Rais Joe Biden awaalika Viongozi wa Africa kwa majadiliano Washington

Rais Joe Biden awaalika Viongozi wa Africa kwa majadiliano Washington

Deng Xiaoping alipomrithi Mao aliichukua China yenye uchumi uliokuwa umechoka sana kwa sera za Kijamaa, miaka ya 1980 akaufungua uchumi wa China hadi kwa makumpuni ya nje ya US, Japan na Ulaya, akalegeza mikono ya serikali katika ku control uchumi na pia akatengeneza mazingira ya sekta binafsi kufanya biashara bila bugdha nyingi za serikali China, hapo ndipo mabadiliko makubwa ya kiuchumi unayoyaona leo China yalipoanzia.
Mbona hizo sera za ujamaa hazijaharibu uchumi wa China. tatizo sisi waafrika [ watu weusi ] tuna matatizo Sana kwenye bongo zetu.
 
Hizo mbegu za mahindi ndiyo zinatoka Marekani? Hebu lete ushahidi kama ni kweli.

Bidhaa za westerners zinazozalishwa China kwa mfano Nike sisi hatuzimudu. Tunanunua feki ambazo Wachina wenyewe wametengeneza. Sasa Mmarekani anapata faida gani sisi tukinunua Nike feki au Iphone feki?
Dah, CocaCola unayokunywa imezalishwa moja kwa moja Marekani? Lakini kwa kila elfu moja ya CocaCola kuna kama mia tano hivi inamwendea mmarekani. Hata mbegu za mahindi ndivyo hivyo hivyo. Popote zinapozalishwa teknolojia ya aina ya mbegu ni ya wamagharibi na hizo mbegu unavyozinunua kila msimu kuna senti zinamnufaisha mwenye trademark.

Hilo la bidhaa za wamagharibi kutoka China kwamba hatuzimudu nisilizungumzie sana. Sidhani kama tuna uwezo wa kutofautisha kati made in China ambazo asili yake ni Marekani na made in China ambazo asili yake ni China zinazoingizwa Tanzania. Kuna watanzania wanaweza kuafford bidhaa kutoka popote pale, tena original, na hapa suala la msingi siyo product imetoka wapi au nani anafaidika. Suala la msingi ni mifumo ya uchumi wa dunia iliyoasisiwa na marekani na washirika wake ambavyo imefanya hata kale ka uwezo ketu kadogo ka ubunifu na uzalishaji kalikoanza kujengwa awamu ya Nyerere na viwanda vyake, na aina ya elimu na maarifa yaliyokuwa yakitolewa mashuleni wakati ule, kalivyofutika kabisa kabisa.

Mmarekani hapa anajitokeza kwa sababu thread inamhusu Biden na dhana ya "Power Afrika".
 
Ulaya hadi kuna vyama vya siasa vyenye mrengo wa kijamaa "social democracy" parties afu kuna watu wapo bize kusema eti ujamaa ndio ulififisha viwanda vyetu. Viwanda vyetu havikufa kwa sababu ya sera za kijamaa. Vilikufa kwa sababu watu waliopewa dhamana ya kusimamia viwanda hivyo walikuwa watu wabovu sana kupewa majukumu hayo. Who knows pengine kulikuwa na hata na sabotages za kiCIA ili kuifanye nchi iingie mrengo wa "free-market".
 
Asante Russia kwa kutueshimisha leo hii tunaalikwa sio shit hole tena USA ameona ameanza kupoteza ushawishi wake duniani ndio mahana anawaalika kabla ya Russia kufanya alichofanya ukraine ilikuwa inapigwa simu tu tena siyo na rais wa marekani bali waziri wa mambo ya nje unapewa order then una follow ukikataa wanakukatia misaada putin amewafundisha nchi nyingi kuwa west awapo kama vile walivyokuwa wanatukalilishwa yaani watu smart,grnius etc. baada ya kuona Russia amepania kuja kuwekeza na kuleta tech yake africa na wao ndio wanaamka uzuri wa sisi tanzania atufungamani na upande wowote akija Russia sawa akija USA na yeye sawa ..
Kipindi Obama anawaalika ulikuwa bado unabebwa mgongoni.
 
