Rais anatoa wapi fedha za kuanzisha Samia scholarship? Tuache mchezo na fedha za umma kisiasa. Fedha zirudishwe HESLB!

Hizi ndizo akili za vijana ambao ni taifa la leo na kesho! Inasikitisha sana.
 
Samia hatoi hela Zozote, ni Ushenzi na Uchawa wa viongozi kubadili jina za hizo scholarship, zilikuwepo kabla ya Samia na hata kabla ya JPM . Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya kila mwaka wanatoa hizo scholarship kwa ajili ya kufadhili postgraduate. Ushenzi wa viongozi na uchawa, kuanzia mwaka Jana hizo scholarship wakaanza kuzipa jina la Samia Scholarship….. but ni zile zile zinazotokaga kabla hata Samia hajakaribishwa Dar kutoka kizimkazi.

Utaona hata pesa za SGR , wanaziita pesa za mama zimejenga SGR, , utaseMa hizo pesa anatoa baba yake au baba Abdul . Mambo ya hovyo sana , this is the reason Africa remains cheap and poor .
 
Huyu mama amezidi kwa kweli.
 
Sasa hivi hata ufadhili wa kusomesha madaktari bingwa/bingwa bobezi umebadirishwa jina unaitwa 'Samia scholarship' wakati kipindi cha Magu kurudi nyuma ufadhili huu ulikuwepo lakini jina la Rais halikutumika. Kwa hiyo ni aina fulani ya uchwawa(viongozi wa chini wanajipendekeza kwa Rais) na pia kumpa political mileage Rais
 
Yale yale.ya EOTF ya.mama anna mkapa. Sijui imefia wapi iliwasomesha wachaga.akina temu marekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…