Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchungaji naona unapotea kwa kujenga hoja juu ya mtu akiweza kutumia mawasiliano ya komputa basi atakuwa anajua katiba inasema, kwani kuna waumini wangapi ambao wanaweza kusoma na kuandika na wengine ni maprofesa na bado wanakuja kanisani kupata mafunzo kuhusu biblia , kuelimika si maana yake ni kujua kila kitu na kwa misingi hiyo basi nami ni sehemu ya jamii ambayo sijui mfumo wa ukahimu lakini najua kwa kiwango kikubwa matumizi ya kumpyuta na mifumo ya fedha . mchungaji umejenga hoja juu ya watanzania kutojua kutafsiri katiba lakini tambua ni asilimia chini ya kumi ya watanzania ndio wamepata kuiona katiba na si kuisoma kwa hiyo basi ningependa hoja yako ungeijenga kwa misingi ya ufafanusi na si mashambulizi
Nadhani uko sahihi sehemu moja ya jibu lako na sio sahihi sehemu ya pili ya jibu.Kama ni yes basi makamu wa rais ndo atakalia kiti kwa muda utakaokuwa umebaki!
Rev. KishokaKatiba ya Tanzania imeanza kufundishwa tangu Shule za Msingi na Sekondari, enzi hizo nikisoma, unless uniambie kuwa wamefuta somo la Uraia na kufundisha Katiba kwa Watanzania.
Katiba ni kitu(kitabu) cha pili kwa Rais wa nchi yeyote baada ya ktabu cha muongozo wa kidini iwe Biblia, Kuran au Zen na mafundisho mengine yeyote ya kidini.
Kama dini inasema usiibe, Katiba nayo inasema usinyamae kimya ukiona mtu analiibia Taifa (Katiba kifungu 27).
Hivyo basi tatizo ni utashi binafsi wa kuona kuwa Katiba si kitu cha muhimu kama kukariri mambo ya kina Socrates, Nelkon na Adam Smith kama si Hemingway na Shaaban Robert.
Ndio maana Watanzania tunatawaliwa na watu tunaowachagua kwa maana tunapuuzia Katiba yetu ambayo ni muongozo na agano la kujenga na kuongoza Taofa letu. Ni uzembe huu wa kudai Katiba ni ya Wanasiasa ndio unaofanyika Makanisani na Misikitini ambapo Wafuasi wa dini huamini kuwa kusoma Biblia au Kuran na kuielewa hata kudadisi si kazi yao bali ni kazi ya Mashekhe na Wachungaji, na haishangazi kuona kuwa hata humo Makani sani na Misikitini watu wanaburuzwa tuu na kulishwa upupu mara nyingine kama Watanzania wanavyolishwa upupu (hasa Wabunge) na Wanasiasa huku Katiba iko wazi na haina ugumu wowote wa kuielewa!
Bottom line ni UVIVU wa kutaka mtu mwingine afanye kazi ya kutafakari na kuchangua na hata kuelewa kilichoandikwa kwa maana una dharau ya kuona haki yako si kitu cha kupewa kipaumbele!
Si kweli mkuu wangu Kichuguu kama ni hivyo basi cha kwanza kuadhibiwa ni katiba maana hata yenyewe imetabiri kifo cha rais tena kwa maandishi na haikuishia kwa rais tu imeendelea kwa wote wataofuata. Huu ni mpangilio wa utendaji kazi na wala si kitu cha ajabu na nchi zote huwa zinalizungumzia hilo tena kwa uwazi kabisa. Kosa litakuja tu endapo utapanga kumuua rais na ikajulikana hivyo...........it amounts to a treasonable offense punishable by death to compass or imagine the death of His Excellency the President of the United Republic of Tanzania!
Rev. Kishoka
Wakati unasoma nafikiri ulipitia darasani mtu kuuliza swali si lazima awe hajui jibu, unaweza ukauliza kwa faida ya wenzako, kwa hiyo hata godwine sina uhakika kama kweli hajui au anajua jibu la swali alilouliza lakini swali lake limetusaidia hata sisi wengine tusiojua na wale waliosahau.