Another thing: westerners wameadvance sana kwenye ukoloni wao mamboleo. Hata kama kitu umenunua kutoka China au Singapore lakini mwenye kiwanda na mtaji unaweza kukuta ultimately ni mmagharibi, na hapo sijaingiza "soft-products" kibao unazowalipa bila kujijua.

Umetoa elimu kubwa kuhusu hii dhana isiyoeleweka ya outsourcing contracts, kuwa kiatu(nike), simu, engine (general motors, generators, rolls Royce)n.k zinaweza kuwa zinazalishwa mfano China lakini mmiliki ni USA, Germany au Japan n.k

Kificho hiki cha nani mmiliki umekitengua, sisi tunasema ni China ndiyo mmiliki kumbe mmiliki halisi yupo ulaya ya magharibi, Amerika ya Kaskazini au Japan.
The outsourcing of labor overseas is a natural result of the globalization of markets, and businesses' drive to cut costs to maximize profits. If workers in countries such as India or China can do the same job for a fraction of the price that domestic labor demands, those jobs will be sent abroad
 
CocaCola unayokunywa imezalishwa moja kwa moja Marekani? Lakini kwa kila elfu moja ya CocaCola kuna kama mia tano hivi inamwendea mmarekani. Hata mbegu za mahindi ndivyo hivyo hivyo. Popote zinapozalishwa teknolojia ya aina ya mbegu ni ya wamagharibi na hizo mbegu unavyozinunua kila msimu kuna senti zinamnufaisha mwenye trademark.

Hawa jamaa wa ulaya na marekani ya kaskazini pia Asia ya mbali waliona mbali sana sana.
 
Zimbabwe ilikuwa ni nchi yenye uchumi mzuri, inayozalisha na kuuza chakula na bidhaa za viwandani kwa wingi nje mpaka pale Mugabe alipoanzisha vurugu zake za mashamba na ubabe wa kisiasa.

Kenya ni nchi yenye uchumi mkubwa na mzuri kuliko nchi zote za Africa Mashariki pamoja na migogoro ya kisiasa waliyoipitia kwa muda mrefu sana.

Nchi karibia zote duniani zinakopa na zina Rushwa, hata huko China Rushwa ipo sana tu.
Kenya ni nchi isiyo faa imeoza kila sekta hakuna Cha kujifunza mapinduzi ya kimaendeleo Kenya . Hiyo nchi haina tofauti na Ghana na Nigeria . Afrika kote kumeoza hakuna Cha kujifunza kuhusu mapinduzi ya kiuchumi labda tuvuke nje ya mipaka ya Afrika na kuenda kujifunza huko Asia ya mbali na ulaya Ila Afrika inanuka uongozi mbovu kila kona.
 
Deng Xiaoping alipomrithi Mao aliichukua China yenye uchumi uliokuwa umechoka sana kwa sera za Kijamaa, miaka ya 1980 akaufungua uchumi wa China hadi kwa makumpuni ya nje ya US, Japan na Ulaya, akalegeza mikono ya serikali katika ku control uchumi na pia akatengeneza mazingira ya sekta binafsi kufanya biashara bila bugdha nyingi za serikali China, hapo ndipo mabadiliko makubwa ya kiuchumi unayoyaona leo China yalipoanzia.
Kwa hiyo unataka kusema baada ya kuingia Deng Xiaoping 1978 ndipo ujamaa ukazikwa china?🤔
 
Ma Raisi wanaojielewa hawataenda, watatuma tu wawakilishi ila kimsingi ni mtego huo wa kuona nani anaunga mkono ushoga na nani haungi mkono ili kusudi waje kuanzisha vurugumechi na kuiba rasilimali.

