini tunatakiwa kujipanga ili tatizo likitokea basi lisilete madhara makubwa kwani tumeshaona kwenye sherehe ya muungano rais wa zanzibar alikaimu nafasi ya rais wa jamhuri katika sherehe zile mnazi mmoja isijekuwa nae pia akawa na nafasi ya kukaimu urais pindi rais wa jamhuri atapofariki ghafla, ndio maana lazima tuliweke sawa hili
 
Muuliza swali yuko sahihi kuuliza hata kama liko kwenye katiba, mambo kuandikwa kwenye katiba au vitabu si sababu ya kutouliza maswali na karibu maswali yote hutokea vitabuni, nafikiri katiba inaishia kwa watu wanne tu wanaofuatana yaani Rais--Makamu--Spika na Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa, endapo hao wote hawapo mfano wapate ajari ya ndege wakiwa pamoja katiba iko kimya nani atashika madaraka, jeshi au?....
 
..........it amounts to a treasonable offense punishable by death to compass or imagine the death of His Excellency the President of the United Republic of Tanzania!
 
..........it amounts to a treasonable offense punishable by death to compass or imagine the death of His Excellency the President of the United Republic of Tanzania!
weka ni kifungu gani kwenye katiba au act gani ili watu wakijadili kinachoweza kutoa hukumu kwa mtu kufikiri tuu au ni nchi ya kusaikika?
 
Najiuliza muuliza swali analiuliza kwa msingi gani na ana uelewa gani wa mfumo wa utawala na katiba ya Tanzania.

Jinsi swali lilivyojengwa, inaniambia wazi kuwa muuliza swali ama hajui Katiba ya Tanzania inasemaje au kaamua kutoelewa mfumo wa Serikali yetu na Katiba inavyofanya kazi inapokuja suala la Urais wa nchi.

Kama muuliza swali haelewi mfumo wa Serikali ya Tanzania na muundo wake Kikatiba na yupo hapa mwenye uwezo wa kutumia internet, basi kuna walakini katika mfumo wa elimu ya Uraia Tanzania kuwa mtu mwenye usomi na uwezo wa kutumia Internet, hafahamu na haelewi Katiba ya nchi yake inasemaje na inafananaje..

Sasa hili ni hatari ukizingatia kuwa kuna Watanzania wengi ambao hawajui haki zao na wajibu wao Kikatiba na wengine kwa makusudi hupuuzia kuelewa kilichoandikwa ndani ya katika kana kwamba vile si jukumu na kazi yao na ni ya Wanasiasa pekee. Hili ndilo linalosababisha Tanzania kuendelea kuwa Taifa linalotawaliwa na kundi fulani lilnalolinyonya Taifa na kuendeleza udumavu wa Demokrasia, Elimu na Haki za Uraia!
 
weka ni kifungu gani kwenye katiba au act gani ili watu wakijadili kinachoweza kutoa hukumu kwa mtu kufikiri tuu au ni nchi ya kusaikika?

Treason Act, 1351

teh!!! teh!!!! teh!!!
 
Twamuombea Mungu afya njema na maisha marefu rais wetu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Amen
 
Najiuliza muuliza swali analiuliza kwa msingi gani na ana uelewa gani wa mfumo wa utawala na katiba ya Tanzania.

Jinsi swali lilivyojengwa, inaniambia wazi kuwa muuliza swali ama hajui Katiba ya Tanzania inasemaje au kaamua kutoelewa mfumo wa Serikali yetu na Katiba inavyofanya kazi inapokuja suala la Urais wa nchi.

Kama muuliza swali haelewi mfumo wa Serikali ya Tanzania na muundo wake Kikatiba na yupo hapa mwenye uwezo wa kutumia internet, basi kuna walakini katika mfumo wa elimu ya Uraia Tanzania kuwa mtu mwenye usomi na uwezo wa kutumia Internet, hafahamu na haelewi Katiba ya nchi yake inasemaje na inafananaje..

Sasa hili ni hatari ukizingatia kuwa kuna Watanzania wengi ambao hawajui haki zao na wajibu wao Kikatiba na wengine kwa makusudi hupuuzia kuelewa kilichoandikwa ndani ya katika kana kwamba vile si jukumu na kazi yao na ni ya Wanasiasa pekee. Hili ndilo linalosababisha Tanzania kuendelea kuwa Taifa linalotawaliwa na kundi fulani lilnalolinyonya Taifa na kuendeleza udumavu wa Demokrasia, Elimu na Haki za Uraia!

Mchungaji naona unapotea kwa kujenga hoja juu ya mtu akiweza kutumia mawasiliano ya komputa basi atakuwa anajua katiba inasema, kwani kuna waumini wangapi ambao wanaweza kusoma na kuandika na wengine ni maprofesa na bado wanakuja kanisani kupata mafunzo kuhusu biblia , kuelimika si maana yake ni kujua kila kitu na kwa misingi hiyo basi nami ni sehemu ya jamii ambayo sijui mfumo wa ukahimu lakini najua kwa kiwango kikubwa matumizi ya kumpyuta na mifumo ya fedha . mchungaji umejenga hoja juu ya watanzania kutojua kutafsiri katiba lakini tambua ni asilimia chini ya kumi ya watanzania ndio wamepata kuiona katiba na si kuisoma kwa hiyo basi ningependa hoja yako ungeijenga kwa misingi ya ufafanusi na si mashambulizi
 
wee ukifa nani atarith familia? easy
kijana bado unaendeleza mila za kurithi? mimi nikifa familia itabaki huru kila mmoja ataendeleza shughuli zake kwa misingi niliyowawekea. sijajua swali lako linalenga nini au unadhani nchi ni mali ya familia? mfumo wa kurithi familia nadhani utaishia katika kizazi cha miaka ya 60 na kama kuna mtu anayetegemea kurithi familia ya mtu basi yuko nyuma kimawazo . kwa hiyo bado kuna sababu ya kujadili misingi ya kuchukua nafasi ya rais pindi ataposhindwa kuendelea na kazi zake kwa sababu mbali mbali ikiwemo kufa , ugonjwa na kushindwa majukumu yake kwa ujumla, lazima iwekwe wazi na ijulikana kwa watanzania wote .
 
..........it amounts to a treasonable offense punishable by death to compass or imagine the death of His Excellency the President of the United Republic of Tanzania!

Mhhh....Mkuu Kichuguu,..kwamba Rais hawezi kufikiriwa kama anaweza kufa au?
 
no comment. sijapenda kuchangia hii, namwombea asife.

Teh teh teh, lakii si inawezekana...Je kama ni mapenzi ya Mungu. Naona na wewe mkuu leo umeingia kwenye mtego,mueleweshe mleta hoja tu...Kumpa uelewa mleta Hoja,haitamfanya Rais Afe!
 
Back
Top Bottom