Kuhusu katiba kufundishwa shuleni ni kweli inafundishwa lakini mangapi wewe uliyosoma darasa la tano au la sita au hata sekondari na chuo bado unayakumbuka, mtu unaweza ulifundishwa au hukujifunza katiba lakini ukapita muda ukawa umesahau. Mfano mzuri wa maandiko matakatifu ya biblia na koran ni mistari mingapi unaikumbuka kichwani, kama unaikumbua yote sasa kwanini kila mwisho wa wiki unaenda kanisani, vivyo hivyo na katiba ni vizuri kuwa tunajikumbusha hata kama tuliisoma darasani.
Rev KishokaLuteni,
Kuna vitu core katika Biblia na Kuran ambavyo tumevishika, same thing with Katiba. Ndio maana kila mara watu huendelea kujisomea Biblia, Kuran na wengine Katiba maana ni misingi mikuu ya Dini na Utaifa wao.
Ukisema eti si lazima kuvielewa sawa na kusema hadithi ya Juma na Rosa uliyojifunza darasa la tatu, ina maana basi mwendo ni kuburuzwa bila kujifunza ili kuelewa!
Mhhh....Mkuu Kichuguu,..kwamba Rais hawezi kufikiriwa kama anaweza kufa au?
Si kweli mkuu wangu Kichuguu kama ni hivyo basi cha kwanza kuadhibiwa ni katiba maana hata yenyewe imetabiri kifo cha rais tena kwa maandishi na haikuishia kwa rais tu imeendelea kwa wote wataofuata. Huu ni mpangilio wa utendaji kazi na wala si kitu cha ajabu na nchi zote huwa zinalizungumzia hilo tena kwa uwazi kabisa. Kosa litakuja tu endapo utapanga kumuua rais na ikajulikana hivyo.
Nadhani uko sahihi sehemu moja ya jibu lako na sio sahihi sehemu ya pili ya jibu.
1. Ni kweli kuwa Makamu wa Rais atakaimu nafasi ya Rais.
2.sio kweli kuwa atakaimu kwa muda wote uliobaki,
3. Ikitokea kwa namna yoyote ile Rais hawezi kuendelea na shughuri zake za Urais kama Kifo, ugonjwa n.k. Makamu wa rais atakaimu nafasi ya Rais na atakuwa na mamlaka kamili kama Rais. Atakaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha siku 90 (zinahesabiwa toka muda alioapishwa na jaji mkuu) Na baada ya hapo Tume ya Uchaguzi itaitisha Uchaguzi ndani ya kipindi hicho cha siku 90.
Kwa mfano Raisi akichaguliwa October 2010 na ikatokea amefariki Dec 2010 huwezi kusema kuwa Makamu wa rais atakaimu nafasi ya Rais kwa mamlaka kamili kipindi chote kilichobaki yaani January 2011 mpaka October 2015. Rais alichaguliwa kwa kura kwa kukiwakilisha chama chake na huyu alikuwa ni running mate tu.
Muuliza swali kauliza swali zuri sana tusilibeze. Kutokana na swali hili tunaweza kugenerate maswali mengine ya nyongeza ili watu tujifunze katiba yetu.
1. Kama Makamu wa Raisi amekaimishwa nafasi ya rais Je, na yeye (makamu wa rais ambaye wakati huo ni Kaimu rais) atakuwa na Makamu wake?
2. Je kama jibu ni ndio huyo makamu wake atapatikana vipi? (kwani makamu wa rais ni running mate wa mshindi wa mgombea wa kiti cha urais)
3. Ni nani atakayeweza kutangaza kuwa Rais yupo katika hali ya kutoweza kuendelea na shughuri zake? (Imagine Rais amekuwa attacked na ugonjwa ambao unaathiri utendaji kazi wa akili yake, lakini anaweza kutembea na hata kubishana, Je kuna sheria ya kumbana rais akapimwe? Je kama amelazwa kitandani ni muda au hali ipi inatosha kusema VP a-take over?) nani wa kudeclare hili? kwa vigezo vipi?