Siku zote tulikuwa tunafanyiwa the easy way through bogus treaties ila kwa sasa kitakachofata ni the hard ways kwa njama za vurugu wanachukuliwa kundi la walamba asali wanalambishwa buyu vurugu zinaanza kuikataa CCM biashara inaisha.[emoji23][emoji23][emoji23]
Marais wote wataenda
 
WACHAMBUZI BOBEVU WAKITANZANIA WAJITOSA KUJADILI JINSI YA NCHI KUJIKWAMUA KIUCHUMI IENDE MBELE KWA KASI

Balozi Dr. Ramadhani Dau, balozi Mohammed Mtonga, balozi Baraka Luvanda na watendaji wengine tajwa wa kitanzania kama makatibu wakuu wa wizara bara na visiwani wakichukua nafasi kama wachambuzi baada ya kuona mengi, wazungumzia kuhusu uchumi, Business Forums n.k

Masuala ya kitamaduni, geoposition, bandari kama chanzo cha ku boost GDP ya nchi, masoko makubwa, ujirani na nchi nyingi, Tanzania ijiimarishe iwe kituo kikuu cha usonara na uchongaji vito vya thamani na madini kama ilivyo Dubai UAE / Brussels Belgium vivutio vya utalii ku-boost GDP kama Singapore na Malaysia , fursa kubwa ni kujifunza mafanikio ya wengine.

Cambodia kuwa na viwanda zaidi vya nguo 500 wakati hawalimi pamba huku Tanzania ina pamba bora zaidi nyuma tu ya Egypt lakini Tanzania haitumii fursa ya pamba vilivyo, wananchi kupewa ubia ktk kilimo kikubwa kama kule Malaysia n.k

Masuala hayo mazito yajadiliwa kwa undani na kujiuliza Tanzania tumekosea wapi hadi 2020 hatupo sawa kwa ukubwa wa kiuchumi na nchi kama za Singapore au Malaysia
Source : mwanahalisi TV
 
Kusonga mbele hakuwezi kutokea kwa kubembelezana. Hao viongozi wawekewe targets wakishindwa kuzifikia watimuliwe tu ofisini.

Hakuna haja ya kufuga wezi wa kodi zetu kwa maisha ya kifalme ikiwa hawana wanaloweza kulifanya.
WACHAMBUZI BOBEVU WAKITANZANIA WAJITOSA KUJADILI JINSI YA NCHI KUJIKWAMUA KIUCHUMI IENDE MBELE KWA KASI

Dr. balozi Ramadhani Dau na wachambuzi wengine wazungumzia kuhusu uchumi, Business Council n.k

Source : mwanahalisi TV
 
Ulikuwa ni mwanzo wa kuanza kuzikwa kwa ujamaa China na katika utawala wake sera nyingi sana za kibepari ziliruhusiwa China.
Kama unasema na kuamini kuwa Deng Xiaoping alizika ujamaa China kwa kuruhusu wawekezaji. Je ni nani aliyeleta wazo na kuanzisha sera ya ujamaa wenye sifa za kichina ndani ya nchi ya China?🤔
 
Ulikuwa ni mwanzo wa kuanza kuzikwa kwa ujamaa China na katika utawala wake sera nyingi sana za kibepari ziliruhusiwa China.
slide_1.jpg
 
Hayo mambo ya Ujamaa wenye sifa za kichina ni porojo to za CCP.

Unapozungumzia mfumo uchumi wa ujamaa kuna mambo ya msingi yanayoufanya mfumo kuwa wa kijamaa. Hayo ni pamoja na serikali badala ya nguvu za soko kupanga nini kizalishwe, lini, wapi na nani, nani apate faida kiasi gani n.k Je, China inafanya hivyo kwa sasa??
Kama unasema na kuamini kuwa Deng Xiaoping alizika ujamaa China kwa kuruhusu wawekezaji. Je ni nani aliyeleta wazo na kuanzisha sera ya ujamaa wenye sifa za kichina ndani ya nchi ya China?[emoji848]
 
Back
Top Bottom