Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kisheria bodi ya mikopo ya elimu ya juu pekee ndiyo bodi rasmi ya serikali ya kutoa mikopo, kulingana na vigezo mbalimbali vilivyowekwa. Wako vijana wanaokosa mikopo wakati wanavyo vigezo vyote, kwanini fedha hizo zielekezwe kwa wengine ilihali ni fedha ya umma na inatolewa kwa mfumo na utaratibu maalum unaozingatia mahitaji?
Natambua kuna taasisi binafsi zinazotoa scholarship kwa wanafunzi wanaofanya vizuri, lakini taasisi hizo zinatumia fedha zake binafsi na nyingi huwa ni taasisi na kampuni za biashara zinazotumia fedha binafsi, mfano benki, Mo Dewji foundation n.k au kama ni taasisi za serikali mfano benki kuu, huwa kuna utaratibu maalum na kuanzia ngazi ya Masters
Je, fedha hizi za Samia zinatoka mfuko gani? Zinatoka kwenye mfuko wake binafsi? Kama sio, fedha hiyo inatoka wapi? Utaratibu ni upi ambao labda ni bora kuliko utaratibu ulioidhinishwa kwa sheria ya bunge?nini maana ya bodi ya mikopo HESLB?
Tunaomba maelezo kutoka wizara husika