4. Uchaguzi ukiitishwa ndani ya siku 90 utahusisha nafasi ya Rais tu au serikali nzima? (Je bunge nalo litavunjwa ili uchaguzi mkuu uitishwe?)
mambo kama haya yasipotamkwa na katiba yanapotokea husababisha Vaccum na hiyo kujazwa lazima equilibrium ishake
Katiba haijaandika hivyo katiba haitaji kamati kuu ya CCM katiba huwa haitaji miundo ya vyama, katiba ikishazaliwa huwa haifi inabadilika ila chama kinazaliwa na kufa.When there is lacuna Kamati kuu ya CCM inakaa na kutuamulia mkuu kwani hujui hilo?, ndiyo maana inabidi tupigie kelele kuandikwa katiba inayolingana na mfumo tulio nao, vinginevyo ule msemo wa Chama ndiyo kina shika hatamu za uongozi wa nchi utaendelea kuwa valid mpaka pale CCM wakapo shinikizwa na wananchi kuacha mchezo wa kujitangaza washindi wa chaguzi.
Katiba ya Tanzania imeanza kufundishwa tangu Shule za Msingi na Sekondari, enzi hizo nikisoma, unless uniambie kuwa wamefuta somo la Uraia na kufundisha Katiba kwa Watanzania.
Katiba ni kitu(kitabu) cha pili kwa Rais wa nchi yeyote baada ya ktabu cha muongozo wa kidini iwe Biblia, Kuran au Zen na mafundisho mengine yeyote ya kidini.
Kama dini inasema usiibe, Katiba nayo inasema usinyamae kimya ukiona mtu analiibia Taifa (Katiba kifungu 27).
Hivyo basi tatizo ni utashi binafsi wa kuona kuwa Katiba si kitu cha muhimu kama kukariri mambo ya kina Socrates, Nelkon na Adam Smith kama si Hemingway na Shaaban Robert.
Ndio maana Watanzania tunatawaliwa na watu tunaowachagua kwa maana tunapuuzia Katiba yetu ambayo ni muongozo na agano la kujenga na kuongoza Taofa letu. Ni uzembe huu wa kudai Katiba ni ya Wanasiasa ndio unaofanyika Makanisani na Misikitini ambapo Wafuasi wa dini huamini kuwa kusoma Biblia au Kuran na kuielewa hata kudadisi si kazi yao bali ni kazi ya Mashekhe na Wachungaji, na haishangazi kuona kuwa hata humo Makani sani na Misikitini watu wanaburuzwa tuu na kulishwa upupu mara nyingine kama Watanzania wanavyolishwa upupu (hasa Wabunge) na Wanasiasa huku Katiba iko wazi na haina ugumu wowote wa kuielewa!
Bottom line ni UVIVU wa kutaka mtu mwingine afanye kazi ya kutafakari na kuchangua na hata kuelewa kilichoandikwa kwa maana una dharau ya kuona haki yako si kitu cha kupewa kipaumbele!
kuuliza sio ujinga,nchi karibia nyingi zinazoongozwa na rais,pindi rais akifa makamu wa rais ndio anachukua nafasi,kama ilivyotokea zambia mwaka uliopita nadhani
no comment. sijapenda kuchangia hii, namwombea asife.
Originally Posted by ANTIBAYOTIKI![]()
![]()
Hata kama huoni mema ya CCM bado mchango wako ni mfu!
1. Watu wote hawaitazami CCM kwa sura unayoitazama wewe
2.Hata hizo nchi unazosema za wenzetu wanaweka mambango hata kama kuna uvurundwaji mkubwa kiasi gani
3.Chadema na hata Dk Slaa wanaweza kabisa kuwa mapandikizi ya CCM wanaonufaika na udhalimu huu wa kuwachezea akili wadanganyika kwa kujifanya wako vitani kumbe sanaa tu