Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Kabla ya juzi mkuu wa mkoa wa Njombe alikuwa Ole Sendeka, juzi akawa Jumanne Fikha, leo Mwita Rubya!

Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais, kwa sasa aachane na haya mambo ya kutumbua na kuteuateua, afanye mambo mengine. Hayana faida yoyote kwa sisi wananchi, tumeshayachoka.
Wananchi wepi hao unaowasemea kuwa wamechoka na tumbua tumbua ya jembe magufuli? Jisemee mwenyewe,mbona Mimi sijachoka?

JPM hapendi mazoea kazini acha watu wazoee kuishi kwa maadili ya kiutumishi wa umma.
 
Mbona hata hujuwi kinacho endelea una anza laumu sibora ukae kimya. Nani kamtumbuwa? Au umeelewa nn kwenye mada some time waza postive
Lakini tuwe wakweli tu,kwani hili sio mala ya kwanza kutokea awamu hii!! Yaani hadi una toa press releases ya jina la mteuliwa ina maana kila sehemu umeshajiridhisha, ni ajabu ndani ya siku mbili tu ule uteuzi una utengua tena!!! Kuna tatizo kwenye mteuaji
 
Kafanya kazi siku mbili tu

Hahafanya kazi ndo alikua anasubiria akaape kesho Chamwino sasa anapangulua mabegi mwenzake wa Mwanza ndo anaenda Chamwino

Hii ilishawahi kutokea pia kwa Christina Mndeme na Bilinith Mahenge

Mama Mndeme alikua DC Dodoma akachaguliwa kuwa RC pale pale Dom usiku huo akaanza kujimwambafai na kuwaambia DED na watu wengine kuwa watamkoma sasa amekua Boss wao kumbe msee anasoma msg(amezitrap mwenyewe alisema) asubuh kabla ya kwenda kuapa akachenji kota Mndeme akampeleka Ruvuma na onyo kali Mahenge akamleta Dodoma
 
Hivi mkuu wa mkoa akiumwa, akiwa likizo, akisafiri mbali, mkoa unaongozwa na nani?
Kwa muundo wa kiserikali, kila kitu kinaweza kuendelea hata kama mhusika rasmi akiwa hayupo. Hakuna haraka ya kihivyo sana.

Ilikuwa ni jambo rahisi tu, serikali kutoa mwongozo katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi nini kifanyike (mfano mtu akiamua kwenda kugombea, basi aliye nyuma yake anakaimu ofisi, then mengine yatafuata upepo ukipita).

Maana kwa hali ulivyo sasa Rais anahangaika kujaza nafasi zinazoachwa wazi haraka haraka mnoo bila weredi mpana, maana anaweza kuniteua kuchukua nafasi ya fulani ambaye amekwenda kugombea ubunge sehemu fulani kumbe mimi pia niko njiani keshokutwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CUF sehemu fulani.

Mkuu wa Mkoa asipokuwepo mara nyingi anakaimisha kwa DC wa wilaya ya mjini au DC senior kuliko maDC wengine kwenye huo mkoa
 
Rais Magufuli leo July 19,2020 amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya July 17,2020 ambapo amemteua aliyekuwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Mwita kuwa RC Njombe, Mwita ameteuliwa badala ya Jumanne Fhika ambaye atabaki Ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.
View attachment 1510811
Naomba nielimishwe. Ninavyofahamu mimi vyeo vya RC na DC kama ilivyo uwaziri ni vyeo vya kisiasa na sio kiutumishi. Hawa, ukiwa sahihi, sio watumishi wa umma. Sasa mtumishi wa umma ( meneja wa Tanroads) anapoteuliwa kushika nafasi ya kisiasa ( Mkuu wa Mkoa) ina maana kuwa anachukua likizo kwenye utumishi wake wa umma? Kwa maneno mengine, atakuwa bado " permanent and pensionable"?

Amandla...
 
Ameanza sherehe kabla ya kiapo
Jumanne Fhika juzi tarehe 17/7 aliteuliwa na rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, leo tarehe 19/7 katenguliwa...

Nini sababu,
1. Amekataa?
2. Hafai?
3. Ukosefu wa umakini wakati wa kuteua? au,
4. Mteuzi kadanganywa.
 
apewae ndie aongezwae! subiri zamu yako!
Mimi cheo changu cha baba wa familia ya watoto 13 wake 2 ni kikubwa kuliko cha Urais na nilishaapishwa mara 2 nisubiri tengua teua za bongo njoo tulime matikiti huku muraaa heka moja unapata milioni 20 ukilima heka 5 zidisha hapo na ni kwa miezi 3 tu
 
Huyo mwamba katenguliwa kabla hajaapiswa, tena ndani ya siku mbili tu. Mwaka huu tutaona Mengi 😀 😀 😀
 
Mimi cheo changu cha baba wa familia ya watoto 13 wake 2 ni kikubwa kuliko cha Urais na nilishaapishwa mara 2 nisubiri tengua teua za bongo njoo tulime matikiti huku muraaa heka moja unapata milioni 20 ukilima heka 5 zidisha hapo na ni kwa miezi 3 tu
wapi
 
Back
Top Bottom